Dimba la Benjamin Mkapa kufungwa

Dimba la Benjamin Mkapa kufungwa

Capo_di_Tutti_Capi

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
111
Reaction score
168
Shirikisho la soka Afrika (CAF) limeshauri kutotumika Dimba la Benjamin Mkapa ili kufanyiwa marekebisho kwa kile wanachodai kuwa eneo la kuchezea (pitch) limeharibika.

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakochezwa leo kati ya Yanga SC na KMC FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam utafungwa kwa mwezi mmoja kupisha marekebisho hasa kwenye eneo la kuchezea.

Meneja wa uwanja huo Salum Mtumbuka amesema kuwa baada ya michezo miwili ya mashindano ya Afrika mwishoni mwa wiki walikutana na maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika ambao waliwapa maelekezo ya kufanya marekebisho hayo.

"Tulikubaliana na CAF wakati marekebisho yanaendelea, mechi zitakazochezwa hapo labda zile za kimataifa za CAF na timu ya Taifa. Mechi nyingine za ligi kuu watatumia Uwanja wa Uhuru au viwanja vingine," amesema Mtumbuka

Credit by @fumo255
View attachment 2527029
 
NCHI HII KUNA WATU WANAPEWA KAZI KUWA NA UWEZO WA KAZI HUSIKA. INA MAANA HUYO MENEJA WA UWANJA HAKUONA KUWA PITCH IMECHOKA MUDA TU?
 
Back
Top Bottom