Dk. Kitila Mkumbo, Kwanini watu makini wasianzishe chama chao?

Dk. Kitila Mkumbo, Kwanini watu makini wasianzishe chama chao?

Annuity

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Posts
338
Reaction score
198
Nimesoma makala ya Mh. Dk. Kitila Mkumbo katiaka gazeti la Raia Mwema Toleo no. 332 la Jumatano tarehe 1 Januari 2014. Katika makala yake Dk. Mkumbo alitoa ushauri wa kutokomeza ubabaishaji na ujanjaujanja katika uongozi wa siasa, na hasa aliposema kuwa watu wengi makini wanashindwa kujiunga na vyama vya siasa kulingana na hali hii.

Mfano ni pale aliposema, nanukuu.. ''Sababu ya pili, ambayo ni muhimu zaidi, ya watu makini kusita kujiunga na vyama vya siasa Tanzania ni kuogopa kuvalishwa ubabaishaji na ujanjaujanja ambao umejaa katika vyama vyetu vya siasa. Kikubwa zaidi watu wengi makini wanaogopa kupakwa matope kwa sababu siasa zetu pia zimejaa uzushi na uwongo mwingi''.

Lakini ningependa kumwambia Dk. kuwa sidhani watu makini kama ni waoga sababu wanjitambua na pia kama wanaona hizo hali mbaya katika vyama vya siasa kwa nini wakimbilie huko badala ya kuanzisha chama chao (cha watu makini) na kukiendesha kwa umakini kama walivyo,​ badala ya kuingia huko na kusababisha tafrani zinazorudisha nyuma harakati za ukombozi?

Hivyo basi ushauri wangu kwa Mkumbo hao watu makini anaodai wanakwepa kuingia kwenye vya siasa kutokana na hiyo mizengwe waungane na waanzishe chama chao nasi tutawaunga mkono kwa nguvu zote coz hao ndio tunaowahitaji Tanzania kwa sasa.
 
Apeleke unafiki huko msaliti anafanya spring doctor. Doctor mkubwa linahongwa kwa uroho wa madaraka anatufundisha nini wanafunzi wake
 
Hii ni sawa na kusema kama shule za kata si nzuri kwanini msijenge shule zenu?

Kuwa msomi hata kuwa na PhD ndiyo sifa za kiogozi makini?

Kapuya ni Professor lkn si ndiye huyu analawiti na kubaka mayatima na under age?
 
Ajiulize na ajijibu mwenyewe,yeye ndiye SI unit.Kwa nini pamoja na usomi wake alikubali kuchakachua viti maalumu mpaka kina Joyce ni wabunge,yule mama hadi akahamia NCCR?Kwa nini alikubali kutumiwa na mbowe?si angejitambua mapema akajitoa
 
Dr. Mkumbo sio Mwanasiasa yeye ni POLITICAL OPPORTUNIST like many in our GVT; Kuanzisha CHAMA sio DEMOKRASIA ya kupata hizo KURA...

Kupata Kura za Wananchi sio lazima UWE MTU MAKINI... aligombea UDIWANI kijijini kwake - pamoja na Ph.D yake na Umakini wake... aliangushwa na Jamaa aliyemaliza Darasa la Saba; Jamaa wa CCM...

Kwahiyo UKIDHANI wasomi - WATU MAKINI wanaweza kuanzisha CHAMA na kuwa Makini kwa WANANCHI -- MSAHAU
Wako wapi wale waalimu wa CHUO KIKUU wengine walikuwa na Ph.D's za HISABATI??? Waliotaka URAIS ??
Wako wapi wale wakina CHE-MPONDA - Ma Professor... Jukwaani hawakuweza hata kualika watoto wanaocheza SEMBO kuwasikiliza...

Kama hataweza kupeperusha BENDERA kwa MDOMO wake U-MAKINI hauhitajiki...
 
je katika makala yake amethibitisha kwamba naye alikuwa kiongozi wa kisiasa ndani ya CHADEMA
 
Hapa naona huyu dr Kitila Mkumbo kweli kichwa yake haiko sawa na huu udaktari sijui aliupataje. Ni hivi karibuni alikana kuhusika na uongozi Chadema pale alipovuliwa ukuu wake katika chuo kikuu DUCE. Sasa anapotoa mada kama hiyo anataka kutuaminisha nini sisi watanzania? Siasa za kweli hazitaki ubabaishaji kama alionao yeye Mkumbo na zzk. Watu wanauawa na kufungwa na kupata ulemavu wa kudumu. Aanzishe chama chake aone kama ni rahisi hivyo.
 
Yaani hao watu makini wanasubiri kuanzishiwa vyama na vilaza alafu baadae wanaishia kulalamika huku wakijiita watu makini!!!
Kitila anzisheni chama na mukiite Chama Cha Watu Makini (CCWM).
 
Hilo nalo wazo zuri Lakini cdm itaathirika kwa kiasi kikubwa Sana ikiwa Akina zitto na wenzake watatotoka la sivo busara itumike katika mamuzi
 
Hapa naona huyu dr Kitila Mkumbo kweli kichwa yake haiko sawa na huu udaktari sijui aliupataje. Ni hivi karibuni alikana kuhusika na uongozi Chadema pale alipovuliwa ukuu wake katika chuo kikuu DUCE. Sasa anapotoa mada kama hiyo anataka kutuaminisha nini sisi watanzania? Siasa za kweli hazitaki ubabaishaji kama alionao yeye Mkumbo na zzk. Watu wanauawa na kufungwa na kupata ulemavu wa kudumu. Aanzishe chama chake aone kama ni rahisi hivyo.
khaa!! Hii issue ya kusema mtu aanzishe chama chake kwani CDM ni mali ya nani hasa???
 
Yaani hao watu makini wanasubiri kuanzishiwa vyama na vilaza alafu baadae wanaishia kulalamika huku wakijiita watu makini!!!
Kitila anzisheni chama na mukiite Chama Cha Watu Makini (CCWM).

Mkuu Mtazamo, niliwahi taka kujiunga na Chama cha Demokrasia Makini cha Prof L. Shayo, lakini nikagundua na wao hawakuwa makini!
 
Back
Top Bottom