Diwani earnings

Diwani earnings

Jmo

Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
17
Reaction score
2
Waheshimiwa habari zenu?
Kuna mabishano hapa naomba mnisaidie kwamba kati ya diwani na mtumishi mwingine wa serikali kama mwl, afisa kilimo, mhasibu nk(desk officers) nani ana earning nzuri
chukulia miaka 5 au 10 ya udiwani na huyu mfanyakazi mpaka kustaafu!
 
diwani hana mshahara mnene ka afisa kilimo chukulia hod,ila ana perdiem ndefu mana nje ya wilaya anakula 80 per day,akiwa wilayani kwake 65 plus nauli,pia wamejiwekea utaratibu wa 'kuwanyanyasa' watumishi,ukiwa fisadi na miradi unaweza kutumia udiwani kupushi,ila ukiwa mwenzangu na mimi CDM unapigania watu kipato cha udiwani huwezi kulingana na afisa mpaka kustaafu
 
Mdugu zangu kwanza udiwani ilikua kazi ya heshima tukifuata utaratibu wa uingereza ambako hakukua na malipo yoyote ila diwani anakua mojawapo ya matajiri wa kata basi anapewa uakilishi na jamii husika.

Kwa sasa hasa kwa mazingira yetu ikawa ngumu wakawa wanapewa 60,000 kwa mwezi mpaka pinda alipojaleta mabadiliko akiwa waziri wa tamisemi ndipo ikapanda kidogo. Hadi sasa madiwani wanalipwa kidogo ila ni mtaji wa kupata marupurupu kibao na asilimia kubwa bila kujali chama wanatafuta udiwani kulinda maslahi yao au ya mabwana zao aka waliowaweka madarakani na si wananchi. Vivyo hivyo wabunge na marais.

My take better mjasiriamali na wengineo than udiwani
 
Nawaelewa Okw na Mabulangati so mnataka kunambia km ni kugombea upitie CCM na siyo CDM!
 
Back
Top Bottom