Diwani afumaniwa na mke wa sheikh usiku wa manene | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani afumaniwa na mke wa sheikh usiku wa manene

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Sep 22, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Na Joyce Joliga, Songea

  DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tunduru amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mmoja wa masheikh mkoani hapa.

  Katika fumanizi hilo la aina yake, sheikh huyo alipigwa na butwaa baada ya kumshuhudia diwani huyo akiwa amejifunga kiunoni kitenge ambacho alimnunulia mkewe mara baada ya kubisha hodi.

  Tukio hilo limetokea juzi saa nane usiku baada ya mume wa mke huyo kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mkewe ameonekana katika nyumba ya diwani huyo (jina tunalo).

  Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, diwani huyo alikiri kutokea kwa fumanizi hilo lakini akadai kuwa ni njama zilizopangwa na washindani wake wa kisiasa ili kumchafua.

  Baadhi ya watu waliodai kushuhudia tukio hilo walisema kwamba mikakati ya kumfumania ilipangwa na majirani baada ya kuona mke huyo wa sheikh ameingia ndani kwa diwani huyo.

  Walidai diwani huyo ana tabia ya kula na wake za watu na hiyo imemjengea uhasama kwa watu wengi kiasi kwamba ilibidi wato taarifa kwa sheikh huyo ili kumkomoa.

  Mara baada ya shehe kupata taarifa hizo aliongozana na mwenyekiti wa kitongoji cha Raha leo, Mkwanda Mussa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Kitani, Nyenje Madefu hadi nyumbani.

  Kwa mujibu wa mashuhuda hao, jopo hilo lilipofika kwenye nyumba walimokuwemo ndani na kubisha hodi, diwani huyo alifungua mlango akiwa amejifunga kitenge cha mke wa shehe huyo kiunoni na kuwataka waeleze shida waliyoijia.

  Walisema diwani huyo alipigwa na butwa na kuonekana kuwa na kigugumizi baada ya jopo hilo kumueleza kuwa limefika kumtafuta mke wa shehe waliyehisi kuwa yumo ndani.

  Kabla hajajibu lolote waliingia ndani na kumkuta mke wa sheikh akiwa amelala kitandani na ikawa ni ushahidi wa kumkamata diwani huyo hadi ofisi za kata ili kumhoji.

  Baada ya mahojiano ya muda mrefu, inadaiwa kuwa diwani huyo alikiri kosa la kulala na mwanamke huyo na ikaamuliwa alipe Sh300,000 kama faini kwa sheikh.

  Alifanikiwa kupata Sh150,000 na kuahidi kiwango kilichobaki atakilipa hara iwezekanavyo.

  Baadhi ya wakazi wa kata anayoongoza diwani huyo, walidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa alio nao kwa ajili ya kula na wake za watu.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi huu mhhh
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Si ajabu huyo shekhe ana wake 4 kama dini yao inavyowaamuru....wacha madiwani wawasaidie!
   
 4. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Duh, kazi ipo mwaka huu, sasa wanagawa wake,

  Madiwani wanagawa dozi, lol
   
 5. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo Sheikh ana wake wangapi?
  Pia ana umri gani kulinganisha na huyo mkeye?

  Yeye alikuwa wapi mpaka mkewe aondoke saa nane za usiku?
  Hayo ndiyo matokeo ya mitara na mizee kuoa binti wadogo halafu hamuwapi za kutosheleza.

  Kwa mtindo huu ukimwi unanawiri tuu. Masheikh ongezeni kuoa vimwaliiii, vijana wa kuwasaidie kuimarisha mitara yenu wapo..

  Ushauri wa bure kwa vijana na madiwani, endeleeni kuishi karibu na wake za Masheikh.
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kuna sehemu moja hapa Tanzania inaitwa Karagwe; huko fumanizi inakuwa ni deal, yaani inapangwa kwa makubaliano ya mke na mume. Juzi kuna mwalimu mmoja alilipa Tshs 8,000,000/=!. Nashangaa huyo sheikh analipwa 300,000/-
  Swali ni je mkishalipwa hizo hela kama 8m/- mke unamuacha au unaendelea nae? Hivi unadhani huyo aliyelipa hizo hela si kama amelipa mahari kwako - hawezi kuishia hapo., lazima ampate mkeo na atamfanya mchezo mbaya tu!
   
 7. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hao na pamoja na wajumbe wa nymba kumi ndio zao, kwa mfano ukigombana na mkeo akaenda kushtaki kwa balozi kama ni usiku atasema mwache alale hapa wewe nenda kalale nyumbani, asubuhi tutasuluhisha. Sasa kama ndugu hujagundua ukimwacha tu mkeo jua kabanduliwa
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hii kasheshe na mwezi huu mtukufu lakini watu badala ya kujisafisha ndo wanaendelea kufanya maovu inasikitisha
   
 9. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kwetu Kisumu huyo Diwani na huyo Binti mngelikuwa mshawazika kwa hivi sasa!
   
 10. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Duh, ipo kazi, yaani unamuuza mkeo kwa sababu ya vijisenti?!!
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hata kwenye mfungo anagawa?
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Astakafirulahi!!!!
   
 13. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kuna habari zisizo rasmi kuwa kuna wanaume hasa jijini Dar huwaruhusu wake zao kwenda kujiuza kama makahaba ili wapate pesa. Yaani shida tupu.
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  duuh sheikk bwana ,sipati picha anamuona diwani kavaa khanga aliyomnunulia mkewe kama zawadi kwa kumpikia futari mwezi mzima..hahaaaa
   
 15. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Kweli wameishiwa hao, sasa wanagawa wake zao, hizi ndio ndoa za muta, lol
   
 16. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chamtumavi. Kipi bora kuwaoa hawa wanawake au kuwaweka Vimada? Labda nikwambie Tanzania mkoa unaongoza kwa Ukimwi ni Mbeya ukifuatiwa na mwanza,shinyanga na Iringa N.k.

  sasa tujiulize kuna asilimia ngapi huko ya waislam wenye taratibu za kuoa wake wengi wanne.

  Ukiangalia Takwimu za Ukimwi utaona walio owa na kuolewa ndio wanamaaambukizi ya hali ya juu. Sababu dini yenu imekataza kuachana, hivyo unatafuta kipozeo pembeni na yeye anatafuta kisha mnamalizana kitandani na ndani ya familia
   
 17. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Na sehemu zenye maambukizi machache kabisa ni mikoa ya pwani including Zanzibar, ambako majority ni ........!!!! Unajuwa watu wengine sijui huwa hawana cha kuchangia!!! I think wanachofanya ni mradi tu mtu achangie wakati hana hoja ya msingi!!! Hata aliye-post thread hii naamini kashawishika zaidi kwavile inamuhusu sheikh!! Nashawashika zaidi kuamini hivyo kwavile mara nyingi miongoni mwa thread zake ni zile zenye ushabiki wa kidini!!!! Wakati mtu anaamini uzinifu huo umetokana na kuwa na wake wengi, kwanza ajiulize yeye ana wake wangapi na amewahi kuzini mara ngapi!! Na hata kama hana mke, ajiulize kama hajawhi ku-cheat!!! By the way, tuseme huyu mke hatoshelezwi kwakile kinachohisiwa labda yupo ndani ya mitala, what abt huyo diwani?!
   
 18. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama mwanamke alijipeleka mwenyewe kwa diwani hata ningekuwa mm ningemega tu si kajileta.
  Hizo data zenu za ngoma msijifariji sana hiyo mikoa inayoongoza ni kutokana tu na kwamba huenda watu wengi waliopimwa walikuwa wanaumwa tayari ndo maana wanaonekana wapo juu na mikoa mnayosema haina huenda watu bado hawajaanza kuumwa na kupimwa.
  Tathadhari wakuu msile peku eti mkoa wetu ni wa mwisho haujui wa kwanza atakuwa wa mwisho na wa mwisho atakuwa wa kwanza?
   
 19. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hafif, Cha msingi mtie mkeo atosheke, hatokwenda kwa diwani kama katosheka. Wewe unagusagusa tu, Pengine aliyekuwa zamu jana ka-maximize halafu unarudi kwa bi mdogo au wa kati shughuli kwisha kazi. Unategemea nini na bibie utamu anaujua.

  Sijui wewe unaamini mitara au one to one, but cha msingi mkidhi mwezi wakoooo!!!!! kheeeeee
   
 20. c

  cesc Senior Member

  #20
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  dunia imekwishaaaa.....hakuna uaminifu tena ktk ndoa...
   
Loading...