Kazwala mkuu
JF-Expert Member
- Jul 2, 2016
- 1,034
- 2,250
Mfano kama wakati huu ni wasanii wengi wana ngoma kali na video kali lakini hawatajwi kama hawa mabwana, mfano wa wasanii wenye ngoma tamu kwa sasa ni Barnaba boy (lover boy) Chegge (Waache waoane) Dully (Inde) Ben Poul (Moyo mashine) Jux (Wivu) na wengine wengi.....lakini bado wanaonekana kuachwa mbali mno.Mtu wa tatu bado hajajitokeza
Naona hawa farasi wawili wanakimbizana wenyewe tu hao wengine naona wanajifurahisha wenyewe tu
Naam hawa wapo vizuri sana, huyu Dimpoz kuna wakati alikuwa anamkaribia sana Diamond ila sijui kwa sasa amekosea wapi!Ben pol na dimpoz
Naam kijana anakuja vema ila kwa sasa swali lipo pale pale.....nani ni mtu wa tatu?nadhani tukimpa muda Rayvannyatakuwa ndo 3.
Kweli kabisa vanessa anastahili kua namba tatu nevy kenzo inabidi waamke na wawe serious na mziki waoyaani umeongea kitu cha msingi sana, hao wengine hata wapige ngoma kali vipi watu wanawaanhalia hao tu namba 1 na 2
Kwangu Mimi namba 3 ni Vanessa au Navy Kenzo ( kimtazamo Wa kimataifa)
Kwa sisi watu wa Hip hop tunaamini mtu wa kwanza ni Fid Q.....ila katika hawa wawili wanaovuma ni kwa sababu ya nguvu kubwa ya watu wazito na wenye pesa walio nyuma yao na team pia.
Samahani mkuu naomba kukuuliza,hivi hao madogo Baraka na Abdukiba unaosema "vijana wa " kiba una maanisha nini sijakuelewa .............???Salaam
Katika wasanii wa kizazi kipya wenye gumzo kubwa kwa sasa ni Diamond na Ali Kiba, wasanii hawa wana timu kubwa za mashabiki kiasi kwamba kila upande huamini kuwa msanii wao ndiyo zaidi hivyo ligi hiyo haijawahi kuhitimishwa popote pale.
Naam mambo yamepamba moto kweli kweli na mziki wetu unapasua anga zaidi kila kukicha kupitia ushindani wao.
View attachment 407967Mziki wa sasa umekuwa unafika mbali na kusikilizwa na wengi duniani, lakini pia vijana wetu wengi wamejiajiri kupitia mzikiView attachment 407968Lakini kila unapouliza nani msanii namba moja, kama hutajibiwa Diamond basi utajibiwa Ali kiba, tuwachukue wote kwa pamoja na tuendelee mbele.....nani mtu wa tatu? Ni yupi anaefuata mara baada ya hawa?
Je, ni vijana wa Diamond, Rayvan na Harmonize?
Je, ni vijana wa Kiba, Baraka de prince na Abdul Kiba?
Ni Barnaba boy
Rich mavoko
Duly Sykes
Ben Poul
Jux
Ommy Dimpoz
Belle 9
Rama dee
Chegge
Au nani?
Je, kwanza wao (Diamond na Kiba) wanastahili kuwa mbele ya wasanii hawa wengine?
Yupi mtu wa tatu?
Karibuni wataalam wa tasnia hii.
Kwa fanbase naunga mkonyo hojacommando Jide.
Dimpoz ni kweli alikuwa na potential ya kuwa 'Top Player' kwa kipindi kile, ila tokea alipotoa Wanjera Graph yake ikaanza kushuka. Ben Pol ni msanii mkali ila hana potential ya kuwa Top Player kwenye muzikiBen pol na dimpoz