n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,013
- 2,684
na Betty Kangonga | Tanzania Daima | Novemba 13, 2012
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameshindwa kuwa muwazi katika kuainisha makundi yaliyoko ndani ya chama hicho.
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Dk. Bana alisema Rais Kikwete alipaswa kuwa muwazi kwa kuyataja makundi yanayoonekana kukivuruga chama hicho badala ya kutumia diplomasia zaidi.
Dk. Bana ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Mapango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia (REDET), alisema kuwa hotuba aliyoitoa Rais Kikwete ni nzuri, lakini ina upungufu kutokana na kushindwa kuyataja makundi yanayosigana.
Alisema kuwa kama kweli Rais Kikwete alikuwa na nia ya kutaka kuondoa makundi hayo, alipaswa kuyataja hadharani kuliko kuyaficha hatua inayoonyesha kuwa ameshindwa kukabiliana nayo.
"Kama kweli alikuwa na nia ya kutaka kuyamaliza makundi yaliyopo ndani ya chama chake alipaswa kuyataja kwa kuwa ni kiongozi wa juu wa chama hicho angeagiza Kamati ya Maadili kuyaita makundi hayo ili kuyapa onyo," alifafanua.
Bana aliongeza kuwa hatua hiyo ingesaidia makundi hayo kuogopa na kupunguza kasi inayokifanya chama kuwa na mvurugano.
Kuhusu suala la rushwa, alisema kuwa bado Rais ameshindwa kuwa wazi katika kudhibiti hali hiyo isijirudie na badala yake amekuwa akikemea pasipo kuchukua hatua madhubuti.
Msomi huyo alisisitiza kuwa kama hakuna mkakati maalumu wa kudhibiti rushwa ndani ya chama hicho, upo uwezekano wa kusambaratika jambo; linaloweza kusababisha taifa kuyumba.
"Lakini hotuba yake ni nzuri ameweza kuwajengea wanachama wake kuzidi kujihami kutokana na kuweka wazi kuwa wanazidi kusimamia na kutekeleza sera katika serikali yake," alisema.
Dk. Bana pia alipongeza hatua ya kuchaguliwa kwa Philip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, akisema kuwa hatua hiyo inaweza kukisaidia chama hicho kurudi katika nidhamu yake kama ilivyokuwa zamani.
"Kumrejesha Mangula ni kurudisha nidhamu ndani ya chama hicho ambayo ilishaanza kupotea hatua iliyokuwa ikipoteza imani kwa wananchi," alisema.