Dini na kabila vina mchango gani katika mahusiano?

mshai

Senior Member
Sep 10, 2014
104
38
habari ya ninyi wana JF

napenda tujadili kiasi gani mahusiano yanaathiriwa na tofauti ya dini au kabila au vyote kwa pamoja...

Nimeamua kutupia huu uzi kwa sababu huwa nackia sana kuhusu hii kauli 'mapenzi hayachagui dini wala kabila'
Na wakati mwingine unasikia wengine wanaapa kuwa hawezi kuoa / kuolewa na mtu wa dini/ kabila fulani.

Swali linalohitaji maoni yako mkuu
Ni kwamba ww binafsi unaonaje kuhusu nguvu ya tofauti ya dini/kabila baina yako na mwenzi wako katika mahusiano yenu..?
 
Mapenzi huanzishwa kwa makubaliano ya watu wawili katika mambo kadha wa kadha na changamoto kubwa hapo inaweza kuwa Dini kuliko Ukabila maana hiyo hushirikisha hadi wazazi wa wapendanao...Na wakati mwingine wapendanao wasipokuwa strong katika maamuzi yao wanaweza kuachanishwa na wazazi maana mzazi wa upande mmoja anaweza kukataa mtoto wake kutoka katika Dini yake na anasema bora uachane na huyo MUME/MKE..Kuliko ubadili dini...
Mara nyingi maamuzi ya mwisho yanategemea sana misimamo ya wapendanao pindi changamoto hizo zinapojitokeza..
 
Dini au kabila ni chanzo cha kudhoofisha maelewane baina ya watu kwa watu na jamii pia, hasa suala hili la mapenz,, binafsi napinga sana kitendo cha kuwatenganisha au kutowaunganisha wawili wanaopendana kisa kuna utofaut wa Dini ama kabila,
 
Love is chemical.

Emotions zote huwa ni chemical reaction ndani ya ubongo kabla hazijahamia moyoni.

Mapenzi yakikufanya kuacha dini(kumkana Mungu unayemuamini), basi hata maisha yatakushinda pia.

Siku zote kama mwanaume anatakiwa aongozwe na kichwa halafu moyo ndio ufuate, ukiruhusu moyo uongoze kichwa unavua sifa ya kuitwa mwanaume.

Ninapinga mtu kukana dini yake kwa sababu ya mapenzi(chemical reaction in the brain)
 
Pia tatizo kubwa lipo kwa wazazi, wakubwa wa familia na jamii inayowazunguka,, huku ndio kuna tatzo mno
 
Love is chemical.

Emotions zote huwa ni chemical reaction ndani ya ubongo kabla hazijahamia moyoni.

Mapenzi yakikufanya kuacha dini(kumkana Mungu unayemuamini), basi hata maisha yatakushinda pia.

Siku zote kama mwanaume anatakiwa aongozwe na kichwa halafu moyo ndio ufuate, ukiruhusu moyo uongoze kichwa unavua sifa ya kuitwa mwanaume.

Ninapinga mtu kukana dini yake kwa sababu ya mapenzi(chemical reaction in the brain)

Love chemistry
 
nitavumilia ukabila ila dini NO!!!!! imagne muslim vs christian----- hapana hapo tutadanganyana tu.
 
1466606366790.jpg
 
Uhuru wa moyo kumpenda mtu bila kuangalia dini au kabila lake kwa kuangalia vigezo vingine ambapo moyo wako unapenda, mfano uzuri wa sura, tabia, umbo, life style yake, rangi yake, urefu/wembamba/unene, elimu, utajiri au background yake nk.

Dini zina mfumo na utaratibu wake na kabila zina mila na desturi zake..
Ikitokea wapendanao wamependana bila kuchagua dini au kabila maana yake itabidi waweke tofauti zao pembeni bila kufuata dini, mila na desturi zao zinataka nini labda kwenye mambo muhimu.

kwa hiyo inabidi wote/ mmoja wapo alegeze uzi akubali kuacha maamrisho ya dini yake, baadhi ya mila na desturi ili kupatikane uwiano.
 
Kiukweli naweza olewa na mtu Wa kabila tofauti na langu ila napo nabagua kidogo lakini mutu isiyo ya dini yangu, bas tena!!!! Cwez kumkana Mungu kwa sababu ya mutu.
 
Kiukweli naweza olewa na mtu Wa kabila tofauti na langu ila napo nabagua kidogo lakini mutu isiyo ya dini yangu, bas tena!!!! Cwez kumkana Mungu kwa sababu ya mutu.
Yule mchumba wako mpya uliempata mzima?.......Msalimie!
 
kabila na dini vinatengeneza kitu tukiite "value system". manake maamuzi yako, ndoto zako, vyenye maana kwako, visivyoruhusiwa kwako vinatokana na misingi ya dini ulikulia pamoja na familia ulikotoka "kabila". ss wewe una amini mbuzi ni chakula mwenzio ana amini mbuzi ni dhambi kubwa sana kula, usiku si mtalala njaa. kuanzisha mahusiano watu especially wenye dini tofauti wengi hua wenye ni wale wanachukulia dini poa.. wanaweza dumu japo kwa shida. sbb waliokolewa ata marafiki wa dini nyingine hawana.
kabila kwa maisha ya kuchanganyikana mashuleni, makazini na alichofanya nyerere kutofanya sawa haina madhara sana kwenye uhusiano paka ukute mwenye kabila lake kweli..
 
Back
Top Bottom