Dhihaka kwenye uongozi wa nchi mpaka lini?

Shakidinkili

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
458
250
Kuna maoni tofauti tofauti yametolewa na wananchi mbali mbali wakiwepo Wasomi kuhusu sakata la Mawaziri wanne kuachia ngazi za Uwaziri kufuatia kashfa ya OPARESHENI TOKOMEZA UJANGILI. Mh. Balozi Kagasheki alitamka mwenyewe bungeni na wengine watatu waliwajibishwa na Mamlaka iliyowateua. Maoni ninayotaka kuyazungumzia hapa ni hii kauli ya ''MAWAZIRI HAWAKUTENDA MAKOSA ISIPOKUWA WAMEWAJIBIKA KISIASA.'' wanaweza kuomba/kugombea au kuteuliwa tena kwenye nafasi zingine ikiwepo ukuu wa nchi (Uraisi) Kauli hii kwangu mimi nitasema ni dhihaka au utani kwenye masuala nyeti. Yeyote yule atayejisikia kuchangia mawazo yake, ninamsihi asiingize ushabiki wa kisiasa, kiitikadi, u-ccm wala u-chadema bali azingatie utaifa kama Mtanzania.
1. Kwangu mimi haiingii akilini kama mkuu wa kitivo katika chuo kikuu akishindwa kuongoza kitivo ati anaweza kufikiriwa kupewa nafasi ya kuwa Makamu mkuu wa chuo.
2. Haiingii akilini mwangu kama Waziri aliyeshindwa kuongoza wizara moja, kuwawajibisha na kuwathibiti watendaji katika wizara hiyo ati afikiriwe kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
Watanzania tuondokane na mawazo mgando, watanzania tunataka maendeleo ya kweli ya nchi yetu, tunataka watoto wote wa kitanzania wafaidi matunda ya raslimali za nchi yao. Watoto wa Kitanzania ikiwezekana wasomeshwe na serikali yao mpaka upeo wa akili zao kwa kutumia raslimali za nchi yao. Haya yote hayawezi kupatikana kama tutaendelea kuwategemea watu waliopewa nafasi lakini wakashindwa kuzitumikia nafasi hizo ipasavyo, badala yake tunaleta lugha rahisi ati wamewajibika kisiasa. Watanzania tuachane na majibu mepesi, watu wakisema ukweli wanaambiwa, Hayo ni maneno tu hata kwenye khanga yamo. au huo ni upepo tu unavuma na utapita. Nini wajibu wa Waziri katika Wizara anayoiongoza? Watanzania tukae tukijua kuwa ''OLD HABITS DIE HARD'' mimi ninaamini hiyo ndio hulka yao hivyo sioni umuhimu wa wao kufikiriwa kupewa nafasi kubwa zaidi. Kama tatizo ni ubovu wa sera, je wao walitoa mchango gani ili kuboresha sera za Wizara walizokuwa wanaziongoza. Sio kama ninawachukia wahusika, bali tujiulize hivi hakuna Watanzania wengine wenye uwezo wa kuongoza mpaka tuendelee kuwafikiria wao tu? Watanzania walio wengi wana maisha magumu kupindukia, watanzania wanahitaji viongozi makini, viongozi wawajibikaji, viongozi wazalendo wanaoguswa na umaskini wa watanzania ili wawaletee maendeleo ya kweli, maendeleo ya watu sio vitu. Labda ukimya wa watanzania unawaponza. Viongozi mkae mkijua kuwa '' MSIONE KONDOO ANAONGOZA NJIA YA KWENDA MACHINJIONI MKADHANI ANAFURAHIA KWENDA KUCHINJWA.'' Haya ni mawazo yangu na wewe unakaribishwa kuchangia pasipo kejeli wala matusi. WASALAAM.
 
mavumbi

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
462
250
Mkulu: dhihaka kwenye uongozi? Au uelewa wa dhana ya uongozi na dhima yake ndio tatizo? Na ukituambia tusiingize maoni yenye kuashiria kuwepo kwa udhaifu wa vyama vya siasa katika suala la uongozi huoni kuwa unatuminya kifikra?

Hoja yangu: Hawa viongozi tunawapataje katika mfumo (process) wa Kitanzania? Sidhani kama kuna tatizo kudai kwamba mfumo wenyewe umegubikwa na udhaifu mkubwa wa mifumo ndani ya vyama vyetu vya siasa. Samahani!
 
bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,812
2,000
Sababu zilizosababisha Ali Hassan Mwinyi kujiuzulu kama waziri wa mambo ya ndani hapo awali na baadaye kumfanya awe Rais wa SMZ, na makamu wa pili wa rais, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mwenyekiti wa CCM taifa, ndizo zitasababisha mtu yeyote aliyejiuzuri kurudi tena kuongoza
 
Shakidinkili

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
458
250
Bila samahani. Ushabiki wa kisiasa au vyama vya siasa mara nyingi unapotosha mambo mengi. Ilimradi mtu amependa chongo basi huita KENGEZA. Tunataka facts ambazo zinajenga, zisizolinda chama au ushabiki wako wa kisiasa. Tanzania ni nchi yetu wote tunatakiwa tuijenge kwa pamoja.
 
Shakidinkili

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
458
250
Tafakari upya. Mh. Ben Mkapa, Raisi mstaafu alipokea kijiti nchi ikiwa katika hali gani? Ruksa ilitufikisha wapi?
 
RUKAKA

Senior Member
Apr 17, 2011
100
195
Jamani mbona mnazunguka. Tuseme wazi tatizo si waziri wala watendaji. Bali ni mfumo. Mkulu akitoka yataisha.
 
jidodo

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
1,176
0
Tafakari upya. Mh. Ben Mkapa, Raisi mstaafu alipokea kijiti nchi ikiwa katika hali gani? Ruksa ilitufikisha wapi?
Kabla hujajiuliza Mkapa alipokea nchi ikiwa hali gani jiulize kwanza Mwinyi aliipokea chini ikiwa kwenye hali gani. Kwa kukusaidia rejea hutuba ya kwanza ya Mwinyi bungeni mwaka 1985 utafahamu aliipokea nchi ikiwa na akiba ya fedha za kigeni kiasi gani. Jiulize pia au uliza watu hali mahitaji muhimu ya binaadamu ilikuwaje.
 
m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,367
2,000
Mbona Ali Hassan Mwinyi alijiuzuru kisha akawa Rais wa nchi na akaongoza vizuri?

Aliongoza vizuri kwa kuporomosha uchumi wa nchi? au kuongeza madeni na kuifanya ombaomba? wafanyakazi watamkumbuka kwa kuwakosesha mishahara coz ndicho kipindi pekee mfanyakazi alikuwa akikopwa mshahara hadi hata kwa miezi 2 na zaidi! nakuona kama shabiki mandazi vile!
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
38,186

ushaambiwa nyerere hakuacha hata senti tano hazina,actually kufilisika nchi ndo sababu ya yeye kubwaga manyanga baada ya kina mkono kuitafuna nchi na kisha kutorokea nje ya nchi.
 
bdo

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,812
2,000
Ungefunguka tu, mafumbo ya nini tena - au taarabu, toa data na ulinganifu, yeye kaja kimya na wewe unampima tena, sisi mbumbu tutafanyeje sasa?
Kabla hujajiuliza Mkapa alipokea nchi ikiwa hali gani jiulize kwanza Mwinyi aliipokea chini ikiwa kwenye hali gani. Kwa kukusaidia rejea hutuba ya kwanza ya Mwinyi bungeni mwaka 1985 utafahamu aliipokea nchi ikiwa na akiba ya fedha za kigeni kiasi gani. Jiulize pia au uliza watu hali mahitaji muhimu ya binaadamu ilikuwaje.
 
Shakidinkili

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
458
250
Ndugu Rukaka unaposema tatizo ni MFUMO. Hii kitu mfumo ni kitu gani ambacho hakiwezi kutenguliwa kama vitabu vitakatifu vya Mungu? Tukiendelea kuwakumbatia watu wa aina hii, dhahiri mfumo utabaki ule ule, kamwe hautarekebishwa na matatizo ya watanzania yatabaki pale pale. Huyo Mkulu akitoka atamrithisha swahiba wake. Tuambie nini kifanyike.
 
Shakidinkili

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
458
250
Kama ulizaliwa kwenye nyumba ya udongo hutakiwi kuridhika kuwa hata wewe uwaache watoto wako kwenye nyumba ya makuti. We need to go forward, that is all. Watanzania tunataka viongozi watakao tupeleka mbele.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,489
2,000
Kuna maoni tofauti tofauti yametolewa na wananchi mbali mbali wakiwepo Wasomi kuhusu sakata la Mawaziri wanne kuachia ngazi za Uwaziri kufuatia kashfa ya OPARESHENI TOKOMEZA UJANGILI. Mh. Balozi Kagasheki alitamka mwenyewe bungeni na wengine watatu waliwajibishwa na Mamlaka iliyowateua. Maoni ninayotaka kuyazungumzia hapa ni hii kauli ya ''MAWAZIRI HAWAKUTENDA MAKOSA ISIPOKUWA WAMEWAJIBIKA KISIASA.'' wanaweza kuomba/kugombea au kuteuliwa tena kwenye nafasi zingine ikiwepo ukuu wa nchi (Uraisi) Kauli hii kwangu mimi nitasema ni dhihaka au utani kwenye masuala nyeti. Yeyote yule atayejisikia kuchangia mawazo yake, ninamsihi asiingize ushabiki wa kisiasa, kiitikadi, u-ccm wala u-chadema bali azingatie utaifa kama Mtanzania.

1. Kwangu mimi haiingii akilini kama mkuu wa kitivo katika chuo kikuu akishindwa kuongoza kitivo ati anaweza kufikiriwa kupewa nafasi ya kuwa Makamu mkuu wa chuo.

2. Haiingii akilini mwangu kama Waziri aliyeshindwa kuongoza wizara moja, kuwawajibisha na kuwathibiti watendaji katika wizara hiyo ati afikiriwe kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
Watanzania tuondokane na mawazo mgando, watanzania tunataka maendeleo ya kweli ya nchi yetu, tunataka watoto wote wa kitanzania wafaidi matunda ya raslimali za nchi yao. Watoto wa Kitanzania ikiwezekana wasomeshwe na serikali yao mpaka upeo wa akili zao kwa kutumia raslimali za nchi yao. Haya yote hayawezi kupatikana kama tutaendelea kuwategemea watu waliopewa nafasi lakini wakashindwa kuzitumikia nafasi hizo ipasavyo, badala yake tunaleta lugha rahisi ati wamewajibika kisiasa....

...

...

Tuache Siasa kando, Kuna vitu unachanganya Mkuu,

Uhusiano wa Mkuu wa Kitivo na Utendajhi wa Kitivo anachokisimamia uko wa moja kwa moja zaidi kuliko wa Waziri na Wizara husika.

Mkuu wa kitivo anaweza akawa na Taaluma ya Kitivo Husika, labda Kitivo cha Sayansi kikasimamiwa na Mwanasayansi, vivyo hivyo kwa Vitivo vya Sheria, Biashara, Teknohama e.t.c Lakini Mawaziri hua sio watendaji wa Moja kwa Moja kwenye Wizara, na ndio maana wanaweza kuhamishiwa Wizara nyingine bila tabu kwani Hawaja-specialize.

Makatibu Wakuu na Watendaji wengine Wizarani ndio hasa Wanakua Wame-specialize kwenye majukumu hayo. Na ndio haohao waborongaji wakuu.

Labda nikuulize, tuseme katika Maaskari waliofanya unyama kwa wananchi kwenye hiyo OTU, wapo wanaotoka Wizara ya Bw. Kagasheki. Je kuna kesi ilishafikishwa kwa Waziri akaizima kimyakimya bila Mtuhumiwa kuchukuliwa hatua??

Umeshawahi kusikia Sakata la Augustine Lyatonga Mrema alivyomshtaki aliekua Waziri wa Mambo ya Ndani Ndg. Ally Hassan Mwinyi kwa Nyerere juu ya Mauaji yaliyokua yakiendelea Shinyanga na kupelekea Mwinyi Kujiuzulu?? Lakini Mwishowe si Mwinyi akaja kua Raisi wa JMT?? Tena kwa kuelewa Umuhimu wa Aliemchongeaga, akamchagua kua Waziri?
 
Shakidinkili

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
458
250
NINAOMBA UNIAMBIE MAJUKUMU YA WAZIRI KATIKA WIZARA ANAYOIONGOZA. KWA TAARIFA, HATA MAKATIBU WAKUU WANAHAMISHWA KWENDA WIZARA ZINGINE. Kwa mtizamo wa haraka jinsi michango ya wana jf inavyojitokeza, Waziri hana kazi yoyote kwenye wizara.
 
duchi

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,766
0
ushaambiwa nyerere hakuacha hata senti tano hazina,actually kufilisika nchi ndo sababu ya yeye kubwaga manyanga baada ya kina mkono kuitafuna nchi na kisha kutorokea nje ya nchi.
Aliacha akiba ya 3,000 Us dollars tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom