Dismas Ten wa Yanga ni zaidi ya msemaji

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
273
500
Kila klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara ina msemaji wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za mchezo huo. Ilizoeleka ukiwa msemaji wa vilabu vikubwa vya Yanga na Simba lazima uwe unasikika na kuwa mtu maarufu sana. Mfano kina Jerry Muro na Haji Manara.

Kwa sasa hapa Tanzania hakuna ubishi kuwa moja ya wasemaji wa vilabu maarufu zaidi nchini kwa sasa ni Ndugu Haji Sunday Manara msemaji wa klabu ya soka ya Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu msimu wa 2017/18 na wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki ambao wanacheza ligi ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi.

Ila leo ningependa kueleza majukumu ya maafisa habari wa vilabu kuwa pamoja na kuhakikisha habari zinazohusu vilabu vyao zinawafikia wadau kwa wakati kwa kuzungumza na waandishi, mitandao ya kijamii, website ya klabu nk, kuitangaza, kuitetea, kuilinda na kuikuza brand ya vilabu vyao pia wanao wajibu wa kuwa wabunifu kwa kuitumia brand ya vilabu vyao kuwa vyanzo vya mapato.

Katika hili afisa habari wa klabu ya Yanga Ndugu Dismas Ten ni mtu mahiri. Amebadili mfumo wa utoaji taarifa mfano masuala yote ya timu na mechi wanazocheza wasemaji ni benchi la ufundi, meneja wa klabu, nahodha na wachezaji wenyewe kwa namna walivyojipanga. Habari hizi anaziweka kwenye website ya klabu ambapo wadau wote huzidownload huko kwa matumizi yao hii imekuwa moja ya chanzo cha mapato kwa klabu, amebuni kipindi cha Yanga TV, amekuwa mbunifu wa muonekano wa sare na mavazi mbalimbali ya klabu ambayo pia yamekuwa kwa kiasi fulani kuchangia mapato ya klabu japo hata yeye amekuwa hafurahishwi na namna zinavyouzwa.

Kwa sasa anakamilisha ubunifu wa muonekano wa skafu, saa, kofia, raba, vikombe vya chai, glass za vinywaji, vikoi, khanga, makava ya simu, opener, holder za funguo, soksi, vitambaa vya mkononi, mikoba au mabegi ya shule, mabegi ya safari, mikoba ya kike, viatu vya wazi, wallet za kike na kiume,headphones,diaries nk

Kama ataendelea kuungwa mkono na viongozi wenzake wa klabu kama ilivyo sasa na klabu ikaweka utaratibu mzuri wa namna klabu itanufaika na nembo yake kwa vitu vitakavyouzwa basi Yanga itauaga umaskini.
IMG_20190221_115143_763.JPG
IMG_20190221_101201_230.jpeg
IMG_20190221_100741_452.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attachments

3llyEmma

JF-Expert Member
Oct 23, 2017
5,012
2,000
Kwa kazi hizo Ten anajitahidi Hongera zake ila Aongeze hamasa kwa mashabiki wasiwe wavivu kuja uwanjani kuisapoti timu ukizingatia inapitia wakati mgumu wa kifedha.

Mwisho: Msitegemee Skafu,saa,vikoi,mabegi n.k kumaliza umasikini wa Yanga kwa Tanzania hii, Cha msingi ni mfumo bora wa kuendesha Klabu hii ili haya ya Dismas Ten yawe Ziada tu.
Akhsante
 
MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
824
1,000
He is doing his job professionally we agree BRAVO
BUT NEEDS TO BE MORE ACTIVE....kwenda na wakati ona hata Timu AFCON ILIYOUNDWA KAWEKWA JERRY MURRO NA MANA,MANARA AS IF DISMAS TEN HAWAMUONI ……..
watu wanataka hamasa Zaidi kuliko coloured advets ...Mzeee kiako cha leo Yanga no feed back mpaka sasa mchana...huuuu
 
MUSONI

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
824
1,000
YANGA DAIMA WATATUJUA MWAKA HUU PAMOJA NA FIGISU KIBAO....Karia kushinda na viongozi wa SIMBA …kuwa na vipolo kibao tunao tu mdogo mdogo wakati wanarudi AIRPORT sie NDIO TUNAONDOKA.....
 
Attachments

kisepi

JF-Expert Member
Jun 9, 2015
1,886
2,000
Kila klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara ina msemaji wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za mchezo huo. Ilizoeleka ukiwa msemaji wa vilabu vikubwa vya Yanga na Simba lazima uwe unasikika na kuwa mtu maarufu sana. Mfano kina Jerry Muro na Haji Manara.

Kwa sasa hapa Tanzania hakuna ubishi kuwa moja ya wasemaji wa vilabu maarufu zaidi nchini kwa sasa ni Ndugu Haji Sunday Manara msemaji wa klabu ya soka ya Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu msimu wa 2017/18 na wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki ambao wanacheza ligi ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi.

Ila leo ningependa kueleza majukumu ya maafisa habari wa vilabu kuwa pamoja na kuhakikisha habari zinazohusu vilabu vyao zinawafikia wadau kwa wakati kwa kuzungumza na waandishi, mitandao ya kijamii, website ya klabu nk, kuitangaza, kuitetea, kuilinda na kuikuza brand ya vilabu vyao pia wanao wajibu wa kuwa wabunifu kwa kuitumia brand ya vilabu vyao kuwa vyanzo vya mapato.

Katika hili afisa habari wa klabu ya Yanga Ndugu Dismas Ten ni mtu mahiri. Amebadili mfumo wa utoaji taarifa mfano masuala yote ya timu na mechi wanazocheza wasemaji ni benchi la ufundi, meneja wa klabu, nahodha na wachezaji wenyewe kwa namna walivyojipanga. Habari hizi anaziweka kwenye website ya klabu ambapo wadau wote huzidownload huko kwa matumizi yao hii imekuwa moja ya chanzo cha mapato kwa klabu, amebuni kipindi cha Yanga TV, amekuwa mbunifu wa muonekano wa sare na mavazi mbalimbali ya klabu ambayo pia yamekuwa kwa kiasi fulani kuchangia mapato ya klabu japo hata yeye amekuwa hafurahishwi na namna zinavyouzwa.

Kwa sasa anakamilisha ubunifu wa muonekano wa skafu, saa, kofia, raba, vikombe vya chai, glass za vinywaji, vikoi, khanga, makava ya simu, opener, holder za funguo, soksi, vitambaa vya mkononi, mikoba au mabegi ya shule, mabegi ya safari, mikoba ya kike, viatu vya wazi, wallet za kike na kiume,headphones,diaries nk

Kama ataendelea kuungwa mkono na viongozi wenzake wa klabu kama ilivyo sasa na klabu ikaweka utaratibu mzuri wa namna klabu itanufaika na nembo yake kwa vitu vitakavyouzwa basi Yanga itauaga umaskini. View attachment 1028005 View attachment 1028007 View attachment 1028008

Sent using Jamii Forums mobile app
Kagereeeeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kobello

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
6,922
2,000
Yanga ninayoijua ina rangi za chama kijani na njano. Hakuna zaidi
Ndiyo maana ukaambiwa huijui Yanga.
Rangi asili ni kijani na nyeusi. Kijani kuashiria ubichi au ujana na nyeusi kuashiria uafrica.
Amini hilo, mimi ni yanga damu wa kurithishwa na naijua VIZURI.
Rangi nyeusi ni kitu muhimu sana kwa Yanga, Manji anajua hilo na ndiyo inayotusababisha tuchekwe sasa hivi lakini tutafanikiwa tu kwani hata binadamu mweusi ni mtu anayechekwa sasa hivi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom