sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 649
ASICHOKIJUA Dk. Kitila Mkumbo kuhusu vyama vya siasa ni kwamba; chama tawala mara nyingi hubebwa na ukubwa wa jina na rasilimali zake, lakini vyama vya upinzani (ambavyo ni vya kiharakati), hutegemea sana ukubwa au umaarufu wa majina ya viongozi wake waasisi na wenye mvuto mkubwa kwa wananchi!
Hivi ndivyo navyoweza kuanza kujibu Makala ya Dk Kitila Mkumbo aliyoiandika kwenye gazeti moja linalomilikiwa na serikali, yenye kichwa cha habari kilichosomeka; Sumu ya Chadema ni ulevi wa umaarufu ambapo pamoja na mambo mengine, amevishutumu vyama vyote vya kisiasa nchini kwa kukosa demokrasia.
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema Dk. Kitila Mkumbo, kwenye Makala yake hiyo amesema kuwa anatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa, kulifanyia utafiti jambo hilo na kuliweka bayana kwa faida ya vizazi vyote.
Mimi siyo mtaalamu wa sayansi ya siasa, lakini napenda tu kumjibu Kitila kuwa alichokuwa amejaribu kukifanya yeye na kundi lake ndani ya Chadema hata kusababisha kufukuzwa kwake, ni matokeo ya kutokujua ni wapi na wakati gani hasa demokrasia hupaswa kutumika ndani ya chama chochote cha kisiasa.
Nasema hivyo kwa sababu siyo wakati wote demokrasia hutumika ndani ya chama cha siasa, bali hilo huja tu pale chama kinapokuwa kimeshika dola na kujiimarisha kwa rasilimali watu na pesa; hapo ndipo demokrasia hutumika baada ya chama kuwa maarufu kuliko umaarufu wa waasisi ama viongozi wake wa juu.
Mara nyingi vyama vya siasa vya upinzani kabla havijapata ridhaa ya umma kuongoza nchi, huesabiwa kama vipo kwenye harakati za kusaka uhuru, hivyo basi katika mpito huo demokrasia siyo muhimu sana, bali kinachotazamwa ni umahiri na umaarufu wa viongozi wake wa juu, katika kutetea maslahi ya wanyonge.
Vyama vingi vya kiharakati, kwa maana ya vyama vinavyopambana kushika dola, uimara na umaarufu wake mara nyingi hujengwa kupitia Imani waliyonayo watu kwa umahiri na umashuhuri wa kiongozi au muasisi wa chama hicho, wala kamwe siyo kwa sababu ya kudumisha demokrasia wala mapenzi na Imani ya wananchi kwa chama hicho!
Chama ni watu; hivyo basi watu pia humfuata mtu ndani ya chama chochote cha kisiasa anayeonekana kuwa mahiri na shupavu katika kutetea haki zao wanazoona zinabinywa na chama tawala, kwani kwao mtu kama huyo huonekana kuwa na thamani kubwa sana kuliko ukubwa wala umaarufu wa jina la chama chake!
Kinachotazamwa hapo siyo umaarufu wa jina la chama bali ni umaarufu wa jina ama majina ya viongozi wa juu wa chama, ambao wamekuwa watetezi wa haki za wanyonge kiasi cha watu kujenga Imani kubwa kwao, kuliko Imani waliyonayo kwa chama kama chama!
Mfano; wabunge kama vile John Shibuda, Maswa Magharibi (Chadema), John Cheyo, Bariadi Mashariki (UDP), Edward Lowassa, Monduli (CCM), aliyekuwa mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa n.k, hao panga pangua katika majimbo yao wana majina makubwa kuliko vyama vyao!
Leo hii watu wenye majina maarufu kama hayo, jamii inatambua mchango wao mkubwa katika kutetea haki za wanyonge hasa kwenye majimbo yao, kiasi kwamba hata wakiamua kubadili vyama, bado majina yao huendelea kubeba umaarufu mkubwa na mvuto zaidi kuliko majina ya vyama vyao!
Kumbuka hata Nelson Mandela, wananchi wa Afrika ya Kusini hawakutaka kamwe kusikia habari za demokrasia ndani ya chama cha African National Congless (ANC), walidiriki hata kumpa nafasi hiyo mkewe wakati Mandela akiwa kifungoni, bila kujali majina mengine ndani ya chama hicho.
Vivyo hivyo kwa Nyerere na TANU yake, Kaunda na UNIP, Jomo Kenyatta na KANU, Samora na FRELIMO, Mugabe na ZANU-PF n.k, wote hao wamekuwa waasisi na viongozi wa vyama vyao kwa muda mrefu, kabla na hata baada ya uhuru, kwa sababu majina yao yalikuwa maarufu kuliko yale ya vyama vyao.
Hii ndiyo kusema kuwa; vyama hivyo havikuiona nafasi ya demokrasia ndani ya uongozi wao kwa sababu siyo kwamba viongozi hao walikuwa maimla (madikteta), la, bali wananchi walikuwa na Imani kubwa ya kupata ukombozi kupitia umaarufu wa majina ya viongozi wao.
Kingine ni misimamo yao thabiti dhidi ya serikali kandamizi na sababu nyingine kuu na ya msingi ya kutokuruhusu demokrasia wakati vyama vya upinzani vikiwa kwenye harakati za kusaka ukombozi, ni kuhofia kupandikiziwa viongozi mamluki, dhahifu na wasio na uchungu na malengo ya chama ya kuwaletea wananchi ukombozi kamili!
Lakini utaratibu huo unaweza kubadilika pale tu chama kinapokuwa kimeshika dola na kujiimarisha kwa wingi wa rasilimali watu na fedha; ambapo katika mazingira kama hayo umaarufu wa chama unakuwa hautegemei tena kubebwa na umaarufu wowote wa jina la mwanachama.
Hapo ndipo demokrasia huanza kuchukua nafasi yake, ndani ya chama kwa mwanachama yoyote yule mwenye sifa na vigezo, kuweza kuruhusiwa kugombea nafasi za juu za uongozi wa chama, kwa sababu kimeshika dola na kina wingi wa rasilimali watu na pesa, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.
Ndiyo maana nasema kuwa Dk. Mkumbo na wenzake hawakujua ni majira na wakati gani hasa demokrasia inapaswa kutumika ndani ya chama; vyama vya upinzani havijashika dola yeye anataka viwe na demokrasia! Ana ajenda gani ya siri? Demokrasia hiyo ni kwa faida ya nani? Wananchi ama chama tawala!
Dk. Mkumbo anapaswa kusubiri kwanza vyama hivyo vikamate dola ndipo adai demokrasi; lakini kwa sasa asishangae kuitwa muhaini kama akina Kambona na wenzake walivyoitwa enzi hizo, kabla TANU ya Nyerere ilipokuwa bado haijakamilisha vizuri malengo yake kamili ya ukombozi wa Mtanzania.
Ndiyo maana binafsi sishangai kumuona Prof. Ibrahimu Lipumba na Maalim Seif Sharrif wakiishikilia CUF kwa muda mrefu, Slaa na Mbowe wakiikamata Chadema, Cheyo na Mbatia wakiwa na vyama vyao vya UDP na NCCR-Mageuzi, kwa sababu natambua bado wapo kwenye harakati za kusaka ukombozi.
Sikatai; viongozi wa vyama vya upinzani wanaweza kubadilishwa, lakini siyo lazima iwe kwa kutegemea mfumo wa demokrasia bali hata kwa kutegemea busara, Imani, malengo na umaarufu wa majina ya hao wanaotaka kuwa warithi, yanavyokubalika kwa wanachama na wananchi wengi bila kuathiri mwenendo wa chama.
Hivyo basi hatuwezi kudai demokrasia ndani ya vyama vya upinzani kama Kitila na wenzake wanavyodai; bali sisi tunaidai na kuihimiza zaidi demokrasia hiyo ndani ya chama tawala; huku pia tukisubiri vyama vya upinzani navyo vikamate dola ndipo tuanze kuvidai demokrasia ndani ya uongozi wao! (Ni mtazamo tu, siyo lazima uamini hivyo!)