Dk. Bilal amtisha Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Bilal amtisha Rais Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mdondoaji, Jul 5, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Printer-friendly versionSend to friend

  Ni ikiwa hatamteua kugombea urais Zanzibar
  Mabilioni yamwagwa kutoka Uarabuni
  Mbunge Rostam Aziz ahusishwa

  Dk. Mohammed Gharib Billal

  RAIS Jakaya Kikwete ametishiwa. Ameambiwa asipopitisha jina la Dk. Mohammed Gharib Billal katika kinyang’anyiro cha urais visiwani Zanzibar, yeye na chama chake “watakiona cha moto.”

  Taarifa kutoka ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinasema, tayari Rais Kikwete amefikishiwa ujumbe wa kumshinikiza kumpitisha Dk. Billal.

  Dk. Billal, tayari amechukua na kurejesha fomu ya kuwania uteuzi wa kugombea urais Zanzibar, akiwa mmoja wa waombaji 11 wa nafasi hiyo.

  Taarifa zinasema iwapo Dk. Billal hatateuliwa kugombea urais, wafuasi wake “watachukua hatua,” na kwamba tayari ujumbe wao, ambao hasa ni wa Dk. Billal, umefikishwa kwa rais.

  Chanzo cha habari hizi kimekariri baadhi ya wafuasi wa Dk. Billal wakijiapiza, “Nakwambia Dodoma patachimbika. Hatuwezi kukubali tena kuchezewa na hili tayari tumetuma watu wakamweleze Kikwete.”

  Vyombo vya habari vilikariri juzi Jumatatu, mmoja wa wafuasi wa Dk. Billal, aitwaye Mwinyi Rehan wa masikani ya Kisonge, mjini Magharibi akisema, iwapo mtu wao hatateuliwa, basi wataharibu kura, au kuinyima kura CCM au kuanzisha chama chao cha siasa.

  MwanaHALISI lilipozungumza na Dk. Billal kuhusu “ujumbe wake” kupeleka shinikizo kwa Rais Kikwete na kutishia kuwa asipopitishwa “Dodoma patachimbika,” haraka alijibu, “Hilo si kweli.”

  Alisema akiwa mwanachama anayekijua chama hicho vizuri na kiongozi wa ngazi ya juu, hawezi kutumia staili ya vitisho kwa mwenyekiti ili aweze kushinda uchaguzi.

  Staili ya kampeni za vitisho kwa rais aliyepo madarakani, inadaiwa kuigwa na wafuasi wa Dk. Billal kutoka mafanikio ya kampeni za Kikwete mwaka 2005.

  Ni wanamtandao wa Kikwete wanaodaiwa kumtisha Rais Benjamin Mkapa ili kubadilisha msimamo wake katika uchaguzi wa ndani ya chama.

  Wapambe wakuu wa Kikwete wakati huo, ambao sasa baadhi yao wanamuunga mkono Billal, ndio wanadaiwa kuwa mstari wa mbele kushinikiza uteuzi wa Billal.

  Tokea Dk. Billal achuke fomu ya kutafuta uteuzi, zogo kubwa limezuka visiwani Zanzibar huku kukiwepo juhudi za kushikiniza kupitishwa kwake kwa madai kuwa “amedhulumiwa nafasi hiyo mara mbili mfululizo.”

  Dk. Billali alijitosa katika kinyang’anyiro cha urais kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na kugombea tena mwaka 2005, kabla ya kuenguliwa na chama chake katika hatua za awali.

  Katika uchaguzi wa mwaka 2000, Dk. Billal alishindwa na rais wa sasa wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, wakati katika uchaguzi wa mwaka 2005 alilazimishwa na Rais Mkapa kuondoa jina lake ili rais aliyeko madarakani amalize muda wake wa mihula miwili.

  Tangu wakati huo Billal amekuwa akijiimarisha kwa kujenga mitandao mipya na kuimarisha ile ya awali; ingawa baadhi ya wafuasi wake, hasa wale aliokuwa nao mwaka 2000, kama vile Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna wakiwa tayari wamehama kambi yake.

  Hata hivyo, wengi wa wafuasi wake, hasa wale waliokuwa katika serikali ya Dk. Salimin Amour inayotuhumiwa kuchochea mfarakano Visiwani, bado wamebaki kambini mwake.

  Wakati minyukano ya wagombea ikiendelea, zimepatikana taarifa kuwa mamilioni ya shilingi kutoka Nchi za Falme za Kiarabu, yamemwagwa nchini kwa ajili ya kampeni za mmoja wa wagombea urais mwaka huu.

  Fedha hizo zinadaiwa kupitia kampuni moja iliyoko nchini Kuwait (jina tunalo) na zimeingizwa nchini kupitia pia kampuni binafsi ya mmoja wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Taarifa zilizopatikana juzi Jumatatu mjini Zanzibar zinasema mamilioni hayo ya shilingi yamelenga kulainisha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Kamati Kuu (CC), vyombo vya ulinzi na usalama, vyombo vya habari na waandishi wa habari mmojammoja.
  Mgombea wa kwanza kuhusishwa na mamilioni hayo ya shilingi ni Dk. Billal.

  Gazeti hili lilimtafuta Dk. Billal na kuongea naye kwa simu kutoka Zanzibar. Lilitaka kujua iwapo anafahamu kampuni hiyo ya Arabuni na iwapo amepokea fedha kutoka huko.

  Bila kukiri kupokea fedha kutoka Arabuni na bila kutaja kampuni iliyozipokea nchini, Billal alisema, “Katika hatua hii, nahitaji kila senti, ili mradi fedha hizo zisiwe chafu.

  Kuhusu kuifahamu kampuni ya Arabuni, Dk. Billal alisema tu kuwa amewahi kuisikia ikitajwa katika nyanja za kibiashara.

  Alisema, “…Kampeni zinahitaji fedha. Kama kuna watu wanataka kunichangia mimi siwezi kukataa. Jambo la muhimu ni kufahamu kwamba kuna taratibu za kufuata kwa ajili ya kutoa michango kwa watu wanaowania fursa za kisiasa.

  Akigeukia Sheria ya Gharama za Uchaguzi iliyopitishwa miezi minne iliyopita, alisema “…sheria imeweka wazi kila kitu. Kwa hiyo mimi nitapokea msaada wowote wa hali na mali kutoka kwa mtu au kampuni ili mradi msaada huo umefuata sheria zilizopo nchini na fedha hizo si chafu.

  “I have always run a clean campaign (Siku zote nimeendesha kampeni safi kimaadili). Sina rekodi yoyote mbaya na nadhani wananchi wa Zanzibar wanafahamu kuhusu hilo,” alisema.

  Alipoulizwa iwapo katika juhudi zake za sasa na shinikizo kwa Rais Kikwete anasaidiwa na viongozi wa CCM na serikali, alisema “Katika hatua za sasa, mimi kama mgombea mtarajiwa, nina haki na wajibu wa kutafuta kuungwa mkono na kila mwanachama wa CCM, hususan wajumbe wa NEC.”

  Kuhusu taarifa zilizoenea kuwa anaungwa mkono, kwa hali na mali, na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Dk. Billal alisema, “Kama ilivyo kwa wajumbe wengine, Rostam ni mjumbe wa NEC na kwa namna hiyo ninahitaji pia kuungwa mkono naye. Huo ndio mkakati wangu katika kipindi hiki.”

  Habari zilizopatikana tunakwenda mtamboni zilieleza kuwa mwandishi wa habari Boniface Makene wa gazeti la Rai, linalomilikiwa na Rostam Aziz, ndiye anayetajwa kufanya kazi ya Dk. Billal kwa zaidi ya miezi miwili sasa. Inadaiwa hiki ndicho kiungo cha Rostam na Billal.

  Hivi sasa kuna madai kwamba katika kampuni ya New Habari Corporation inayochapisha gazeti la Rai, limeibuka zogo kuhusu Makene kulipwa mshahara wakati hafanyi kazi za gazeti; bali za Billal.

  Inadaiwa kuwa ni Makene aliyeratibu safari za waandishi wa habari na kulipa mafao yao yaliyotokana na safari ya kwenda Zanzibar kushuhudia Dk. Billal akichukua fomu ya kuwania uteuzi.

  Jingine linalomuunganisha Rostam na Billal ni mstuko alioupata Rostam na kukaripia mmoja wa wahariri wake kwa madai kwamba habari kuhusu Billal iliyochapishwa Alhamisi iliyopita, “haikuwa nzuri.”

  Toleo Na. 874 la Rai, lilichambua Billal kwa kina, likieleza udhaifu wake tangu akiwa waziri kiongozi chini ya utawala wa Salmin Amour.

  Gazeti liliibua taarifa za uchanga wa Dk. Billal katika chama kwani rekodi zinaonyesha alijiunga CCM mwaka 1991 nyakati za ujio wa Mageuzi. Mwaka huu nao bado unatiliwa mashaka na ni moja ya vikwazo vyake mwaka vya sasa.

  Wagombea wengine wawili ambao majina yao yamehusishwa na fedha za Arabuni (majina tunayo) katika uchaguzi, hawakuweza kupatikana kueleza upande wao.

  Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanahusisha umwagaji wa fedha na jitihada za makampuni ya nje kutafuta kupewa mikataba ya utafutaji mafuta baada ya kuenea kwa taarifa za kuwepo rasilimali hiyo nchini.

  Kuna taarifa kwamba watuhumiwa ufisadi wanamuunga mkono Dk. Billal na kwamba mkakati huo umelenga katika kutafuta mrithi wa Kikwete katika uchaguzi wa 2015.


  Source: Mwanahalisi.

  Mtazamo: Jana nilisema kuwa nilisikia tetesi kuwa washkaji wake Dk.Bilal walichimba mkwala kwa mtu wao! Inaelekea kuna kaukweli ndani what is so special ikulu ya zanzibar safari hii? is it deals za mafuta? is it free trade? au wanatetea haki kweli za wazanzibari??
   
 2. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Narudia tena, ...........huu ni mwaka wa uchaguzi tutasikia mengi. Ila itoshe kusema hivi kwanini lifikapo suala la kumpata rais wa Zanzibar basi nguvu kubwa itegemewe kutoka Bara? Hivi sisi wabara kwanini tusiache wao (Zenji) wakasimika kiongozi wamtakaye? Kama nakumbuka vizuri hata huyu wa sasa AAK, ni kama alibebwa tu na viongozi wa Bara na hakuwa chaguo la Wazanzibari.

  Iwapo mambo yatakwenda kama 2000 basi safari hii tutegemee vurugu sana, na kama kweli itatokea hivyo basi NEC ya CCM haitoweza kukwepa lawama. Acheni wachague mtu wao wenyewe ili wasije tupa lawama kwenu!!
   
 3. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Wana mafuta ndugu yangu...haya tu ya kuagiza wanachakachua sembuse hayo ambayo yatachimbwa??? Hilo ni Bonge la dili so wanataka mtu atakae kuwa Zenji awe ni mwenye kuwasikiliza na kutekeleza matakwa yao.....No way Wakawaachia wajiamulie.....
   
 4. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #4
  Jul 5, 2010
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nasikia Bilal ni chaguo la mfanyabiashara mmpoja maarufu wa tz bara mwenyeji wa kaskazini mwa tanzania, mfanyabiashara huyo ameahidi kutumia influence yake kuhakikisha jamaa anakikalia kiti.
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Usitegemee Bara wakawaachia hizi dili za mafuta hata siku moja. Wewe imagine ile kampuni ya kuchimba mafuta kule kusini itatoa dola bilioni 70 kufanikisha uwekezaji wa offshore drilling hizo ukiweka katu 1% unazungumzia kama $700 milion unafanya mchezo!!! vitubilioni vingapi hivyo?
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huyo mfanyabiashara hanitishi maana kama ni mtanzania basi atakuwa na roho kidogo ya uzalendo lakini wanaoniogopesha mie waarabu kutoka kwao huko umangani. Reserves za mafuta kwao zinategemewa kuisha by 2050 according to geological survey sasa wanahamishia nguvu maeneo mapya mh tutasurvive kweli? Hapa panahitajika umakini katika mikataba otherwise hatupati kitu. Na kwanini wapite mlango wa nyumba kumsukuma mtu wanayemtaka aingie ikulu?
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Dr Bilal alistahili kuwa mgombea wa CCM tangu mwaka 2000. Labda kama kuna pingamizi la kiusalama ambalo hatustahili kuambiwa kama mzee wetu JSM alivyofanyiziwa kwenye Urais wa JMT.
   
 8. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Wildcard na Kandambilimbili acheni kutumia codes, nyie tajeni majina moja kwa moja why scared to mention names? JF is where we dare to talk openly
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Rostam huyu!...
   
 10. doup

  doup JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  R U serious Mzigo by 2050 unaweza kuwa umekauka???? Jamani chondechode tuwe na moyo wa subra, ili tuweze kuwa-enslave, kichwani hawa jaamaa hamna kitu uvivu ndi isiseme. kwa mtaji huo Bilal naona kama atauza nchi kama ni kweli anachukua hivyo vijisent toka huko.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Soma Article hii:

  World oil supplies are set to run out faster than expected, warn scientists - Science, News - The Independent

  Check na hiyo graph:

  The End of Cheap Oil, by Colin J. Campbell, Jean Laherrere

  Utapata picha halisi
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Zile tetesi kuwa Dk. Bilal ataendeleza uunguja na upemba bado zipo? kama zipo Bilal hawafai wa Zenji. Tunataka mtu wa kuwaunganisha hawa watu kwani ni ndugu na si kuwagawanya kama walivyofanya hawa waliopo na waliopita. Hainiingii akilini watu wa unguja na pemba ambao ni nusu kwa nusu upande mmoja usiwekwenye serikali kabisa. Kama Dr. Bilal ataendeleza uunguja STOP please or change. Otherwise go for contesting and wish u all the best.
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu!!!
  Yetu masikio tu!!
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Mwakaa huu balaa naipenda sana nchi yangu...nasubiri sana maisha ya siasa za Bongo....mwaka huu keep us posted walahi
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  katika kikao chetu cha mwisho hapa majuzi: shein alipitishwa
   
 16. minda

  minda JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hizo za nasikia ni uvumit tu. time will tell. lets us just wait and see.
   
 17. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndo basi tena jamaa hapiti. amekiri kufahamu kampuni hiyo ya uarabuni, ameriki pia kwamba pesa anapokea kutoka sehemu yoyote.Kuhusishwa na siasa za kuwabagua wapemba ni kinyume na kampeni za ccm. na ndo maana Cheni yuko pale. kuhusishwa na makampuni hayo ya mafuta ni sumu nyingine. Huyu jamaa sidhani kama UWT watamuachia ashinde. yetu macho.
   
Loading...