Shakidinkili
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 458
- 174
Kuna maoni tofauti tofauti yametolewa na wananchi mbali mbali wakiwepo Wasomi kuhusu sakata la Mawaziri wanne kuachia ngazi za Uwaziri kufuatia kashfa ya OPARESHENI TOKOMEZA UJANGILI. Mh. Balozi Kagasheki alitamka mwenyewe bungeni na wengine watatu waliwajibishwa na Mamlaka iliyowateua. Maoni ninayotaka kuyazungumzia hapa ni hii kauli ya ''MAWAZIRI HAWAKUTENDA MAKOSA ISIPOKUWA WAMEWAJIBIKA KISIASA.'' wanaweza kuomba/kugombea au kuteuliwa tena kwenye nafasi zingine ikiwepo ukuu wa nchi (Uraisi) Kauli hii kwangu mimi nitasema ni dhihaka au utani kwenye masuala nyeti. Yeyote yule atayejisikia kuchangia mawazo yake, ninamsihi asiingize ushabiki wa kisiasa, kiitikadi, u-ccm wala u-chadema bali azingatie utaifa kama Mtanzania.
1. Kwangu mimi haiingii akilini kama mkuu wa kitivo katika chuo kikuu akishindwa kuongoza kitivo ati anaweza kufikiriwa kupewa nafasi ya kuwa Makamu mkuu wa chuo.
2. Haiingii akilini mwangu kama Waziri aliyeshindwa kuongoza wizara moja, kuwawajibisha na kuwathibiti watendaji katika wizara hiyo ati afikiriwe kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
Watanzania tuondokane na mawazo mgando, watanzania tunataka maendeleo ya kweli ya nchi yetu, tunataka watoto wote wa kitanzania wafaidi matunda ya raslimali za nchi yao. Watoto wa Kitanzania ikiwezekana wasomeshwe na serikali yao mpaka upeo wa akili zao kwa kutumia raslimali za nchi yao. Haya yote hayawezi kupatikana kama tutaendelea kuwategemea watu waliopewa nafasi lakini wakashindwa kuzitumikia nafasi hizo ipasavyo, badala yake tunaleta lugha rahisi ati wamewajibika kisiasa. Watanzania tuachane na majibu mepesi, watu wakisema ukweli wanaambiwa, Hayo ni maneno tu hata kwenye khanga yamo. au huo ni upepo tu unavuma na utapita. Nini wajibu wa Waziri katika Wizara anayoiongoza? Watanzania tukae tukijua kuwa ''OLD HABITS DIE HARD'' mimi ninaamini hiyo ndio hulka yao hivyo sioni umuhimu wa wao kufikiriwa kupewa nafasi kubwa zaidi. Kama tatizo ni ubovu wa sera, je wao walitoa mchango gani ili kuboresha sera za Wizara walizokuwa wanaziongoza. Sio kama ninawachukia wahusika, bali tujiulize hivi hakuna Watanzania wengine wenye uwezo wa kuongoza mpaka tuendelee kuwafikiria wao tu? Watanzania walio wengi wana maisha magumu kupindukia, watanzania wanahitaji viongozi makini, viongozi wawajibikaji, viongozi wazalendo wanaoguswa na umaskini wa watanzania ili wawaletee maendeleo ya kweli, maendeleo ya watu sio vitu. Labda ukimya wa watanzania unawaponza. Viongozi mkae mkijua kuwa '' MSIONE KONDOO ANAONGOZA NJIA YA KWENDA MACHINJIONI MKADHANI ANAFURAHIA KWENDA KUCHINJWA.'' Haya ni mawazo yangu na wewe unakaribishwa kuchangia pasipo kejeli wala matusi. WASALAAM.