Wakuu, habari..
Ni changamoto gani na dharau ulizokumbana nazo kwa masekretari pindi unapeleka barua ya kazi au unashida na HR au manaja?
Mimi ilikuwa mwaka jana katika kiwanda cha kuchakara samaki hapa Dar.
Ilikua majira ya asubui mida ya saa tatu. Kwanza kimbembe cha mlinzi ilikua balaa, yaani mlinzi anataka kukagua vyeti vyangu. Nilimkatalia kwani tayari bahasha ilikuwa imefungwa, ndipo akaniruhusu kwa mbinde baada ya mwenzie kumwambia aniruhusu tu.
Nikafika mapokezi, nilimkuta secretary, namsalimia mara mbili hakuitika, ndipo nikamkazia mpaka karibu na meza yake na kumsalimia.
Aliitika kwa huku akijifanya anachati kwenye simu yake.
Baada ya salam nilimwambia nimeleta barua ya kazi katika kiwanda chenu, akanijibu, HAMNA KAZI.
Nikamweleza naweza kuiacha barua yangu hapa kwamba ikitokea niweze kufahamishwa? Hakunijibu chochote zaidi ya kuondoka kuelekea nje.
Ilinibidi niondoke, hakika siku hiyo nilikosa furaha, sikuweza kula.
Nashukuru kwa sasa nimepata kazi, na yule dada nimemsamehee.
Alamsiki.