Star
JF-Expert Member
- Dec 5, 2007
- 461
- 4
Nimeshindwa kuitafutia mada hii, sanduku. Hatimae nimeiweka hapa kwa wakufunzi walete moto moto zao. Dini au siasa. Ningeweka ktk dini nahofia ingehamishwa na ningeweka katika siasa ingelikua kinyume chake.
Lengo: Ni mambo yanayoendelea nchini Marekani kila kukicha kuhusu uchaguzi mkuu wa urais, tukielekea mwezi wa November mwaka huu Allah akutuweka hai. Mambo sio madogo. Nchi iliyokuwa ikiheshimika kwa human right sasa inajikuta ni ya mwanzo katika matusi, ubaguzi wa kidini na rangi.
Kweli, imenuuma sana kuona ndugu yetu mwenye asili ya jirani zetu (Wakenya) Baraq Obama akitukanwa matusi ya nguoni na Mgombea mweza katika chama chao cha Democratic. Nimeiona kwa macho yangu video hii, Hillary Clinton akimwambia Obama '..ulikuwa ukileta vijisheria vyako vya kiislamu vya kigaidi...' Hili lilitokea jana katika Debate inayowaelekeza katika kupigiwa kura Jumamosi inayokuja katika Jimbo maarufu lilopata nakama hivi karibuni Carolina ambalo wakaazi wake wengi ni wenye asili ya Africa.
Pia imekuwa ikitembezwa barua hivi karibuni, kua Obama ni Muislamu, aliapishwa kuwa Senetor wa Jimbo kwa kutumia Quran. Ingawa mwenyewe Obama ameyakanusha hayo. Pia barua ikieleza kwa sababu baba wa Obama ni Muislamu, na baba wake wa kambu ni muislamu, na alikulia na kusoma katika nchi yenye waislamu wengi Indonesia. Hili limekuwa ndio silaha kubwa kwa wapinzani wake.
Kwakweli mimi nikiwa kama Muislamu, nashangaa nchi kama Marekani inaonesha wazi kuwa wana chuki dhidi ya Waislamu (in general). Yaani Muislamu ana kosa gani katika duniani hii? Kama uvamizi wameshafanya, kama mali (mafuta) wameshaiba tena nini chengine? Hata uhuru basi tunyimwe?
Tafadhali kama una hoja weka, lakini isiwe vioja na kunitukana, labda kuna pahala nimekosea nisamehe. Ahsante