Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,188
- 8,215
DIDIER DROGBA, TUNAPASWA KUAMINI TU.
.
Chelsea wakisherehekea miaka nane ya taji la klabu bingwa Ulaya mwaka jana, Didier Drogba aliombwa azungumze chochote kuhusu taji lile.
Drogba alisema hataizungumzia mechi kwasababu kila mtu alitazama, kwa heshima kubwa alisema atatoa kisa kifupi kumuhusu yeye na Juan Mata kuelekea ubingwa ule. Hadithi yenyewe hii hapa.
Miaka nane iliyopita meneja wetu Andre Villas Boas alifukuzwa, wachezaji tulifanya kikao cha pamoja, tulihisi kama tunahusika kwa kiasi fulani kufukuzwa kwa kocha wetu.
Nahodha wetu John Terry alizungumza, Frank Lampard, Peter Cech na waandamizi wote kwenye timu walizungumza.
Tulikubaliana tutoe kila kitu kwa ajili ya mashindano ya Ulaya. Licha ya kwamba tulishapoteza 4-1 dhidi ya Napoli, tulisema tuweke akili zetu zote kuwa tunahitaji klabu bingwa.
Baada ya kile kikao nilimfuata Juan Mata, kijana mdogo wa miaka 23 na kumuambia, "Tafadhali Maestro, naomba unisaidie kushinda taji la klabu bingwa Ulaya"
Alinitazama na kuniambia, "Didi! Acha ukichaa. Wewe ndiyo unapaswa kunisaidia mimi kushinda klabu bingwa" Nilimuambia, "Nimekuwa hapa kwa miaka nane na sijawahi kushinda, naamini wewe ndio utatusaidia kushinda wakati huu."
Hiyo ilikuwa mwisho wa February na miezi mitatu baadae tulikuwa Munich, uwanja wa nyumbani wa wapinzani wetu. Rangi zao zilikuwa zimetawala uwanja.
Walitufunga dakika ya nane kabla mechi kuisha. Nilivunjika moyo sana, wakati naenda katikati kuanzisha mpira Juan Mata aliniambia, "Didi, amini tu! Amini tunaweza"
Nikiwa nakaribia kumwaga machozi nilimuambia, "niamini nini tena Juan? Zimebaki dakika nane tu nilie kama nilivolia miezi michache iliyopita nilipopoteza fainali ya AFCON nikiwa na Ivory Coast.
Dakika ya mwisho tulipata kona, kona ya Kwanza kwetu dhidi ya 18 walizopiga Bayern Munich. Mata alinifuata tena na kuniambia,
"Didi bado unaamini? Kama huamini sitakwenda kupiga. Nilitazama jukwaani na kuwatazama mashabiki wa Chelsea nikamuambia 'NINAAMINI' Nenda kapige.
Mata aliileta kona ndani ya box, kilichofuata baada ya hapo ni historia. Chelsea wanatwaa taji la kwanza na la meisho la UEFA.
Didier Drogba ana miaka 43 leo. Happy birthday legend.