Dk. Mpango asema Serikali itaendelea kukopa hadi kieleweke

Cybergates

Cybergates

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2016
Messages
278
Likes
448
Points
80
Age
19
Cybergates

Cybergates

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2016
278 448 80
Waziri mpango ajibu hoja za wabunge kuhusu deni la taifa
"Serikali itaendelea kukopa hadi kieleweke kwa kuwa sio dhambi ikiwa fedha hizo zinakwenda kukuza uchumi"

Chanzo: Mwananchi

========

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango amewaeleza wabunge kuwa Serikali itaendelea kukopa mpaka kieleweke kwa kuwa hakuna dhambi kukopa ikiwa fedha hizo zinakwenda kukuza uchumi.

Dk Mpango amesema hayo jana Jumatatu jioni wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/19.

Kuhusu hoja kuwa Deni la Taifa linakuwa kwa kasi kubwa wakati uchumi unakua kwa kasi ndogo, Dk Mpango alisema deni hilo ni himilivu akisema baadhi ya wabunge wanashindwa kukokotoa hesabu.

Alisema Deni la Taifa liliongezeka kutoka dola 22.3 bilioni za Marekani mwaka 2016 na kufikia dola 26 bilioni ilipofika mwezi Juni 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 17.

“Deni hilo ni sawa na asilimia 31.2 ya GDP (Pato la Taifa) ikilinganishwa na ukomo wa uhimilivu wa asilimia 56. Uhimilivu wa Deni la Taifa hupimwa kwa kuzingatia uwezo wa nchi kulipa deni”

Dk Mpango alitoa takwimu za nchi za Afrika Mashariki za uhimilivu wa deni la taifa kwa nchi hizo akisema Tanzania bado iko vizuri na iko katika nafasi nzuri ya kukopesheka na wataendelea kukopa.

Alizitaja nchi hizo na uhimilivu wa deni lao kuwa ni Uganda ambayo ni asilimia 35.4, Rwanda asilimia 36.6, Burundi asilimia 43.4 na Kenya asilimia 50.4 akisema hali ni nzuri kulinganisha na nchi nyingine.

Alilinganisha nchi hizo na Zambia yenye uhimilivu wa asilimia 57.2, United Republic of Emirates asilimia 60.3, Marekani asilimia 73.8, Morocco asilimia 77 na Uingereza asilimia 92.2.

“Misri ni asilimia 92.6, Msumbiji asilimia100.3, Italia asilimia 132.5 na Ugiriki asilimia 181.6. Kwa takwimu hizi sisi bado tuna nafasi kubwa ya kukopa,”alisema Dk Mpango na kuongeza;

“Tutaendelea kukopa kwa sababu moja tu kubwa. Kwamba ni kwa ajili ya ni kukuza uwezo wetu wa baadaye wa kumudu uendeshaji wa nchi yetu na kulinda uhuru na heshima ya nchi yetu,” alisema.

“Napenda nisisitize hakuna dhambi ya nchi kukopa ilimradi nchi husika itumie fedha hizo za mkopo kukuza uwezo wa kiuchumi na kuzalisha na kurejesha hiyo mikopo,”

“Kama Rais (John Magufuli) alivyosema alivyokuwa ziarani Kagera kwa kweli tutaendelea kukopa mpaka kieleweke ilimradi Deni la Taifa tuhakikishe linaendelea kuwa himilivu.”

Kuhusu benki za biashara nchini kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa mikopo binafsi, mikopo ya biashara na mikopo ya sekta za uzalishaji, alisema hilo limetokea nchi kadhaa.

“Katika miezi 12 iliyoishia Septemba 2017, wastani wa ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi nchini Kenya ilikuwa asilimia 3.8, Tanzania asilimia 5.0, Uganda 5.2 na Rwanda asilimia 10.3.

Dk Mpango alikuwa akijibu hoja za baadhi ya wabunge kuwa amekuwa na kiburi na hana ushirikiano wa wabunge na wakati mwingine hapokei simu za wabunge wanapomtafuta kumshauri.

Kuhusu ushiriki wa sekta binafsi, Dk Mpango alikiri kuwa ndio injini ya uchumi lakini akasema zipo changamoto kiuhalisia na kusema “akili za kuambiwa tuchanganye na za kwetu”

“Akili za kuambiwa mzee Kikwete alituambia lazima tuchanganye na za kwetu kabla ya kuamua kufikia hatua ya kuwa na sekta binafsi yenye nguvu,”

“Kweli natamani sana wawekezaji wa ndani na nje watatupunguzia huu mzigo. Sekta binafsi tuliyonayo bado inahitaji kulelewa ili iweze kubeba jukumu hili.”

Mwananchi
 
T

TKNL

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Messages
624
Likes
486
Points
80
T

TKNL

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2012
624 486 80
Siasa za Tz bana! mpaka kichwa kinapata moto kwa sababu ya kizunguzungu.
 
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Messages
3,790
Likes
1,340
Points
280
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2007
3,790 1,340 280
Sasa kulikuwa na haja gani kutaka wabunge wajadili? Kama majibu wanayo
 
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
22,201
Likes
47,981
Points
280
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2016
22,201 47,981 280
Nakumbuka Rais alisema atokopa wala kuomba wahisani, ila uyu ana kiri hadharani kabisa.
 
darcity

darcity

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2009
Messages
4,112
Likes
5,847
Points
280
darcity

darcity

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2009
4,112 5,847 280
Huyu anawakilisha majibu ya Ngosha toka moyoni. Hana ujanja
 
Frank Wanjiru

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
8,599
Likes
9,957
Points
280
Frank Wanjiru

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
8,599 9,957 280
Sasa hivi hawataki kuwakopesha tena Nchi za Ulaya wao ndio wameamua kukopa?
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,407
Likes
5,796
Points
280
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,407 5,796 280
Alipoingia alikuwa majigambo na tambo za kitoto na za visasi sasa Namuona anakoeleke soon ataamua na yeye kuzipiga zile zile kupitiakwa Mayanga.....!! Ni muda tuuu!!!
 
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2017
Messages
7,520
Likes
7,748
Points
280
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2017
7,520 7,748 280

Imebak STORI tu,ni funzo kwa wengine wanaotaka hayo madaraka.
 
Auz

Auz

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2016
Messages
4,108
Likes
2,618
Points
280
Auz

Auz

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2016
4,108 2,618 280
Imebak STORI tu,ni funzo kwa wengine wanaotaka hayo madaraka.
Si unajua alisukumiwa humo wakati yeye alikuwa anajaribu tu, licha ya kwamba yeye ni mtu anayejiamini, hakujua yaliyomo huko ndani ndio maana alikuwa na tambo nyingi!
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
28,396
Likes
15,427
Points
280
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
28,396 15,427 280
Nashukuru Mungu kwetu hakuna mweye PhD maana naona Kama Hawa watu wenye PhD mi mak....
 
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2017
Messages
7,520
Likes
7,748
Points
280
SDG

SDG

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2017
7,520 7,748 280
Si unajua alisukumiwa humo wakati yeye alikuwa anajaribu tu, licha ya kwamba yeye ni mtu anayejiamini, hakujua yaliyomo huko ndani ndio maana alikuwa na tambo nyingi!
Sasa wamebak ku compare tu,mbona kenya hivi,mbona URUS vile,
Uchumi wa Marekani unawapa sababu za kukopa kwa kiwango hicho
Wanatania Hawa. Yesu mwenyewe mpaka Leo. Hajaanza kujitegemea na Ana miaka zaidi ya 2000.
Yupo kwa baba Ake.
 
M

Martin George

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Messages
1,668
Likes
1,434
Points
280
M

Martin George

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2017
1,668 1,434 280
Waziri mpango ajibu hoja za wabunge kuhusu deni la taifa
"Serikali itaendelea kukopa hadi kieleweke kwa kuwa sio dhambi ikiwa fedha hizo zinakwenda kukuza uchumi"

Chanzo: Mwananchi

========

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango amewaeleza wabunge kuwa Serikali itaendelea kukopa mpaka kieleweke kwa kuwa hakuna dhambi kukopa ikiwa fedha hizo zinakwenda kukuza uchumi.

Dk Mpango amesema hayo jana Jumatatu jioni wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2018/19.

Kuhusu hoja kuwa Deni la Taifa linakuwa kwa kasi kubwa wakati uchumi unakua kwa kasi ndogo, Dk Mpango alisema deni hilo ni himilivu akisema baadhi ya wabunge wanashindwa kukokotoa hesabu.

Alisema Deni la Taifa liliongezeka kutoka dola 22.3 bilioni za Marekani mwaka 2016 na kufikia dola 26 bilioni ilipofika mwezi Juni 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 17.

“Deni hilo ni sawa na asilimia 31.2 ya GDP (Pato la Taifa) ikilinganishwa na ukomo wa uhimilivu wa asilimia 56. Uhimilivu wa Deni la Taifa hupimwa kwa kuzingatia uwezo wa nchi kulipa deni”

Dk Mpango alitoa takwimu za nchi za Afrika Mashariki za uhimilivu wa deni la taifa kwa nchi hizo akisema Tanzania bado iko vizuri na iko katika nafasi nzuri ya kukopesheka na wataendelea kukopa.

Alizitaja nchi hizo na uhimilivu wa deni lao kuwa ni Uganda ambayo ni asilimia 35.4, Rwanda asilimia 36.6, Burundi asilimia 43.4 na Kenya asilimia 50.4 akisema hali ni nzuri kulinganisha na nchi nyingine.

Alilinganisha nchi hizo na Zambia yenye uhimilivu wa asilimia 57.2, United Republic of Emirates asilimia 60.3, Marekani asilimia 73.8, Morocco asilimia 77 na Uingereza asilimia 92.2.

“Misri ni asilimia 92.6, Msumbiji asilimia100.3, Italia asilimia 132.5 na Ugiriki asilimia 181.6. Kwa takwimu hizi sisi bado tuna nafasi kubwa ya kukopa,”alisema Dk Mpango na kuongeza;

“Tutaendelea kukopa kwa sababu moja tu kubwa. Kwamba ni kwa ajili ya ni kukuza uwezo wetu wa baadaye wa kumudu uendeshaji wa nchi yetu na kulinda uhuru na heshima ya nchi yetu,” alisema.

“Napenda nisisitize hakuna dhambi ya nchi kukopa ilimradi nchi husika itumie fedha hizo za mkopo kukuza uwezo wa kiuchumi na kuzalisha na kurejesha hiyo mikopo,”

“Kama Rais (John Magufuli) alivyosema alivyokuwa ziarani Kagera kwa kweli tutaendelea kukopa mpaka kieleweke ilimradi Deni la Taifa tuhakikishe linaendelea kuwa himilivu.”

Kuhusu benki za biashara nchini kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa mikopo binafsi, mikopo ya biashara na mikopo ya sekta za uzalishaji, alisema hilo limetokea nchi kadhaa.

“Katika miezi 12 iliyoishia Septemba 2017, wastani wa ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi nchini Kenya ilikuwa asilimia 3.8, Tanzania asilimia 5.0, Uganda 5.2 na Rwanda asilimia 10.3.

Dk Mpango alikuwa akijibu hoja za baadhi ya wabunge kuwa amekuwa na kiburi na hana ushirikiano wa wabunge na wakati mwingine hapokei simu za wabunge wanapomtafuta kumshauri.

Kuhusu ushiriki wa sekta binafsi, Dk Mpango alikiri kuwa ndio injini ya uchumi lakini akasema zipo changamoto kiuhalisia na kusema “akili za kuambiwa tuchanganye na za kwetu”

“Akili za kuambiwa mzee Kikwete alituambia lazima tuchanganye na za kwetu kabla ya kuamua kufikia hatua ya kuwa na sekta binafsi yenye nguvu,”

“Kweli natamani sana wawekezaji wa ndani na nje watatupunguzia huu mzigo. Sekta binafsi tuliyonayo bado inahitaji kulelewa ili iweze kubeba jukumu hili.”

Mwananchi
Kuna tofauti yeyote kati ya kukopa na " kutembeza bakuli"? nisaidieni jibu kiswahili kinanisumbua kidogo!
 
Forum statistics

Threads 1,236,992
Members 475,348
Posts 29,275,243