Dhima ya kiingereza na nadharia yake

Dhima ya kiingereza na nadharia yake

Regnatus Cletus

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2018
Posts
1,114
Reaction score
959
Moderators, naomba Uzi wangu usimame peke yake.

Ninasikitishwa sana na baadhi ya nadharia potofu zinazozushwa na watu kwa makusudi ama kwa kutoelewa juu ya matumizi ya lugha ya Kiingereza mashuleni na umuhimu wake.

Nadhani tungeanza kwa kuvunja vunja kipande kimoja baada ya kingine;

JE, KIINGEREZA NI KUELIMIKA???

Hapana, ni ukweli kwamba Kiingereza sio kipimo cha moja kwa moja cha kuelimika kwasababu maarifa yanaweza kufundishika katika lugha yoyote.

Lakini pia ni ukweli kwamba MAARIFA tuyapatayo nchini Tanzania toka kidato cha kwanza mpaka elimu ya juu yanatolewa kwa lugha ya kiingereza.

Hivyo, mtanzania akiniambia ameelimika kwasababu anafahamu kiingereza siwezi kustaajabu kabisa. (kama ameenda vidato).

Utawezaje basi kuelimika kama haukifahamu kiingereza??? Hayo maarifa uliyapata wapi?? na ulifaulu namna gani??

Nchini Tanzania, Mtu anayesema ameelimika na hafahamu kiingereza anaweza asieleweke kabisa.

Kwasababu tutajiuliza ulisoma namna gani?? Maana ni Kiingereza ndicho kinachotumika kufundishia, ama sivyo!!!!?

Mtanzania Kusema kwamba ameelimika na hakifahamu Kiingereza, NI UONGO!!

JE, WACHINA NI WASOMI WASIOJUA KIINGEREZA??

Ni ukweli kwamba, wachina hufundishia kichina katika ngazi zote za elimu.

Hivyo mchina akisema yeye ni msomi na hajui Kiingereza anaeleweka vizuri.

Maarifa yake ameyapata katika kichina , na kwasababu hiyo ni msomi katika lugha ya kichina, na hajui kiingereza kwasababu hakujifunza. HIYO INAELEWEKA KABISA.

Kwa sasa kumepatikana kichaka cha kujificha kwa wale ambao ung'eng'e umewakataa na kuwasaliti vinywani mwao, na kichaka hicho ni CHINA na RUSSIA!!

Nadhani hatuna haja ya kujificha huko, kwasababu hata hao wachina wanajifunza kiingereza kama lugha kwasababu wanaelewa kuwa Kiingereza ndio lugha ya dunia!!

Na zaidi ya yote, sisi bado ni nchi ya dunia ya tatu ambayo tunahitaji miingiliano na wazungu katika kila nyanja.

Kwanini tunapenda sana kujificha CHINA?? kwanini tusitizame mataifa yanayotumia Kiingereza ambayo ndio mengi zaidi?? Najiuliza sana kwanini iwe china. JIBU NI KUWA, HICHO NI KICHAKA CHA MAGOI GOI WA KIINGEREZA.

Lugha ya kiingereza ndio lugha ya maarifa ambayo yamehifadhiwa katika maandishi, internet, na kila mahali.

Najaribu kufikiri nisingekuwa nafahamu kiingereza, haya maarifa yaliyorundikwa google si ningekuwa nayapita mbali???

Tizama videos YouTube, TV series, Vitabu vya taaluma na fasihi, Taarifa za habari za kimataifa, magazeti nk. TUNAKIHITAJI KIINGEREZA.

FEDHEHA AIPATAYO GOIGOI WA LUGHA YA KIINGEREZA;

Kwasababu Tanzania sio kisiwa, tumejikuta tunafanya miingiliano mingi na nchi zingine ndani ya Afrika na nje ya afrika katika BIASHARA, ELIMU, AJIRA, MAKAZI, USAFIRI, NA MAMBO MENGINE YA KIJAMII.

Kuna mtanzania mmoja alipata nafasi ya kuhutubia kongamano fulani nchini Kenya, aliishia kujiuma uma tu na kuongea lugha za mashetani huku akitiririsha machozi ya aibu.

Wote mnakumbuka Ndugu yetu mmoja wa magogoni alienda UGANDA, alipoulizwa maswali na muandishi akabaki anababaika na kugugumia kama trekta mpaka ikabidi RAIS MUSEVEN AOKOE JAHAZI!!! NI FEDHEHA KUBWA.

WATANZANIA, TUNAPASWA KUJIFUNZA KIINGEREZA BADALA YA KUJIPOTOSHA.
 
Nimewahi tu siti, ngoja waje wenye busara zao na kujua hio lugha watupe muongozo.
 
Watanzania tunasoma kitu katika lugha Tatu

Ya kwanza ukisha soma kwa kiingereza unapeleka katika lugha ya kiswahili halafu ndo unamalizia katika lugha ya kienyeji

Kwa hiyo huo mchakato huwa ni mrefu ndo maana kama mtu anataka kuongea kiingereza akili yake inatafsiri lugha tatu kwa pamoja ndo maana kiingereza kinakuwa shida

Si kweli kuwa kutojua kiingereza hujaelemika no shida ni communication skills
 
Unawezaje kutafsiri Kiingereza kama haukijui???
 
Naomb kuuliza, Wengne wanaongea kiingereza wakilewa, huyu nae tumtafsiri kama aliyelimika?
 
Kwa sasa Dunia inazo lugha Kuu za Kimataifa Kama 7 hivi (Mfano:Kiingereza,Kifaransa,Kihispania,Kiarabu,Kichina na Kirusi).Maarifa Mengi yapo katika Lugha ya Kiingereza.Kwa hiyo wale tulioanza shule enzi za Ujamaa tukapigwa propaganda tusifanye makosa Kwa watoto wetu.Inawapasa wanetu wajue Kiingereza na Kiswahili kwa Ufasaha.Aidha Kwa wale waliofikia level ya postgraduate wanashauriwa kuongeza lugha nyingine ili kuongeza wigo.Baada ya Kumaliza Chuo Kikuu nilipata Kazi Kwenye Transnational Corporation na Medium of communication ilikuwa Kiingereza.Ripoti zote Kiingereza. Ilibidi nilipiwe Tuition fees British Council siyo kwa ajili hasa ya Lugha ya Kuandika,lakini Kufundishwa Jinsi ya Kutamka ili Wenzetu waweze kunielewa!Hapo ndiyo nilielewa mapungufu ya Elimu yetu.Kama mhitimu wa Shahada ya Pharmacy yale maformula yalikuwa kchwani na kuyaandika ilikuwa rahisi--Changamoto ilikuwa kuzungumza kibiashara/Kikazi.Nikaja baadaye Kufanya Kazi na Kampuni nyingine ambayo lugha kuu zilikuwa English na French.Waliokuwa wanaufahamu wa hizi lugha 2 walikuwa na advantage kwenye kupanda madaraja.Tusidanganganyane,Weredi wa lugha za Kimataifa ni mhimu sana,kwenye kazi na kwenye biashara.
 
Mbona kuna mtu ana PhD na hawezi kuzungumza hata sentesi kumi za kiingereza kwa ufasaha,ina maana hajaelimika?😂
 
miongoni mwa mambo yanayonikera zaidi nchi hii ni mifano ya China na Urusi
 
Ukitaka kua wa kitaifa jua kiswahili pekee...

Ukitaka kua wa kimataifa jua lugha zaidi ya moja kingereza kikiwa kimoja wapo...

Hao wanaopinga kingereza mbona wakitaka kuangalia movie wanaona kheri waangalie zilizo kwenye lugha ya kingereza... hata kama hawakielewi...

Cc: mahondaw
 
Kwa sasa Dunia inazo lugha Kuu za Kimataifa Kama 7 hivi (Mfano:Kiingereza,Kifaransa,Kihispania,Kiarabu,Kichina na Kirusi).Maarifa Mengi yapo katika Lugha ya Kiingereza.Kwa hiyo wale tulioanza shule enzi za Ujamaa tukapigwa propaganda tusifanye makosa Kwa watoto wetu.Inawapasa wanetu wajue Kiingereza na Kiswahili kwa Ufasaha.Aidha Kwa wale waliofikia level ya postgraduate wanashauriwa kuongeza lugha nyingine ili kuongeza wigo.Baada ya Kumaliza Chuo Kikuu nilipata Kazi Kwenye Transnational Corporation na Medium of communication ilikuwa Kiingereza.Ripoti zote Kiingereza. Ilibidi nilipiwe Tuition fees British Council siyo kwa ajili hasa ya Lugha ya Kuandika,lakini Kufundishwa Jinsi ya Kutamka ili Wenzetu waweze kunielewa!Hapo ndiyo nilielewa mapungufu ya Elimu yetu.Kama mhitimu wa Shahada ya Pharmacy yale maformula yalikuwa kchwani na kuyaandika ilikuwa rahisi--Changamoto ilikuwa kuzungumza kibiashara/Kikazi.Nikaja baadaye Kufanya Kazi na Kampuni nyingine ambayo lugha kuu zilikuwa English na French.Waliokuwa wanaufahamu wa hizi lugha 2 walikuwa na advantage kwenye kupanda madaraja.Tusidanganganyane,Weredi wa lugha za Kimataifa ni mhimu sana,kwenye kazi na kwenye biashara.
Enzi za ujamaa ni miaka gani hiyo mlikuwa hamjifunzi Kiingereza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu unayoiongelea ni ipi ? Article yako ni inclusive kama vile elimu na maarifa yote yamesitirika katika Kiingereza.
Ni vema pia ukazingatia kuwa Elimu inayowabana watu kujifunza/kuelewa Kiingereza ni Elimu rasmi aka.Formal Education. Lakini kumbuka kuwa Formal education is just a tip of the Iceberg.
 
Hakuna lugha bora kuliko nyingine hatuwezi kuamini kuwa kwa sababu masomo ya sekondari yanatolewa kwa kiingereza basi tunaelimika kwa kupitia kiingereza kwa sababu hata kama tukisoma kwa lugha hiyo ulimwengu wetu ni wa Kiswahili na unatusaidia kufasiri.
Tunaelewa kwa Kiswahili licha ya kusoma kwa Kiingereza na kwa Mtazamo wangu naona tukitumia lugha ya Ulimwengu wetu(Kiswahili)itakuwa vizuri zaidi.
Hizi kauli kwamba Kiswahili hakiwezi ni za Kibwanyenye na zenye nia ya kuutukuza ukoloni mamboleo kwa kutumia Lugha.
Wewe mwenyewe inawezekana kabisa ulikuwa ukisoma Kiingereza lakini ulielewa kwa Kiswahili na kwa maana hiyo Matumizi ya lugha mbili katika kujifunza na kuelewa ni sababu moja wapo ya vijqna wengi kutofanya vizuri masomo yao.
Hata huo mfano uliotoa wa China unapaswa kujua kuwa siyo Wachina wote wanajifunza Kichina.
Kutumia Kiswahili hakumaanishi matumizi ya Kiingereza yatakufa la hasha!..kwa sababu naona wakereketwa wa Kiingereza mmeanza kupiga mayowe.
Kauli za kuhadaa Watubkuwa Kiswahili hakiwezi na hakina msamiati wa kutosha nazo ni kama hewa chafu lakini haiwezi kuchafua Kiswahili kwa ukweli kwama Lugha zote hukua na huongeza msamiati wake kwa nija mbalimbali.
KISWAHILI KWANZA
 
Elimu unayoiongelea ni ipi ? Article yako ni inclusive kama vile elimu na maarifa yote yamesitirika katika Kiingereza.
Ni vema pia ukazingatia kuwa Elimu inayowabana watu kujifunza/kuelewa Kiingereza ni Elimu rasmi aka.Formal Education. Lakini kumbuka kuwa Formal education is just a tip of the Iceberg.
Mkuu ungekuwa Masumbwe leo ningekupa ofa ya unachopendelea kwa hii hoja.
 
Back
Top Bottom