Shakidinkili
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 458
- 174
Kabla hujajiuliza Mkapa alipokea nchi ikiwa hali gani jiulize kwanza Mwinyi aliipokea chini ikiwa kwenye hali gani. Kwa kukusaidia rejea hutuba ya kwanza ya Mwinyi bungeni mwaka 1985 utafahamu aliipokea nchi ikiwa na akiba ya fedha za kigeni kiasi gani. Jiulize pia au uliza watu hali mahitaji muhimu ya binaadamu ilikuwaje.Tafakari upya. Mh. Ben Mkapa, Raisi mstaafu alipokea kijiti nchi ikiwa katika hali gani? Ruksa ilitufikisha wapi?
Uko sawa sawa kabisa!Jamani mbona mnazunguka. Tuseme wazi tatizo si waziri wala watendaji. Bali ni mfumo. Mkulu akitoka yataisha.
Mbona Ali Hassan Mwinyi alijiuzuru kisha akawa Rais wa nchi na akaongoza vizuri?
ushaambiwa nyerere hakuacha hata senti tano hazina,actually kufilisika nchi ndo sababu ya yeye kubwaga manyanga baada ya kina mkono kuitafuna nchi na kisha kutorokea nje ya nchi.Aliongoza vizuri kwa kuporomosha uchumi wa nchi? au kuongeza madeni na kuifanya ombaomba? wafanyakazi watamkumbuka kwa kuwakosesha mishahara coz ndicho kipindi pekee mfanyakazi alikuwa akikopwa mshahara hadi hata kwa miezi 2 na zaidi! nakuona kama shabiki mandazi vile!
unajua maana ya mfumo?Jamani mbona mnazunguka. Tuseme wazi tatizo si waziri wala watendaji. Bali ni mfumo. Mkulu akitoka yataisha.
Kabla hujajiuliza Mkapa alipokea nchi ikiwa hali gani jiulize kwanza Mwinyi aliipokea chini ikiwa kwenye hali gani. Kwa kukusaidia rejea hutuba ya kwanza ya Mwinyi bungeni mwaka 1985 utafahamu aliipokea nchi ikiwa na akiba ya fedha za kigeni kiasi gani. Jiulize pia au uliza watu hali mahitaji muhimu ya binaadamu ilikuwaje.
Kuna maoni tofauti tofauti yametolewa na wananchi mbali mbali wakiwepo Wasomi kuhusu sakata la Mawaziri wanne kuachia ngazi za Uwaziri kufuatia kashfa ya OPARESHENI TOKOMEZA UJANGILI. Mh. Balozi Kagasheki alitamka mwenyewe bungeni na wengine watatu waliwajibishwa na Mamlaka iliyowateua. Maoni ninayotaka kuyazungumzia hapa ni hii kauli ya ''MAWAZIRI HAWAKUTENDA MAKOSA ISIPOKUWA WAMEWAJIBIKA KISIASA.'' wanaweza kuomba/kugombea au kuteuliwa tena kwenye nafasi zingine ikiwepo ukuu wa nchi (Uraisi) Kauli hii kwangu mimi nitasema ni dhihaka au utani kwenye masuala nyeti. Yeyote yule atayejisikia kuchangia mawazo yake, ninamsihi asiingize ushabiki wa kisiasa, kiitikadi, u-ccm wala u-chadema bali azingatie utaifa kama Mtanzania.
1. Kwangu mimi haiingii akilini kama mkuu wa kitivo katika chuo kikuu akishindwa kuongoza kitivo ati anaweza kufikiriwa kupewa nafasi ya kuwa Makamu mkuu wa chuo.
2. Haiingii akilini mwangu kama Waziri aliyeshindwa kuongoza wizara moja, kuwawajibisha na kuwathibiti watendaji katika wizara hiyo ati afikiriwe kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
Watanzania tuondokane na mawazo mgando, watanzania tunataka maendeleo ya kweli ya nchi yetu, tunataka watoto wote wa kitanzania wafaidi matunda ya raslimali za nchi yao. Watoto wa Kitanzania ikiwezekana wasomeshwe na serikali yao mpaka upeo wa akili zao kwa kutumia raslimali za nchi yao. Haya yote hayawezi kupatikana kama tutaendelea kuwategemea watu waliopewa nafasi lakini wakashindwa kuzitumikia nafasi hizo ipasavyo, badala yake tunaleta lugha rahisi ati wamewajibika kisiasa....
...
...
Aliacha akiba ya 3,000 Us dollars tu.ushaambiwa nyerere hakuacha hata senti tano hazina,actually kufilisika nchi ndo sababu ya yeye kubwaga manyanga baada ya kina mkono kuitafuna nchi na kisha kutorokea nje ya nchi.