Dili la usafiri; Mbeya/Dar/Mbeya

Dili la usafiri; Mbeya/Dar/Mbeya

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,819
Reaction score
802
Katika kuendelea na mchakato wa matumizi ya Noah niliyo nayo hapa Mbeya; nimeanza safari za Mby/Dar/Mby nikitoka jioni hapa Mbeya na kuelekea Dar ambako nafika alfajiri.

Ila biashara hii kama walivyocomment watu humu.. Ina changamoto zake.. Hasa uhakika wa kupata abiria wa kutosha Noah (8-9). ikitokea hivyo unaweza usipate kitu ukaishia kuweka mafuta tu. Pia kwa mchana ni shida kwa kuwa Trafic police wanakuwa kazini maeneo mengi, japo usiku pia kwenye check point kama kawaida, wakiona Noah tu wanajua ni dili.

Nimefikiri kuwa ningekuwa sometimes napata watu kwa oda wenye malengo yanayo fanana kutoka dar-mbeya na Mbeya dar kama vile wafanya biashara wangekuwa wanaji organise wao au mizigo yao mimi nitawabebea. Kupeleka Mbeya/Dar....
Kama ni wao abiria pia ingekuwa poa zaidi.

FAIDA YAKE;

  1. Kusafiri wakati wanaopenda wao mfano jioni ili wafike Dar/Mby asbh.
  2. Kuagiza mizigo yao midogo kwa umbo lakini yenye thamani ikafika vema
  3. Kufika kwa wakati na kuwa na control na safari nzima (kula , kupumzika, kuchimba dawa nk) nk

Kwa wazo hili naomba ushauri na jinsi ya kufikia wazo hili kiutekelezaji (kama linafaa kujiingizia kipato kutumia mali mtu aliyonayo).

KUMBUKA: safari nimeshaanza, ila kutegemea abiria wa kudalaliwa na wapiga debe kwenye vituo vikuu, hailipi kivile; kuna abiria alitoa nauli sh 40,000 Mby-Dar; mimi nikaambiwa ametoa 35,000 na bado nimpe jamaa elfu 5.. duh?!!
 
We IPILIMO,
Mifano yako mingi ni ya kuigiza ndio maana mpaka leo watu hawachangii uzi huu.
Maana unajichanganya kwenye maelezo yako,inaoneakana kama unafanya research ya biashara vile.

Hembu eleza.

-Dar-Mbeya-Dar ni km ngapi
-Na unatumia mafuta kiasi gani,
-Na je umeisajili kama gari ya Biashara
-Je umepewa kibali na sumatra kwa route hiyo kwa uwezo wa gari lako?
-Kutoka mbeya kuja Dar unaweza kupata Abiria kwa kupitia madalali kwa kuwa mbeya ni kwenu,je ikifika Dar kurudia huko inakuwaje kwenye kupata Abiria ndani ya siku moja
-Faida kiasi gani kama ikipata abira kamili kwa round trip
-Driver unamlipa kiasi gani kwa siku

Ni hayo tu,maana kama umeishaanza basi majibu yake ni mepesi sana
 
Back
Top Bottom