Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Sisi Wakazi wa Tabata Segere kwa Bibi tuna changamoto ya Barabara ambayo inaelekea Hospitali ya Segerea, kuna dimbwi kubwa la maji ambalo linazuia wapita njia, pikipiki, na magari madogo kupita. Magari makubwa tu ndiyo yanayoweza kupita angalau yakiwa na uhakika hayatapata tabu sana.
Hali hiyo tumesharipoti Serikali za Mtaa lakini hakuna kinachofanyika, tunapata athari kwa biashara mvua ikinyesha, maji machafu yanaingia ndani ya fremu za biashara, jambo linalosababisha wafanyabiashara kufunga maduka yao kwa kukosa wateja na uharibifu wa mali.
Barabara hiyo ni muhimu kwa sababu inatumiwa na magari ya wagonjwa (Ambulance) na wajawazito wanaoelekea hospitalini, lakini sasa imekuwa hatari kwani watu wanadumbukia kwenye maji.
Tulitoa taarifa Serikali ya Mtaa tangu mwezi wa tisa Mwaka 2025 lakini wanatuambia suala hilo liko mikononi mwa mhandisi (engineer) bila hatua zozote kuchukuliwa hadi sasa.