Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 kurudi nyuma mpaka miaka ya 90, tulikuwa na kizazi cha kipekee ya burudani, wazee wa Disco Vumbi. Watoto mwisho saa 12 jioni kisha saa 1 usiku mpaka majogoo ni mwendo wa dancehall.
View: https://youtu.be/souwByxnz0w?si=ImOldzFPAD7fUcmC
Enzi hizo ladies free halafu wanaume mnalipa kiingilio! Wacha kabsa! enzi za kina Dj Cobo, Clubs zilijaa wadada wengi ili kuvutia wanaume kuingia, mwanga hafifu, na sauti nzito za spika zilizoachia muziki ya Jamaica.
Miaka ya 90 kulikuwa na Djs wanajua kucheza na nyimbo kadhaa ili kuwapatia watu kitu roho inapenda, wakazi wa Dar es Salaam kwa wale wahenga wanakumbuka fujo za Magnum, Mambo Club pamoja na New Silent Club, kulikuwa na dundo za ajabu ikifika wakati wa usiku.
Lakini kulikuwa na wakati mmoja uliotawala mioyo ya mashabiki na kuthibitisha ubingwa na ubora wa DJ, au kama walivyojulikana mitaani—Manju muziki: pale dundo la Diwali Riddim ilipoingia kitaa. Hapo ndipo ustadi wa DJ ulipoonekana wazi—si kucheza tu wimbo, bali kusimulia hadithi kwa mpigo mmoja uliovaa nyimbo zaidi ya 45.
Ninamkumbua Zonte wa Zonte wakati akiwa ni boss wa FM Club, yule mzee baba alikuwa akipenda Djs waweke nyimbo ambazo zitaongeza wateja zaidi na sio kuwafukuza.
Chanzo cha hadithi ya dundo hili ni Steven “Lenky” Marsden, mtayarishaji wa muziki wa Reggae kutoka Jamaica aliyesoma mazingira, akaisoma dunia, kisha akaamua kubadilisha mwelekeo wa dancehall, na kupika dundo ambalo lilibadilisha kabsa hali ya hewa.
Stori inaendaje? Ilikuwa mwaka 1998 bwana, Lenky akiwa zake studio alikuwa akipika midundo kadhaa, na akiwa anachezea kinanda ghafla alipata idea kwanini asitumie midundo ya tofauti ambayo ndani ya Jamaica haikuwahi kutokea.
Alijaribu kupiga mdundo wenye asili ya India ambao mara kadhaa hutumika kwenye sherehe za Diwali au maarufu kama Dipavali. Moja ya sherehe kubwa sana kwa wahindu wenye imani ya Jaini pamoja na Wasikhi.
Dipavali ama kwa lugha iliyozoeleka kama Diwali ni sherehe ya ushindi wa kiroho ambao Dharma aliupata dhidi ya Adharma. Kwa wahindu na jamii za wahindi walikuwa na nyimbo kadhaa ambazo walizitumia katika sherehe hiyo.
Mfano nyimbo kama: Jaadu Teri Nazar, Rim Jhim Rim Jhim, Zara Sa Jhoom Loon Main na kama haufahamu tu hata Bole Chudiyan ya Kareena Kapoor & Hrithik Roshan maarufu kama Krish pamoja na Godfather Amitabh Bachchan ni sehemu ya sherehe ya Diwali ukisikilkza utaona mdundo wake
Ila kitu kibaya ni kuwa mwanzoni watu wengi ndani ya Jamaica hawakuelewa kabsa hiyo kazi waliona ni kazi ya ovyo sana. Lenky aliweka udambwidambwi wa sauti ya makofi na jambo hilo halikuungwa mkono kabsa na watu, huku baadhi wakiona ni kama anataka kuharibu muziki wa Dancehall.
Mwamba akarudi ndani na kuipika upya na kuongeza mambo zaidi na mwaka 2002 ndipo aliporudi na kuwapatia tena wajamaika Diwali Riddim. Cha ajabu ni kuwa watu wa mwanzo ambao walilikubali dundo hili na kuona kuwa hiki chuma ni kizito sana walikuwa ni Assassin Zumjay pamoja na General Degree ambao walikubali kuweka mistari yao kwenye dundo hili.
Na dude lilipofika kwenye radio mbalimbali ndani ya Jamaica, aisee Mzee baba Lenky alipigiwa simu kila nyingi kinyama kutoka kwa watu kuhusu dundo ambalo amelipika, watangazaji wa redio kadhaa walionesha kuwa dundo hili litapelekea mabadiliko makubwa kwenye muziki wa Dancehall.
Wiki iliyofuata kila msanii alitamani kuweka naye mstari ni kama dundo lilikuwa linaongea na wao, huku Godfather Elephant Man, kule Bounty Killer, mwanamama Tanya Stevens, Wayne Marshall, Brick & Lace, kundi la TOK na wengine wengi.
Ila ajabu ilikuwa ni moja, Lenky hakutengeneza dundo tofauti bali alikuwa anatumia dundo lile lile, huku akiongeza overdubs, tweaks, layers kuendana na kila tempo ya msanii husika.
Mfano, kwa Sean Paul aliongeza ufundi kwenye kinanda pamoja na violini, hapo tukapata chumba kizito sana cha Get Busy, matokeo yake ni nini? Wimbo huu unakwenda kukishusha mzigo wa 50 Cent cha In Da Club kwenye chati za Billboard Hot 100, na Sean Paul akafungua pazia la vyuma vya Dancehall kuanza kutamba kwenye chati kubwa duniani.
Wayne Wonder naye akaona isiwe kesi akamfuata Lenky na kutengeneza wimbo wa No Letting Go wimbo ambao kama Dj hakuweza kuucheza basi ataishia kupewa matusi na kejeli za kutosha kama sio kupigwa na chupa. Hiki chuma kilikwea mpaka namba 11 kwenye chati za Billboard ndani ya Marekani huku kikipata nafasi ya 3 ndani ya Uingereza.
Mwanadada Lumidee naye akatoka na chuma kwa jina la Never Leave You, wahenga tulikuwa tunasubiria kipande cha Uh Oooh, Uh Oooh. Baraka juu baraka chini, mafanikio makubwa ni pale ambapo Brick & Lace walipokuja na Love is Wicked.
Lakini ajabu ni kuwa hata wimbo wa Rihanna wa Pon de Replay pia ulitumia dundo la Diwali Riddim. Rihanna aliwaacha watu hoi kwani chuma hiki kilikwenda na kukamata namba 2 kwenye chati za Billboard Hot 100. kwa wiki 12 Rihanna akikaa kwenye top 10 na wiki 23 kwenye top 100.
Diwali Riddim ilikuja na mapigo tofauti ya sauti za makofi, sauti yenye asili ya msukumo wa muziki wa dansi za India, na mdundo wa kipekee sana ambao ulikuwa ni kama madawa ya kulevya.
Hiki kipindi ndipo kulizaliwa shughuli za kucheza madenso, wale Prehistoric Human beings tunaelewa vizuri. Mitaani watu walionesha umwamba katika kucheza madenso kwenye nyimbo kama vile: “Get Busy” ya Sean Paul, “No Letting Go” ya Wayne Wonder, “Never Leave You (Uh Oooh, Uh Oooh)” ya Lumidee, “Overcome,” “Elephant Message,” “Sufferer,” “Party Time,” na “Love Is Wicked.”
Kwa DJ yoyote mpaka sasa, kucheza dundo la Diwali Riddim ni alama wa heshima pamoja na kuonesha ubora wake katika kucheza na deck. Kuicheza vibaya ni aibu; kuelewa nyimbo ambazo zimetumia dundo hili kisha kuzicheza vizuri ni baraka ambayo watu ndio hukupatia.
Ndani ya clubs hapa Tanzania, Manju muziki waliitumia kuonyesha timing zao, ufundi wa mixing, na uwezo wa kusoma hadhira. Ulipobadili kutoka “Get Busy” kwenda “No Letting Go,” kisha ukarejea kwa “Party Time,” ulikuwa unajua kuamsha watu haswa.
Jambo hili lilikuwa ni kama lina uchawi ndani yake. Steven “Lenky” Marsden, wewe ni Godfather, kazi yako haikuburudisha tu—iliunganisha dunia kwa mpigo mmoja.