'Divide and Rule'

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,044
2,000
Watawala wetu hutuambia kuwa "wakoloni weupe" walitumia njia hii ya kutugawa ili watutawale vizuri, kwa mfano utawala wa Kijerumani nchi yetu Tanganyika ilikuwa imegawanywa sehemu za kiutawala takriban 20 hivi kama Tabora, Kondoa-Irangi, Ujiji, Bismarcburg, Ulanga, Wilhelmstahl, Kilwa, Dodoma, Langenburg, Pangani, Bagamoyo, Mwanza, Rufiji na kadhalika.

Enzi za Kiingereza wao wakaigawa nchi yetu katika majimbo manane tu nayo ni Jimbo la kati, ziwa, magharibi, kaskazini, nyanda za juu, mashariki, Tanga na kusini. Tulipo pata uhuru sie tukageuza majimbo hayo kuwa mikoa na kuzalisha mikoa takribani 20 hivi. Majimbo yalikuwa yamewaunganisha kwa mfano Wanyamwezi, Waha, Wafipa na baadhi ya Wasukuma katika UTAWALA wa JIMBO MOJA tu lakini tulipoanzisha mikoa hii ikatuweka Wanyamwezi peke yao Wagogo peke yao, Wahehe peke yao, Waha peke yao n.k.
Dhambi hii ya 'wagawe uwatawale' bado inaendelea kwa msemo wao wa KULETA MAENDELEO ndio maana tumeona wananchi wa Mpanda wakisherehekea kupata (UHURU) mkoa wao uitwao Katavi. Katika katiba kama hili lisipoainishwa kuwa nchi yetu iwe na mikoa maslani kumi tuu kwa ajili ya UCHUMI tutakuwa na mingi zaidi mpaka MIA.

Rais Kagame wakati akiingia madarakani aliikuta Rwanda ina 'mikoa' mingi na yeye akaipunguza na sasa kila mtu anaitolea mfano nchi hiyo kwa kuendelea kiuchumi.
Tafakari.:evil:
 

NEGLIGIBLE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
356
225
watawala wetu hutuambia kuwa "wakoloni weupe" walitumia njia hii ya kutugawa ili watutawale vizuri, kwa mfano utawala wa kijerumani nchi yetu tanganyika ilikuwa imegawanywa sehemu za kiutawala takriban 20 hivi kama tabora, kondoa-irangi, ujiji, bismarcburg, ulanga, wilhelmstahl, kilwa, dodoma, langenburg, pangani, bagamoyo, mwanza, rufiji na kadhalika.

Enzi za kiingereza wao wakaigawa nchi yetu katika majimbo manane tu nayo ni jimbo la kati, ziwa, magharibi, kaskazini, nyanda za juu, mashariki, tanga na kusini. Tulipo pata uhuru sie tukageuza majimbo hayo kuwa mikoa na kuzalisha mikoa takribani 20 hivi. Majimbo yalikuwa yamewaunganisha kwa mfano wanyamwezi, waha, wafipa na baadhi ya wasukuma katika utawala wa jimbo moja tu lakini tulipoanzisha mikoa hii ikatuweka wanyamwezi peke yao wagogo peke yao, wahehe peke yao, waha peke yao n.k.
Dhambi hii ya 'wagawe uwatawale' bado inaendelea kwa msemo wao wa kuleta maendeleo ndio maana tumeona wananchi wa mpanda wakisherehekea kupata (uhuru) mkoa wao uitwao katavi. Katika katiba kama hili lisipoainishwa kuwa nchi yetu iwe na mikoa maslani kumi tuu kwa ajili ya uchumi tutakuwa na mingi zaidi mpaka mia.

Rais kagame wakati akiingia madarakani aliikuta rwanda ina 'mikoa' mingi na yeye akaipunguza na sasa kila mtu anaitolea mfano nchi hiyo kwa kuendelea kiuchumi.
Tafakari.:evil:
nadhani ulikuwa unamaanisha "divide and rule"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom