Ofisi za serikali zimeendelea kumuandama diamond platnumz
Taarifa iliyoanza kutoka Feb 22 na
kusambaa kwa kasi kwenye mitandao
ya kijamii ni pamoja na hii ya Diamond
Platnumz kuitwa Makao Makuu ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kwa ajili ya mahojiano mafupi.
Kupitia post yake aliyoipost instagram
Diamond Platnumz ameandika
>>’Mapema leo nilipo ripoti makao
makuu ya TRA baada ya kuitwa ili
kuelezea ni namna gani nayapata
mapato yangu na namna gani nalipa
kodi ya serikali’.
Hii itakua ni mara ya pili kwa Diamond
Platnumz kuitwa na mamlaka
hiyo,mara ya kwanza ilikua mwaka
mmoja uliopita ambapo Mamlaka hiyo
ya Mapato ilimkadiria kodi ambayo
Diamond alitakiwa kulipa na kwa bahati
nzuri Diamond Platnumz aliilipa hiyo
pesa.
View attachment 473630