Tetesi: Diwani wa Ifakara aliyeshirikiana na Mbowe kwenye Kilimo aliuawa kwa kukatwa Mapanga

Benson Mramba

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
644
1,482
Kama ambavyo wamesema Lijualikali na Waitara kuhusu Mbowe kuiba fedha na kwenda kufanya kilimo huko Ifakara. Mbowe alifanya kazi hiyo kwa Mgongo wa Diwani mmoja huko Ifakara jina silikumbuki vizuri.

Ila Diwani huyo alishambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana. Taarifa nilizozipata wakati huo kutoka kwa viongozi wa juu ndani ya CHADEMA ni kuwa huenda Diwani huyo aliuawa kwasababu za kimaslahi kuhusu mambo ya mashamba na kilimo aliyofanya na Mbowe. Sikuandika kwasababu sikuwa na taarifa za ndani kuhusu mradi huo maana Wabunge hawa walificha hizi taarifa.

Ila niliwahi kuandika kuhusu hisia zangu za Mbowe kuhusika na upotevu wa Ben Saanane na Shambulio la Tundu Lissu. Magazeti yaliandika habari hii.

Sasa zipo hisia kubwa kutoka kwa viongozi ndani ya Chama kuwa Mbowe alihusika na shambulio la Diwani yule kwa sababu za kimaslahi.

Vyombo husika vifuatilie mwangwi huu!

Kwa tunaomjua Mbowe tunajua anaweza kufanya lolote almradi kulinda maslahi yake. Zitto kama hatakuwa mnafiki atakiri hadharani kuwa alishawahi kukatiwa breki za gari lake wakati fulani. Pia alitaka kuwekewa sumu na Ben Saanane.

Ben Saanane tukiwa nae Mabibo External kwenye Bar moja kubwa pale opposite na kanisa la KKKT baada ya kuondolewa Makao Makuu ya CHADEMA aliniambia kwa mdomo wake kuwa amemwambia Mbowe kuwa kama atabariki yeye kuondolewa Ben Saanane kuondolewa pale Makao makuu basi atajua atakavyojitetea maana wamefanya mengi yeye na Mbowe hivyo Mbowe anapaswa kumlinda. Jibu la Mbowe kwa Ben Saanane lilikuwa " UNANITISHA? Tuonane wiki ijayo" Alipoenda wiki ijayo akapewa cheo ambacho hakipo kwenye Katiba wala muundo wa Chama cha MSAIDIZI WA MWENYEKITI MAKAO MAKUU. alifanya kazi miezi miwili tu.

Nakumbuka alitumwa Hai na baadae Afrika Kusini. Aliporudi Afrika Kusini akiwa airport aliwasiliana na watu wawili kuwa amerudi baada ya hapo hajaonekana tena mpaka leo. Kwa tuliokuwa Makao Makuu mahusiano ya Mbowe na Saanane hayakuwa mazuri tena tangu Zitto aondoke CHADEMA maana siri nyingi zilivuja na hivyo Mbowe akawa anamkataa Saanane ili asichafuke. Mbowe anatumia mtu halafu anamkataa.

Alimtumia Zitto dhidi ya Chacha Wangwe akamkataa, Akamtumia Slaa na akina Saanane akawakataa, akawatumia Komu na Lwakatare dhidi ya Slaa leo amewakataa. Nasubiri anguko la Lissu baada ya Shambulio kufeli.

Muda unanisaidia sana. Ndio maana nasemaga JINI LINAWALA WAFUGA JINI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni propaganda za kipumbavu na za kipuuzi Tz ina chagamoto nyingi zaidi ya Mbowe nguvu mnazo elekeza kwa kimshusha mbowe mgeziweka kwenye masuala yanayo saidia taifa sio chama, corona ipo maleria ipo elimu bado mbovu sector ya afya ina shida kubwa mnatuletea propaganda za mbowe kila wakati watu ni wale wale....tumechoka tunahitaji national issues plz
 
Unaendelea na upuuzi wako kama kawaida yako, ukiambiwa upeleke ushahidi wa tuhuma zako panapostahili utaweza? au unadhani ushahidi ni huo umbea ulioandika hapo juu?

Tafuta kazi ya maana ufanye, wacha kuhangaikia maisha ya wengine, mental slavery ni utumwa mbaya zaidi ya wote hapa duniani, so emanticipate yourself myfriend.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Benson Mramba yaani unaandika mambo ya kijinga tena kwa werevu wa wapumbavu. Ni kama vile una jambo binafsi na Mbowe!

He is a Verified Member kama wewe! Bila shaka mtatolea ufafanuzi hizi shutuma dhidi ya Mwenyekiti wenu. Au ikibidi mumshtaki mhusika au mimshinikize aombe radhi au atoe ushahidi wa maelezo yake.

Haiwezekani kada wenu muasi aje atokwe mapovu kiasi hiki halafu mambo yaishe tu kimya kimya! Wengi tutaamini.

Hizi shutuma ni nzito!! Mfano hiyo shutuma ya huyo Diwani wa Namwawala Mh. Lwena, ninachokumbuka Polisi waliwakamata baadhi ya watuhumiwa, na wengi hatujui mpaka leo hiyo kesi imeishia wapi!
 
Hizi ni propaganda za kipumbavu na za kipuuzi Tz ina chagamoto nyingi zaidi ya Mbowe nguvu mnazo elekeza kwa kimshusha mbowe mgeziweka kwenye masuala yanayo saidia taifa sio chama, corona ipo maleria ipo elimu bado mbovu sector ya afya ina shida kubwa mnatuletea propaganda za mbowe kila wakati watu ni wale wale....tumechoka tunahitaji national issues plz

Sent using Jamii Forums mobile app
Fanya wewe kazi hiyo. Mgawanyo wa majukumu. Kwa sisi wengine Mbowe ni mbaya kuliko Corona. Watu wameuawa, wamefilisika, ndoa zimevunjika na wengine hatuelewi hata kwanini tulipoteza muda kwenye siasa ili tu kuimarisha mfumo wa vyama vingi ili Taifa hili watu wabishane kwa hoja na kuwa na jukwaa mbadala la kusemea.

Sasa anapotokea mtu mmoja kulinda maslahi yake kuliko maslahi ya Chama chenye jasho na damu za wengi na kuliko maslahi ya Taifa hatuna budi kuunganisha nguvu kumdhibiti mtu huyo.

Actually nawashangaa sana usalama wa Taifa na serikali kumwachia Mbowe aiharibu CHADEMA ambayo ilishakuwa Taasis muhimu kwa Taifa hili. Ni bahati mbaya sana.

Pia nawashangaa Wanachadema wenyewe kukaa kimya, kususa na kumuacha afanye atakavyo kana kwamba CHADEMA ina jasho la Mbowe tu. Infact Mbowe hajawahi kupata hasara yoyote wala tabu kwenye CHADEMA. Slaa NDIO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uongo ni kwa faida ya nani?? Kwanini kama una ushahidi wa kupotea kwa fedha za Chadema pamoja na Ben Saanane usifungue shari Mahakamani badala ya kufungua uzi humu?? Nendeni Mahakamani kisha mrudi humu kutuletea mrejesho ni si huu upuuzi wa kuchafua watu bila sababu.

CCM mmeishiwa hoja sasa kilichobaki ni kujaribu kuwachafua watu wasio miliki vyombo vya usalama. Hizi nguvu mnazozitumia humu kwanini msengejielekeza kwa wananchi ili kujinadi kwao??

Slowslow ndiyo kazi yake aliyoibakiza hivi sasa. Toka amekabidhiwa chama kama Muenezi wake hajawahi hata siku moja kwenda mbele ya wananchi kueneza sera za ccm zaidi ya kuwaita waandishi wa habari kuimba nyimbo za kuabudu na kusifu.

Tofauti na hapo kejeli na vijembe kwa wapinzani. Mnapoteza muda mwingi kufikiri mnawabomoa wapinzani kumbe mnawaimarisha. Mmesahau nyumba yenu mnahangaika na ya wenzenu.

Hakuna upinzani mbaya kama huu unaofukata hivi sasa ndani ya ccm hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu mwezi Oct mwaka huu. Niwahakikishieni hamtafanikiwa ktk vita ambapo ninyi wenyewe mnavurugana.

Tunashuhudia hivi sasa M/Kiti wenu Taifa anavyoyumbisha Serikali ukifikiri utaishia tu hapo la hasha. Hata chamani upo. Hasa kwenye nafasi za Wagombea Ubunge. Ni suala la muda tu utanielewa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwisho wa Mbowe utakuwa Mbaya sana damu za watu zitamlilia daima
Hizi ni propaganda za kipumbavu na za kipuuzi Tz ina chagamoto nyingi zaidi ya Mbowe nguvu mnazo elekeza kwa kimshusha mbowe mgeziweka kwenye masuala yanayo saidia taifa sio chama, corona ipo maleria ipo elimu bado mbovu sector ya afya ina shida kubwa mnatuletea propaganda za mbowe kila wakati watu ni wale wale....tumechoka tunahitaji national issues plz

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom