Dialo anunua na kukodi kadi za CHADEMA

Dialo anunua na kukodi kadi za CHADEMA

Mwamson

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
267
Reaction score
92
Jana ndio siku yangu niliyokuwa naingoja kwa hamu ili kuhakikisha yasemwayo kwamba viongozi wangu wa CCM hawjengi chama ila wanajijengea jina ndani ya chama kwa ajili ya kuendelea kuchaguliwa na kumdanganya mwenyekiti wa taifa kuwa wanachapa kazi ya chama.

Uchunguzi huu niliufanya juzi ndani ya kata ya buswelu baada ya kupata taarifa kwamba mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza atakuwa na mkutano ndani ya kata hiyo iliyopo ndani ya manispaa ya ilemela mkoani mwanza.Kwa kuwa mimi ni mwanachama wa chama hicho na tawi langu liko kata ya jirani na kata hiyo nikaona hii ndiyo fursa ya pekee kujiridhisha na tetesi za kukifirimba chama kunakofanywa na viongozi wa ngazi za juu tuliowachagua sisi wenyewe, siku ya alhamisi jioni nitembelea mtaa maarufu ujulikanao kama buswelu center na vitongoji vyake kama bulola,kona,busenga na vijiwe vya pale zembwela.Kwa kuwa nilikuwa na langu moyoni nilikuwa makini saana kuangalia kila kinachoendelea kwa kila mtu na katika mikusanyiko ilioonekana si ya kwaida.

Kilichoniwia ugumu kwenye utafiti wangu ilikuwa ni usiri wa wale niliokuwa nawafuatilia nyendo zao juu ya kile nilichodokezwa kwamba kinafanyika,bahati ya mtende ambayo ilinifanya niishiwe nguvu badala ya kufurahia matpkeo ya uyafiti wangu,kwanza nilipokuta vijana wa mitaani wakigombana kwa kukubali kupokea pesa ndogo kukodisha kadi kwa wajumbe waliokuwa wanawashawishi kutoa kadi za chadema kwenye mkutano wa siku inayofuata yaani ijumaa ya jana,kundi lingine ni lile la vijana wa chadema waliokuwa wanafurahia kupewa pesa lakini wakipanga kutoonekana siku ya mkutano.

Kiwango cha pesa kilikuwa ni elfu tano na kumi,kadi zikitumika badae zinarudishwa kwa wajumbe wanaopitia na kukabidhi kwa wenyewe.hii yote ni kuonyesha kuwa viongozi wa mwanza wanafanya kazi na watu wanawskubali...kwa maelezo na ukitaka kujiridhisha wewe kama mwanajamii na kiongozi muadilifu wa ccm fanya utafiti.

JK Habari ndio hiyo.
 
Diallo anatapatapa sana...anaamini 'EL' akichukua nchi ataradi kunako neema.
 
Wenzao Chadema tunachoma kadi za magamba zikirudishwa tu ! Sasa hawa niaibu tupu mara nyingine utakuta jadi ni mpya na hazina majina halafu wanajitapa wanachadema wamerudi Magambani
 
mjinga sana wewe ... .....unaeibishia taaarifa hii
 
CCM kwishaaa,ndembe ndembe,nyanga nyanga.
 
Ccm sera wameishiwa,wamebaki kuhadaa wananchi tu! Ccm kifo cha mende,ndembendembe!
 
Asante kwa taarifa, je unaweza kuweka ushahidi wa majina (ya watuhumiwa na/au vijana waliotoa kadi zao) au picha ndugu?
Ningefurahi sana kuvipata hivyo ktk uchambuzi wangu.
 
Asante kwa taarifa, je unaweza kuweka ushahidi wa majina (ya watuhumiwa na/au vijana waliotoa kadi zao) au picha ndugu?
Ningefurahi sana kuvipata hivyo ktk uchambuzi wangu.

hata asipoweka ushahidi wowote,hii ipo wazi kuanzia kuiba masanduku ya kura,kuhonga viongozi wa upinzani wahame chama,kununua kadi haya yote ni sera ya ccm hamna cha kushangaa hapa ndugu
 
hata asipoweka ushahidi wowote,hii ipo wazi kuanzia kuiba masanduku ya kura,kuhonga viongozi wa upinzani wahame chama,kununua kadi haya yote ni sera ya ccm hamna cha kushangaa hapa ndugu

Ni kweli mkuu...i like your argument.
 
...alafu mtu kama huyo anateuliwa kuwa waziri wa maliasili,nini kitabaki...?kweli ccm janga...
 
hana tofauti na nape , yeye ameamua kubeba wachina ili kuwadanganya wananchi , POOR DIALLO ! Kuanzia leo naifuta rasmi star tv kwenye king'amuzi changu .
 
Back
Top Bottom