Dira ya nchi yetu Tanzania ni ipi?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
2,998
2,000
Salaam wana JF
Naomba kuuliza hivi nchi yetu hii ina dira yoyote ya maendeleo ambayo inaendelezwa na viongozi? Manake kila rais wa nchi hii akiingia madarakani anakuja na Sera na dira zake akiondoka zinakufa kifo cha mende chalii
1.Mkapa kaja na Uwazi na Ukweli akabinafsisha mashirika ya umma kaondoka madarakani hakuna kilichoeleweka nchi ikaendelea Kuwa maskini na Watanzania wakaendelea Kuwa maskini wa kutupwa

2.JK kaja na maisha Bora kwa kila mtanzania na akaja na Sera ya kilimo kwanza na matokea makubwa sasa( Big Results Now) kaondoka kaacha kilimo kipo mahututi,kaacha umaskini wa kutupwa ingawa baadhi ya Watanzania wajanja walinufaika na utawala wake ,BRN sijui iliishia wapi
3.JPM huyu kaja na sera ya Tanzania ya viwanda Lakini hadi sasa sioni kinachoendelea zaidi ya matukio mara kutumbua,mara kuteua mara Makinikia kushtukia 2020 hiyo hakuna la maana tutakalopata zaidi ya kuendelea na shida na umaskini wa kutupwa
Mnijuze nchi yetu hii ina mpango gani endelevu wa maendeleo manake kila anaekuja anakuja na taratibu zake ambazo kimsingi naona zinarudisha nyuma maendeleo.
 
Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,294

Utaelewa tu ukitumbuliwa au Kama vipi shauri tuje Na sera ya taifa ipi maana kulalamika hakusaidii
 
kobokocastory

JF-Expert Member
Aug 30, 2014
1,059
2,000
Tatizo taifa halina long term & short terms economic masterplans ndio maana kila awamu ya utawala inakuja na kauli mbiu au malengo mapya pasipo kutaka kujua tawala zilizopota ziliishia wapi ili kuwa na muendelezo mzuri.

Mfano mzuri jirani zetu wakanya walijiwekea dira yao chini ya utawala wa rais kibabi (KENYA TOWARDS VISION 2030) na utekelezaji wake umeendelea hata baada ya rais kibaki kuondoka madarqkani serikali ya kenyatta bado wanatembelea blue print ya vision 2030.

Kimsingi serikali yetu inatakiwa iwe na mpango mkakati ambao itawezesha awamu inayoingia madarakani kuwa na muendelezo wa pale awamu iliyopita ilipofikia. Kwa mfano kilimo kwanza imebaki story, Matokeo Makubwa Sasa ( Big Results Now) imekufa sijui kifo gani sasa hivi tuko kwenye Tanzanoa ya viwanda.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom