Dismas Ten wa Yanga ni zaidi ya msemaji

Huyu jamaa ndo anawavalisha yanga masweta mchana wa jua kali? Wanaishiwa maji mwilin kwa kutokwa na jasho... Hana akili kabisa.
 
Msemaji bora wa wakati wote kwa timu ya wananchi ni zahera mkongomani
 
Kila klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara ina msemaji wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za mchezo huo. Ilizoeleka ukiwa msemaji wa vilabu vikubwa vya Yanga na Simba lazima uwe unasikika na kuwa mtu maarufu sana. Mfano kina Jerry Muro na Haji Manara.

Kwa sasa hapa Tanzania hakuna ubishi kuwa moja ya wasemaji wa vilabu maarufu zaidi nchini kwa sasa ni Ndugu Haji Sunday Manara msemaji wa klabu ya soka ya Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu msimu wa 2017/18 na wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki ambao wanacheza ligi ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi.

Ila leo ningependa kueleza majukumu ya maafisa habari wa vilabu kuwa pamoja na kuhakikisha habari zinazohusu vilabu vyao zinawafikia wadau kwa wakati kwa kuzungumza na waandishi, mitandao ya kijamii, website ya klabu nk, kuitangaza, kuitetea, kuilinda na kuikuza brand ya vilabu vyao pia wanao wajibu wa kuwa wabunifu kwa kuitumia brand ya vilabu vyao kuwa vyanzo vya mapato.

Katika hili afisa habari wa klabu ya Yanga Ndugu Dismas Ten ni mtu mahiri. Amebadili mfumo wa utoaji taarifa mfano masuala yote ya timu na mechi wanazocheza wasemaji ni benchi la ufundi, meneja wa klabu, nahodha na wachezaji wenyewe kwa namna walivyojipanga. Habari hizi anaziweka kwenye website ya klabu ambapo wadau wote huzidownload huko kwa matumizi yao hii imekuwa moja ya chanzo cha mapato kwa klabu, amebuni kipindi cha Yanga TV, amekuwa mbunifu wa muonekano wa sare na mavazi mbalimbali ya klabu ambayo pia yamekuwa kwa kiasi fulani kuchangia mapato ya klabu japo hata yeye amekuwa hafurahishwi na namna zinavyouzwa.

Kwa sasa anakamilisha ubunifu wa muonekano wa skafu, saa, kofia, raba, vikombe vya chai, glass za vinywaji, vikoi, khanga, makava ya simu, opener, holder za funguo, soksi, vitambaa vya mkononi, mikoba au mabegi ya shule, mabegi ya safari, mikoba ya kike, viatu vya wazi, wallet za kike na kiume,headphones,diaries nk

Kama ataendelea kuungwa mkono na viongozi wenzake wa klabu kama ilivyo sasa na klabu ikaweka utaratibu mzuri wa namna klabu itanufaika na nembo yake kwa vitu vitakavyouzwa basi Yanga itauaga umaskini. View attachment 1028005View attachment 1028007View attachment 1028008

Sent using Jamii Forums mobile app
Yupo smart sana Siyo mropokaji kama jinga jinga la mikia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom