Ila wasanii wa Tanzania waongo sana, wakifa ndio ukweli unajulikana wengine watakufa na madeni au hata nyumba hawana
Yaani hawa wasanii hawaaminiki kabisa, kanumba watu walisemaga ndo msanii tajir kuliko wote, kafa kumbe hata nyumba hana, lile v8 alinunua kwa mkopo alitoa mil40 deni lingine kafa nalo, aya kuambiana mikwala ya english na kujifanya gentleman kumbe ni yahaya hana hata chumba alichopanga achilia nyumba, yani marehemu alikuwa popote kambi, kifo chenyew kimemkutia guest, yani wasanii wetu hawa mmh
diamond asije kurusha ngumi tu akiona baba zake wa kambo viserengeti boys wanavyosukuma hilo ndinga....si unajua bongo vijana wanavyopenda kuteleza na ganda la ndizi!
wanatafuta umaarufu kupitia vitu vya uongo hawajui kuwa itawagharimu bure hiyo
kweli hapo diamond umefanya vizuri ila ningekushauri ungemfungulia kwanza biashara ambayo angeweza kuifanya hata ukiondoka duniani asitie aibu kama wamama wengine wa watoto mashuhuri walivyo
maana hilo gari kwanza utampa presha bure mamayako, pili nani atakuwa akimuendesha
cha muhimu na cha kufanya mdogo wangu diamond wewe mfungulie biashara ili aifanye ndo itakayomuokoa yeye na sio starehe ya gari ingawaje nalo ni muhimu kwake
Biashara anayo, si nilisikia walichapisha T-shirt za wasafi classic uko ulaya, sasa sijui iliishia wapi, H.O.D alikuja akaipamba hiyo biashara yao, sijui iliishia wapi. Yani ndomo ujanja wote wa kukutana na akina davido kaona ku print tshirt na kuuza ndo ujanja? Akifa mama yake ndo atategemea hiyo biashara? Mmh apa ndo naona umuhimu wa ELIMU
angempata meneja wa music yake wa kumshauri vizuri angefika mbali maana anafanya vitu visivyoeleweka kabisa
Mi hata kabla sijamuona najua ni muarabu toleo la mwishonii ambapo wakienda uarabuni wanaonekana ni weusii tu
Hapa ni wivu wa watanzania uliokithiri, huu ni ugonjwa sugu wa watanzania usokua na dawa wala hospitali. Kutwa tuko negative na maendeleo ya wengine, kila mtu amesema aliloweza kusema kwa uwezo na upeo wake lakini kila ukiangalia ni wivu tu unawasakama. Diamond na mama yake hawakwenda shule ndio maana hafikirii nini afanye, nime quote mliyoandika. Nyie ambao vidato vimepanda hamkupaswa pia kuongea haya mnayoyaongea. Watu wasiosoma ndio wanaweza kuongea haya.
Kujenga au kuangalia kesho haihusiani na elimu wala darasa la mtu, bali akili na wito wa kufanya kile kitu. Sio Marehemu Kanumba au Diamond ambao wana pesa Tanzania na hawakufanya hayo mnayotaka, wako viongozi walioshika nyathifa mbali mbali kubwa tu na uwezo ulikuwepo lakini akili ya nitafanya kesho iliwatawala, walipoondoka madarakani walirudi kwenye vibanda vya wazazi wao vijijini bila chochote. Hawakua na nyumba wala magari ya kifahari waliyokua wanatembelea hapa mjini, hao ni wazee kabisa lakini hawakuangalia kesho.
Diamond na Marehemu Kanumba (RIP) bado hata 30 hawajafika, they still have time kama wana uhai na uzima.
Nitafurahi kama nyie ambao mmesoma sana mtatuorodheshea hapa rasilimali zetu tuzisome japo kwa uchache ili tujue na nyie wasomi mmefanya ya maana na mmeona kesho mkiwa bado vijana.
Acheni hizo, mpeni sifa Diamond pale anapostahili.
♥Diamond ndio tajiri wa kwanza tanzania kununua magari mapya yaliyosajiriwa zamani
~BX .....V8
~AY........Fun cargo
~CM........Harrier Lexus