Dk. Bashiru Ally: Nape, Bashe wanahitaji kupikwa

Siwezi mshangaa Bashiru maana hili lilishatabiriwa zamani,kamwe huwezi maintain akili kubwa ukiwa CCM hasa kwa hii regime.. hata leo Prof. Issa Shivji ikitokea 'akauza utu wake' apewe ukatibu mkuu/ wenezi wa CCM utamkataa kuwa ni yeye.
 
Chuo cha propaganda kilikuwepo kivukoni matunda yake ni ufisadi ktk Serikali, Bunge na judiciary. Watu wanatunga katiba kisha wenyewe wanaipondaponda!
 
Unapomnyooshea kidole mwenzako kuna vidole vine vinakunyooshea wewe mwenyewe.
 
Na majizi pia Mkuu. Wana mtandao wao wa majizi ukiongozwa na kubwa la majizi kuanzia Ikulu umetambaa serikalini, ccm hadi bungeni. Sasa wamejenga chuki kubwa dhidi ya CAG Assad kwa kuuanika hadharani mtandao wao.
Unaijua nchi pekee duniani ambayo waziri anatetea ufisadi kwa ahadi ya kuvua nguo???
 
Reactions: BAK
Tatizo kubwa sana lililotupata wa tanzania ni kipindi cha mpito wakati tukibadili mfumo wa uendeshaji uchumi wa nchi yetu kutoka state owned economy na kuingia kwenye free market economy,ambapo kila mmoja alianza scrambling for wealth.
Viongozi ambao kwa kupindi kirefu walibanwa na miiko ya uongozi ,walianza kutafuta mali kwa bidii kubwa na ndio tatizo la rushwa likaanza kushamiri na kuota mizizi.
Wananchi pia kwa kuona hivyo wakajiingiza kwenye vitendo vya kupokea rushwa,uongozi ukaanza kununuliwa kwa kasi ya ajabu.
Wakazuka madalali wengi wa kisiasa ,fitna kwa kwenda mbele ndani ya vyama vya siasa,matokeo yake ni kujengeka kwa makundi mbali mbali yaliyokuwa yakihasimiana .
Kwa kweli nchi ikawa katika tafrani ,kila mmoja akitaka kujilimbikizia mali.
Kwa hali hii,wananchi na wanachama wa vyama mbali mbali vya siasa walikumbwa na virusi vya kansa ya rushwa,ambayo matibabu yake yanaligharimu sana Taifa.
Unaweza kumuona mtu leo ni mwanaharakati akipinga hiki ama kile kwa nguvu zote,lakini kesho akipata madaraka uwanaharakati unakufa miserably, hapa ndio tunapaswa kutafakari ili kujua kama ni uwanaharakati wa kweli au ni ghilba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…