Diallo: Magufuli una mipango mizuri lakini huna watu

K M S

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
524
424
Nausikiliza mjadala hapa star tv wapo Mh. Dialo, Masalakulangwa. Ni mjadala kuhusu viwanda na kilimo na mheshimiwa Diallo ameonyesha wasiwasi kwa mheshimiwa Magufuli kufaulu mpango wake wa Tanzania ya viwanda.

Amesema pamoja na nia yake njema huenda asifaulu kwani hana watu wa kutimiza ndoto yake ya Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Mwijage upo??

Kama kuna watu muhimu ambao wanaitakia mema nchi hii ni pamoja na Dk. Tonny Diallo. Amemchana live Charles Mwijage kuwa "nchi haiwezi kufikia uchumi wa viwanda bila kwanza kuangalia ni wapi tunapata raw material. Na amesema ni ujinga kufikiria viwanda vya High Technology mfano kuunda pikipiki. Viwanda kama hivi haviwezi kumkomboa mkulima ambaye ni 80% ya watu nchini. Kwamba kama unataka kuinua maisha ya masikini ni lazima viwanda viangalie wakulima maana Mauritius ilijaribu kufanya uchumi wa viwanda kwa kuimplimenti HTI ikashindwa na kurudi kwa wakulima. Amesisitiza rais ajiangalie je anao watu wanaoelewa nia yake njema. Amewataka vijana kuwapinga watu mfano wa Mwijage kuwa hawajui ku-apply Ilani katika sera. Lkn pia amesema nchi haiwezi kufikia uchumi wa viwanda kwa kupuuza sekta binafsi. Diallo ametema madini sana.
 
Ndio maana kila mara anaomba aombewe.
Hata watangulizi wake, walikuwa na nia njema.
Ila somehow na somewhere kuna Tatizo.

Nausikiliza mjadala hapa star tv wapo Mh. Dialo, Masalakulangwa. Ni mjadala kuhusu viwanda na kilimo na mheshimiwa Diallo ameonyesha wasiwasi kwa mheshimiwa Magufuli kufaulu mpango wake wa Tanzania ya viwanda.

Amesema pamoja na nia yake njema huenda asifaulu kwani hana watu wa kutimiza ndoto yake ya Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Mwijage upo??
 
Mbona karibu idara zote,na vitengo vyote vimejazwa makada:iwe ma d.e.d,r.a.as,das,rc,dc na usalama wa taifa!
Watu gani hao anaowasema Diallo!
Kaazi kwelkwel kama Magu anamsikilza anamawazo mzr lkn
 
Kama kuna watu muhimu ambao wanaitakia mema nchi hii ni pamoja na Dk. Tonny Diallo. Amemchana live Charles Mwijage kuwa "nchi haiwezi kufikia uchumi wa viwanda bila kwanza kuangalia ni wapi tunapata raw material. Na amesema ni ujinga kufikiria viwanda vya High Technology mfano kuunda pikipiki. Viwanda kama hivi haviwezi kumkomboa mkulima ambaye ni 80% ya watu nchini. Kwamba kama unataka kuinua maisha ya masikini ni lazima viwanda viangalie wakulima maana Mauritius ilijaribu kufanya uchumi wa viwanda kwa kuimplimenti HTI ikashindwa na kurudi kwa wakulima. Amesisitiza rais ajiangalie je anao watu wanaoelewa nia yake njema. Amewataka vijana kuwapinga watu mfano wa Mwijage kuwa hawajui ku-apply Ilani katika sera. Lkn pia amesema nchi haiwezi kufikia uchumi wa viwanda kwa kupuuza sekta binafsi. Diallo ametema madini sana.
 
Nausikiliza mjadala hapa star tv wapo Mh. Dialo, Masalakulangwa. Ni mjadala kuhusu viwanda na kilimo na mheshimiwa Diallo ameonyesha wasiwasi kwa mheshimiwa Magufuli kufaulu mpango wake wa Tanzania ya viwanda.

Amesema pamoja na nia yake njema huenda asifaulu kwani hana watu wa kutimiza ndoto yake ya Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Mwijage upo??
anaitafuta nafasi ya Mwijage huyu...siyo bure!
 
Sote tunajua hakuna Uchumi wa viwanda utatokeaa hapa Tanzania. JPM anajua hilo, Samia anajua hilo, Majaliwa anajua hilo, Mwijage anajua hilo nk. Hata Diallo anajua hilo.
Tanzania ya Viwanda ni slogan tu ya kuunga unga ili kuwapata watanzania wajinga.
 
Siamini kama hana watu, sema watu waliopo ni masalia ya mifumo ya kibinafsi iliyopita.
Sasa Kubadilika ghafla ni kitu ambacho hakipo. Awape nafasi ya kukua taratibu.
Viwanda vinawezekana 100%.
Siamini katika Viwanda kutoka China,Uturuki,US au Ulaya bali viwanda kutoka ndani kwa watanzania wenyewe.
Sasa huwa sielewi Mwijage amefocus wapi maana hivyo vya nje ni too automatic na vipo vilikuwepo na vitaendelea kuwepo hata bila kauli mbiu kama wakiwekewa mazingira mazuri, ila uwekezaji wa kweli uwe ni kwa jinsi gani wananchi masikini, wa kipato cha kati na matajiri wataingia kwenye viwanda halisi katika kipnegele chochote kile zaidi ya kutegemea wananchi kufaidika kwa kuajiliwa kwenye viwanda.
 
Kwa kuongea maccm wote wanaweza, tatizo ni utekelezaji, ndiyo maana tunahitaji mabadiliko
mabadiliko yapi.
Kosa kubwa lililokosewa uchaguzi uliopita hakukuwa na maana yenye mantiki ya mabadiliko yaliyoongozwa na lws.
mjipange uchaguzi ujao mje na definition halisi ya mabadiliko na mseme nani aliyebadilika atakayesimamia mabadiliko hayo ambaye atakuwa na uhalali wa kusimama nyuma ya maiki.
 
Duu mkisema sana ataelewa tatizo sio raisi tatizo inatakiwa nchi iainishe vipao mbele vya nchi na hii itasaidia kufika tunako enda ila tukibaki na vipao mbele vya dharura tusahau tanzania kuendelea
 
  • Thanks
Reactions: Nio
Sisi tulisha sema Tanzania ya viwanda ni ndoto
Matamko mengi kuliko matendo
Muda mwingi kufukuzana na wapinzani, wamesema nini tuwashitaki
One man show
Unafiki, mtu anaona jambo lkn anajifanya haoni
Uteuzi unaozingatia ukada badala ya uwezo
Mipango mikubwa isiyo tekelezeka
 
Yeye mwenyewe viwanda vyake vyote vilishakufa miaka ya 90 kashindwa kuvifufua leo ndio mtoa ushauri,kweli ukistajabu ya musa
 
Duu mkisema sana ataelewa tatizo sio raisi tatizo inatakiwa nchi iainishe vipao mbele vya nchi na hii itasaidia kufika tunako enda ila tukibaki na vipao mbele vya dharura tusahau tanzania kuendelea
Kwani wewe bado hujaisoma dira ya taifa ya maendeleo ya 2025? Tuna vipaumbele sisi mbona!kama vile, elimu, nishati, maji, ukusanyaji wa rasilimali fedha(mapato), kilimo na uchukuzi.
 
Katu sidhani kama atashindwa kwa kukosa raslimali watu bali management style yake! Workforce iliyojaa woga (full time panic mode); haina nafasi ya kutumia taaluma kwa weledi unaostahiki!
 
Huwa napata shida ninapoona sera ya viwanda ni ya mtu na si taifa… mtu amejiandaa lakini taifa limejiandaa/limeandaliwa kuwa la viwanda?? Na katiba yetu ni kipindi cha miaka 5 au 10 je akiondoka huyo mtu sera hiyo itaendelea?
Lakini hivi viwanda vinavyoongelewa ni vipi kwa sababu hata watendaji nawasikia kila mtu na tafsiri yake!
 
Back
Top Bottom