Diwani Yombo Kilakala akaangwa

Kichapo13

Member
Jan 27, 2013
75
0
Diwani wa Kata ya Yombo Kilakala (CCM) Elizabeth Magwaja amelalamikiwa na wenyeviti wa matawi katika kata hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa anaunga mkono vyama vya upinzani katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Wenyeviti hao wameandika barua kwa Katibu wa CCM wilaya ya Temeke wakimshutumu Diwani huyo kwamba amekuwa akiwasaidia wagombea wa UKAWA ili washinde katika kata yake baada ya wapambe wake kuangushwa katika kura za maoni.
Tayari imefahamika kwamba Kamati ya Maadili ya chama hicho wilaya, itamhoji Diwani huyo wikiendi hii.
 

Kichapo13

Member
Jan 27, 2013
75
0
Hii itamsumbua kwasababu anaonekana Msaliti katika chama chake. Na ikumbukwe tayari Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdallah Bulembo wameshatoa kauli kwamba Diwani atakayehujumu uchaguzi atafukuzwa uanachama. Nahisi dalili si njema kwa huyu mama!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom