Diallo asomeshwa namba: Akaunti za Sahara Media zafungwa na TRA kutokana na kodi ya Tsh. Bilioni 4

Status
Not open for further replies.
Naona Dialo anastruggle mno na hii kampuni yake,aliwekeza kwenye kampeni lakini ni kama haikumlipa,bora auze hiyo media afanye biashara zingine
 
Nakumbuka wakati Rais Magufuli anafunga kampeni zake mkoa wa Mwanza alimsifu jamaa kwa kufa coverage ya mikutano yake na mgombea mwenza kuwa mubashara na akaahidi KUTOMUANGUSHA. Wengi tulidhani angepewa kitengo nyeti sana serikalini kutokana na ahadi ya Rais ila tofauti na matarajio naona wameamua kumsomesha namba kwa kukwepa kodi.

Afadhali yake Diallo amekiri kudaiwa na anafanya mazungumzo ya kulipa deni. Ila Kaka Aikael sasa!
 
A. Dialo bil4 mbowe bil1 katolewa vitu na ofisi kufungwa. ilihali ashasema anamiliki 75% kesi iko mahakamani anaweza kushinda au kutoshinda
Dialo anaongea kwa kujiamini kabsaa apo ndo utaona tofauti kati ya mfanyabiashara wa ccm na mfanyabiashara wa upinzani.
 
Vipi haikutolewa Notice akapewa deadline?? Huyu si umesikia amefungiwa Account...
Kufungiwa account au kufunga office ndio utaratibu ninaojua,sio kwenda kusomba vitu kwa nguvu hadi kusababisha uharibifu namna ile!Lile suala ni siasa imeingizwa ndani!
 
Nakumbuka wakati Rais Magufuli anafunga kampeni zake mkoa wa Mwanza alimsifu jamaa kwa kufa coverage ya mikutano yake na mgombea mwenza kuwa mubashara na akaahidi KUTOMUANGUSHA. Wengi tulidhani angepewa kitengo nyeti sana serikalini kutokana na ahadi ya Rais ila tofauti na matarajio naona wameamua kumsomesha namba kwa kukwepa kodi.
Huu ndio ukomavu kisiasa,kodi lazima kila mtu alipe na bora amekiri kudaiwa na kufungiwa akaunti na kaonyesha utii,hamna jinsi ambavyo raisi anaweza kwenda TRA na kufuta madeni hiyo itakuwa kashfa na ningemshusha thamani kwa hilo.Kuna namna tu Diallo atasaidiwa kama ambavyo wazalendo wengine walivyopewa fursa. Nampongeza kwa kutokutoa sababu za kisiasa kama ambavyo tumesikia wengine wakitaka huruma.
 
naona maigizo tu ili ionekane wamebalance stori ya Mbowe kurushiwa vitu nje .....kwamba hata ccm wanadaiwa....mtukufu hawezi mwangusha msukuma mwenzie
 
Kufungiwa account au kufunga office ndio utaratibu ninaojua,sio kwenda kusomba vitu kwa nguvu hadi kusababisha uharibifu namna ile!Lile suala ni siasa imeingizwa ndani!
TRA utaratibu wao ndio huo... Ila Mbowe yeye anadaiwa na NHC. Wao pia wana utaratibu wao.. Kwani Mbowe ni mpangaji pekee wa kwanza kutolewa vitu nje na NHC??
 
Bil 4- mazungumzo yanafanyika
Bil 1-anafurumushwa na vitu nje ya ofisi

Diallo kakiri kuwa anadaiwa ndiyo maana mdai atamsikiliza namna ya kulipa. Kaka Aikael yeye hakubali deni ndio sababu kafurumushwa kwa kuleta usanii wake wa kizamani.
 
Alitoa Air time ndefu kumtukana Lowasa na kukaribisha watu kumkashifu Lowasa, badala muda huo angeutumia hata kupokea matangazo ya biashara kwa kufanya punguzo la bei hata kwa asilimia hamsini tu ingempa hela ya kupunguza deni, haya kina mwakyembe wao wamefaidika na uwaziri yeye AIBU safi sana Mungu analipa haraka kweli kweli.
Acha roho mbaya wewe.
 
Diallo kakiri kuwa anadaiwa ndiyo maana mdai atamsikiliza namna ya kulipa. Kaka Aikael yeye hakubali deni ndio sababu kafurumushwa kwa kuleta usanii wake wa kizamani.
Kesi si iko mahakamani?Kwann isisubiriwe hukumu?
 
TRA utaratibu wao ndio huo... Ila Mbowe yeye anadaiwa na NHC. Wao pia wana utaratibu wao.. Kwani Mbowe ni mpangaji pekee wa kwanza kutolewa vitu nje na NHC??
Najua mbowe anakesi na NHC na iko mahakamani,kwann wao wajichukulie uamuzi huo kabla ya mahakama kutoa hukumu?Je akishinda!
 
naona maigizo tu ili ionekane wamebalance stori ya Mbowe kurushiwa vitu nje .....kwamba hata ccm wanadaiwa....mtukufu hawezi mwangusha msukuma mwenzie
izo salakasi zao tushazielewa kitambo wasijisumbuwe kabisa hakuna wakumdanganya
 
Huyu sasa ndiye hasa fisadi wa kodi za wananchi maana anadaiwa na TRA tofauti kabisa na sakata la Mbowe na NHC ambayo ni mambo yao binafsi ya mikataba ya kibiashara!!

Kwa nini wamekaa mezani na kuzungumza kwa kutoa excuse za kipuuzi za kutolipa kodi yetu??? Ni yeye tu aliyehama kutoka analojia kwenda digitali? Mbona wenzake hawadaiwi? Au wanafanyia biashara zao ktk sayari nyingine yenye TRA tofauti na hii??

Kwa haki kabisa na kwa mtazamo wangu TRA hapa ndipo walipopaswa kwenda kung'oa milango, kutoa meza, makabati, kompyuta na kung'oa mitambo yao yote na kwenda kuifungia TRA WAREHOUSE hadi alipe deni la kodi yetu kwa maendeleo ya Taifa!!

Hii haikubaliki, unless iwe siyo kweli......ni tetesi tu!!
 
Hivi ni vitu viwili tofauti, Bil 1 ni kodi ya pango anayodaiwa na mwenye nyumba, na hii Bil 4 ni koti ya mapato
Kesi iko mahakamani,inakuaje unajichukulia maamuzi hayo huku hujui hukumu ya mahakama?
I bet kama Mbowe angekuwa anadaiwa na TRA angesombwa kuwekwa mahabusu kisha kufikishwa mahakamani
 
Sasa kilicho baki kila mtu awe ni mnoko kwa kumtaja mwenzake ambaye anadaiwa, kilicho bakia apo. Maana kama wameanza na Mh. Mbowe inabidi tutegeemee na wengineo bila kuoneana huruma
 
kale kawimbo kanakolea sasa " tumeipenda wenyewe........ acha waisome namba eeeee.... (harafu kuna base pale inaitikia) WAISOME NAMBA"...... Kwi kwi kwiiii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom