Division two EGM

mgungani

Member
May 13, 2022
38
60
Kijana aliyepata division two EGM anaweza kuchaguliwa UDSM? Je ni kozi gani nzuri kwake? Je asipopata UDSM anaweza kupata chuo gani kingine au kozi gani. Yeye anapenda kozi yeyote.

Je, nimshauri aombe kozi gani nzuri iliyopo chuo gani kikuu yenye uhakika wa ajira anaweza kupata mkopo? mzazi wake ni mkulima.
 
Ni wewe mwenyewe au? Lakini huyo mtu hakupi uwanja wa kumshauri kwa kuwa hajui anataka nini. Kimsingi ilibid umuulize ANA NDOTO GANI? Yaani anataka kuwa nani? Haiwezekan akuambie anataka course yoyote huyo hajielewi.

Anyway mwambie aende NIT asomee mambo ya SHIP MANAGEMENT, pale na mkopo ataweza kupata,au aombe BUSINESS AND AGRICULTURE hapo UDSM, au aende terminal 3 akaulizie cousre nyingi zinazohusu masuala ya usafiri wa anga, au aende udsm akasomee IT, architecture, au chuo cha ubaharia pale awe wakala wa meli au hata nahodha.

Kuna course ya petrolium ang gas management sijui chuo gani wanatoa, au akasomee masuala ya kuendesha magreada na mitambo ya migodini, aisee mtu asiyesema ndoto zake vitu vya kumshauri ni vingi, wajuvi watakuja na mwongozo zaidi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom