Dk 45 ya leo: Prof Mukandala kapata "walkover"!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,409
Reaction score
14,116
Dk 45 ya leo ilikuwa ina bore.
ITV inabidi wajifunze kuweka watu wenye uelewa mkubwa zaidi ili kuwaweka kiti moto wasomi kama Prof Mukandala katika kipindi cha dk 45 ya leo.

Muulizaji maswali kipindi cha leo si msomi, hivyo maswali yake hayakuwa ya kina na naweza kusema general questions.

Maswali ya kitoto kama wahadhiri kuwa na uhusiano na wanafunzi, wanafunzi na mikopo, hostel za wanafunzi, haya yote yangeweza kujibiwa na karani wa wizara elimu ya juu.

Maswali.mazito juu ya uhusiano wa elimu ya juu na sera ya viwanda sikuyasikia.
Maswala ya matumizi na mafanikio ya utafiti wa wasomi wetu sikusikia.

Matumizi mabaya ya maeneo ya kisomi(Academic Areas) na kuyageuza kuwa ya biashara, kama Mlimani City, hayakuulizwa kisawasawa.
Uwekezaji kitaifa katika elimu ya juu, R&D yaani utafiti katika teknolojia, matazamio katika eneo hilo kiujumla ~hakuna kabisa!

ITV, leo mmempa Prof Lwekaza Mukandala, a walkover!
 
Hawa Maprofesa nao wawe wanaangalia interview za kufanya, anakubalije kufanyiwa interview na kilazerrr?
Nami nimeiona
Maswali yalikuwa si ya mtu aliyepitia chuo na yalijibiwa kirahisi mno kuridhisha gumzo tu.
Tunakumbuka enzi za Msekwa , Kaduma na Prof Mmari
 
Sikuangalia kipindi...... alikuwa bwana Sam Mapesa?? Kama ni mapesa ameshawahi kujadiliwa hapa mara kadhaa kuwa kile kipindi hakimudu
 
ITV inaangaliwa na Watanzania wa kada zote hivyo maswali technical sana yasingefaa,ni sawa kbsa kuuliza general questions
 
Sikuangalia kipindi...... alikuwa bwana Sam Mapesa?? Kama ni mapesa ameshawahi kujadiliwa hapa mara kadhaa kuwa kile kipindi hakimudu
ITV lazima iongozwe na vipindi vyenye viwango.
Viwango vya vipindi vinavyohitaji taaluma haviwezi kuwekwa na mtangazaji mwenye viwango finyu vya elimu.
 
nlichoka sana alipouliza ishu ya mahusiano kiukwel.....
 
Matumizi mabaya ya maeneo ya kisomi(Academic Areas) na kuyageuza kuwa ya biashara, kama Mlimani City, hayakuulizwa kisawasawa.!

Chuo kikuu kina kitivo cha Biashara hicho kitivo umahiri wake ulitaka wakauonyeshee wapi kama sio kupanga mipango kama hiyo ya kibiashara kwenye eneo la chuo?

Vvyu vyenye vitivo mfano vya uhandisi huzalisha hata bidhaa za kuuza.Umahiri wao unatakiwa kuonyeshwa kwenye maeneo yao ya chuo ona chuo cha Makerere wanaanza uzalishaji wa magari

Kwa Tanzania vyombo vingi vya habari vinaajili watu kwa kuangalia kigezo cha sauti nzuri,......
 
Dk 45 ya leo ilikuwa ina bore.
ITV inabidi wajifunze kuweka watu wenye uelewa mkubwa zaidi ili kuwaweka kiti moto wasomi kama Prof Mukandala katika kipindi cha dk 45 ya leo.

Muulizaji maswali kipindi cha leo si msomi, hivyo maswali yake hayakuwa ya kina na naweza kusema general questions.

Maswali ya kitoto kama wahadhiri kuwa na uhusiano na wanafunzi, wanafunzi na mikopo, hostel za wanafunzi, haya yote yangeweza kujibiwa na karani wa wizara elimu ya juu.

Maswali.mazito juu ya uhusiano wa elimu ya juu na sera ya viwanda sikuyasikia.
Maswala ya matumizi na mafanikio ya utafiti wa wasomi wetu sikusikia.

Matumizi mabaya ya maeneo ya kisomi(Academic Areas) na kuyageuza kuwa ya biashara, kama Mlimani City, hayakuulizwa kisawasawa.
Uwekezaji kitaifa katika elimu ya juu, R&D yaani utafiti katika teknolojia, matazamio katika eneo hilo kiujumla ~hakuna kabisa!

ITV, leo mmempa Prof Lwekaza Mukandala, a walkover!
mwamdishi akitakiwa aulize je uhalali wa PHD za wanasiasa wa juu ambazo chuo kimezitoa, wakati kuna ushaidi wa wazi kuwa zimepatikana kwa kunakiri kazi za wengine, je hadhi ya chuo inashuka kwa kugawa phd kwa wanasiasa?
 
Chuo kikuu kina kitivo cha Biashara hicho kitivo umahiri wake ulitaka wakauonyeshee wapi kama sio kupanga mipango kama hiyo ya kibiashara kwenye eneo la chuo?

Vvyu vyenye vitivo mfano vya uhandisi huzalisha hata bidhaa za kuuza.Umahiri wao unatakiwa kuonyeshwa kwenye maeneo yao ya chuo ona chuo cha Makerere wanaanza uzalishaji wa magari

Pengine kwa akili yako biashara nzuri zaidi ni kukiuza chuo kabisa kwa faida.
 
Hajaanza jana huyu jamaa.Hata alipomuhoji Prof Ndalichako aliboa mno.Nadhani anashinda mno mitaani kutafuta breaking news hivyo anakosa muda wa kuandaa maswali ya kina kulingana na watu anaotarajia kuwahoji. Prof au waziri au katibu mkuu anakupa nafasi ya kuuliza maswali kwa dakika 45 halafu unakuja na maswali ya kitoto dah!
 
Back
Top Bottom