el nino
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 4,712
- 5,064
Toka mwanzoni mwa wiki hii Diamond Platnumz na crew yake wamekuwa waki-tease vitu kwa mafumbo kuashiria kuna kitu kikubwa kinakuja.
Diamond-Platnumz Kupitia Instagram Diamond ameshare fomu inayoonesha kuwa ameituma video ya collabo yake na Mr. Flavour iitwayo Nana kwenye kituo cha Runinga cha kimataifa BET International.
Katika fomu hiyo inaonesha kuwa video hiyo iliyoongozwa na Godfather inatarajiwa kutoa May 29, 2015. diamond bet Lakini pamoja na kutease fomu hiyo bado uongozi wake unasema kuwa Ijumaa hii ndio wataweka wazi ni wimbo gani anaotaka kuachia, lakini ni collabo ya kimataifa.
Vitu vyote tutasema kwa wananchi wetu Ijumaa, mashabiki wa Diamond mashabiki wa WCB wasubirie mpaka Ijumaa tutaanza rasmi kusema kama ni wimbo ambao tuna release Diamond featuring Flavour au Featuring P-Square au msanii wa Marekani. Alisema Babu Tale kupitia Sammisago.com
Chanzo: Bongo5