"Dikteta" Nyerere alipotua White House in a State Visit 1963 [VIDEO]

Swali la kujiuliza, kama kweli Nyerere alikuwa kiongozi bora, kwa nini hakuweza kuwasikiliza Mawaziri wake, washauri wake ktk mambo ya Uchumi?

swali hili zuri; mawaziri wake na washauri wake walimshauri kitu ambacho hakuwasikiliza?
 
Labda tuliweke sawa swali zima..Nini maana ya Dikteta.
Wadhungu wanasema:-
A government controlled by one person, or a small group of people. In this form of government the power rests entirely on the person or group of people, and can be obtained by force or by inheritance. The dictator(s) may also take away much of its peoples' freedom.

Kufikia hapa tu, tafsiri nzima inamvaa vizuri Mwalimu na chama CCM kama suti, yaani toka muundo wa katiba, nguvu ya mamlaka ya rais, chama kimoja, baraza la mawaziri na uongozi wa serikali, Bunge, kuweka njia za uzalishaji mikononi mwa serikali na kadhalika.

Hivyo vyote vinamfanya Nyerere na CCM kuwa Madikteta toka wakati ule hadi leo na ndio maana Chadema inapigana kurudisha madaraka hayo kwa wananchi ingawaje mimi binafsi bado naamini kabisa kwamba Watanzania ni Kondoo ambao siku zote wanahitaji mchungaji mwenye bakora mkononi. Na hapa ndio napompendea Mbowe, kila wakimwita Dikteta ndio nampenda zaidi na zaidi!

Hivyo kuwa Dikteta sio kosa wala dhambi inategemea na unawaongoza watu gani na unakusudia kuwapeleka wapi, makosa makubwa ya Nyerere tumeshindwa kuyarekebisha, baadhi tumeogopa kuyagusa kabisa kwa sababu yataondoa nguvu ya chama CCM na viongozi wake (Udikteta) na tukachagua yaliyokuwa rahisi na kwa maslahi ya viongozi wale wale..

Kwa mfano ktk Ubinfsishaji ili kuondokana na Azimio la Arusha, tumeondoa serikali kumiliki hizo njia za kiuchumi lakini tumehalalisha viongozi (ambao ni CCM na serikali) kukamata na kuhodhi njia kuu (commanding heights) kwa kushirikiana na wageni. Yaani tumeondoa Utaifishaji toka serikalini na kuiweka mikononi mwa viongozi kama vile tumetoa fedha mfuko mmoja wa suruali kwenda mfuko mwingine.

Na kati ya makubwa tuloshindwa kuyagusa ni nguvu ya rais, baraza la mawaziri, muundo wa serikali, muundo wa Uwakilishi (Bunge), Muundo wa Halmashauri za miji (ushiriki wa RC na DC).

Haya maswala niloorodhesha hapo yanakifanya chama cha CCM kuendelea kuwa Madikteta na marais wao wote toka Nyerere hadi JK ni Madikteta kwa sababu wananchi hawana sauti na kubadilisha lolote kati ya hayo pasipo viongozi wa CCM kuridhia..

Hapa ndipo unapokuta vyama vya upinzani vinajicontradict wenyewe na policy zao. Wanamsifia Nyerere ambaye ndiye mwanzilishi wa sera hizo za Udictator, halafu wanalalamika CCM inatumia power za kiubabe ktk kutuliza maandamano yao. Wakati wa Utawala wa Nyerere kulikuwa na maandamano ya kupinga utawala wake, na Nyerere mwenyewe akatoa statement ipo kwenye video clip kwamba " I have sufficient power under the constitution to be a Dictator... and this is dilemma.." Ametumia dilemma kuwajulisha wale wanaondamana, kwamba atatumia power kwa njia yoyote ili kuwatuliza wale wanaondamana.
TZ kuendelea mbele ktk mfumo wa sheria, freedom, lazima WTZ wajulishwe kwanza, kwamba Nyerere hakuwa kiongozi mzuri, kwa sababu hakuwapa freedom WTZ kama binadamu. Tukisolve issue tutaweza kuendelea mbele kama nchi yenye demokrasia also checks and balance.
 
Naona wafuasi wa Dictator Nyerere washaanza kampeni zao za kumtukuza Dictator
 
Hapo kwny red unasema watz wote ni kondoo!nlipenda argument zako bt ulivosema watz ni kondoo nkajua fika kwamba unafikiria kwa kutumia masaburi.
 
I'm very happy to be in the White House today as your guest, just as I was the guest of your distinguished predecessor and my friend, the late President Kennedy, in 1963.

Hapo kwenye Red nimejiuliza kama huyu jamaa ambaye kina Salva wanadai ni rafiki wa Obama, anaweza kutamka maneno hayo kwamba Obama ni rafiki yake akiwa Marekani? Kumbuka kwamba maneno hayo Mwalimu aliyatamka akiwa White Houes mbele ya wamarekani wenyewe. Na hakutafuna maneno kwamba Carter naye ni rafiki yake.

Pia akawaambia wazi malengo ya nchi yake kuwasaidi watu wa Kusini mwa Afrika kuondokana na Ukoloni na ubaguzi wa rangi ingawa ilijulikana wazi Marekani na Uingereza ilikuwa inawaunga mkono walowezi hao Kweli jamaa alikuwa ni MWALIMU!!
 
wewe umekosa adabu tu pia siyo utu wema kumjadili marehemu kwa sababu hawezi kujibu tuhuma dhidi yake na walio hai hawana mamlaka ya kumjibia unless wawe na"lasting power of attorney" yaani ruhusa ya kisheria iliyo tolewa na marehemu kabla hajafa inayowapa mamlaka ya kumsemea.

Hisia zangu ni kwamba wewe unasumbulia na udini, mipango ya watu wenye mawazo potofu kama wewe ni kuwachafua na kuwadhalalisha wenye imani tofauti na nyie ( wafu na waliohai) ili dini yenu ionekane bora na superior. Mpango wenu wa muda mrefu ni dini yenu kushika hatamu za siasa, serkali, uchumu, imani na hali ya maisha ya kila siku ya watanzania wote kama wanavyofanya huko misri, sudan, somalia nk

Nyerere siyo kiongozi pekee wa ngazi za juu wa JMT ambaye ni marehemu, wapo akina Karume, Kawawa, Sokoinne nk. Iweje yeye tu ndo marehemu mbaya na dikteta. Vipi marehemu Karume yeye hakuwa dikteta?

Tukirudi kwa waliohai, Mambo mengi yanazungumzwa juu ya Mkapa na ufisadi lakini hakuna anayetaja ufisadi wa Mwinyi, kwa nini? Wakati wa Mwinyi kulikuwa na ufisadi wa nguvu pia kama wa akina Chavda, Loliondo nk. Mbona Mkapa alianzisha tume ya Warioba ambayo ilibaini ufisadi uliokuwa umekithiri kwenye serkali ya Mwinyi, baadhi ya watuhumiwa pia walifikishwa mahakamani, lakini hakuna mtu anaongelea ufisadi wa wakati huo??? Mama Sitti hakutuhumiwa kwenye kashifa za kifisadi? Mch. Mtikila alipata misukosuko mingi kwa kutaja hadharani mafisadi, siku hizo akitumia msamiati wa magabachori

MMKJJ huwezi kuyasema hayo kwa sababu yalitendwa na waungwana siyo? Wabaya ni JKN, BWM, EL, Sumaye, AC na RA aliyetolewa kafara ili kufunika kombe wanaharamu apite. Mnaipeleka nchi pabaya hasa kwa wale wenye imani tofauti na ninyi..

Uchafu wa serikali ya Mwinyi ulisafishwa na serikali ya Mkapa in few months, ndio maana umesahauliwa, na kama ataayemfuata JK atasafisha nchi na kuirudishia heshima inawezekana hata JK tutamsahau kabisa.
 
Hapa ndipo unapokuta vyama vya upinzani vinajicontradict wenyewe na policy zao. Wanamsifia Nyerere ambaye ndiye mwanzilishi wa sera hizo za Udictator, halafu wanalalamika CCM inatumia power za kiubabe ktk kutuliza maandamano yao. Wakati wa Utawala wa Nyerere kulikuwa na maandamano ya kupinga utawala wake, na Nyerere mwenyewe akatoa statement ipo kwenye video clip kwamba " I have sufficient power under the constitution to be a Dictator... and this is dilemma.." Ametumia dilemma kuwajulisha wale wanaondamana, kwamba atatumia power kwa njia yoyote ili kuwatuliza wale wanaondamana.
TZ kuendelea mbele ktk mfumo wa sheria, freedom, lazima WTZ wajulishwe kwanza, kwamba Nyerere hakuwa kiongozi mzuri, kwa sababu hakuwapa freedom WTZ kama binadamu. Tukisolve issue tutaweza kuendelea mbele kama nchi yenye demokrasia also checks and balance.


There is no doubt that JKN was a dictator, ie he had absolute powers and he was absolute ruler. Kwanza aliconsolidate power kwenye chama (kwa kupiga marufuku kisheria vyama vyote vya siasa na freedoma of media), kwa hiyo kulikuwa na party dicatorship, na ndani ya party madaraka yalilimbikizwa kwa kamati fulani, na kwenye hiyo kamati madaraka yalilimbikizwa kwa Nyerere na marafiki zake. Hata kwenye upande wa serikali hali ilikuwa hivyo hivyo rais alikuwa na absolute powers.

LAKINI Je, ni vipi alitumia madaraka hayo? alitumia kujinufaisha yeye na wenzake au kuihujumu Tanzania na waafrika wenzake?

JK anasifiwa kuwa ni liberal, si didkteta, lakini katiba ni ile ile aliyoitumia Nyerere labda ina viraka vinne au vitano kuhusu "uhuru" kisiasa wa vyama vingi, "freedom" of media etc etc

LAKINI angalia nchi inavyokwenda, wezi wanaiba hela na wanajulikana kabisa na anasema hadharani rudisheni nawasamehe, unasikia kabsia kwenye wikileaks Rais wetu alihingwa dola milioni 1, au alikwenda kununuliwa suti......

Cha maana ni nini hapa? Results za kazi za mtu fulani bila kujali jina lake, au jina lake bila kujali results zake.
 
Nyerere was very smartman ila akili yake ilianza kuwa MBOVU baada ya kuja na idea zake za azimio la Arusha na UPUMBAVU wa kusaidia independence za nchi nyingine za Africa bila kuangalia maslahi ya wananchi wake kwanza...na kilichommaliza na kumaliza Taifa kwa ujumla ni siasa zake za KIJINGA za ujamaa na kujitegemea.

great thinking
 
Nyerere was very smartman ila akili yake ilianza kuwa MBOVU baada ya kuja na idea zake za azimio la Arusha na UPUMBAVU wa kusaidia independence za nchi nyingine za Africa bila kuangalia maslahi ya wananchi wake kwanza...na kilichommaliza na kumaliza Taifa kwa ujumla ni siasa zake za KIJINGA za ujamaa na kujitegemea.

great thinking
 
Back
Top Bottom