Dhana ya Tafsiri ya Uhuru wa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana ya Tafsiri ya Uhuru wa nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwakajilae, Dec 15, 2011.

 1. m

  mwakajilae Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa nchini nduguzanguni kuna mikorogo mingi sana juu ya tafsiri ya Uhuru wa nchi hii mwaka 1961,kama nchi ya Tanganyika Huru.
  Lakini tunajisahau kwamba tulichokipata mwaka 1961 hakikuwa Uhuru wa Taifa la Tanganyika bali ulikuwa ni uhuru wa nchi ya Tanganyika.
  Dhana ya Taifa na Nchi ni vitu viwili tofauti vinavyo tegemeana na kuathiriana.,Taifa ni juu ya watu na Nchi ni juu ya Aridhi na mipaka yake.
  Ndani ya miaka50 ya uhuru tumeendelea kujitambulisha kama Taifa huru ili hali ni nchi huru,kwani ukitaka kujua kwamba Taifa halipo huru ndani ya miaka 50 ya nchi,angalia mifumo yetu ya elimu kama inaashiria uhuru wa Taifa,angalia mifumo yetu ya Uzalishaji mali kama inauhusiano na uhuru wa watu wake[Taifa],hebu angalia mifumo ya miundombinu yetu ndani ya miaka 50 ya uhuru kama ina mahusiano wake na wananchi wake!!!
  Lakini kubwa zaidi ni uhuru wa wananchi juu ya nchi yao na Taifa laoVs Uhuru wa mabeberu au viongozi juu ya nchi ya Tanzania!!!
  Mwl Nyerere aliendelea kupigania uhuru wa Taifa mara baada ya kumaliza mchakato wa kwanza wa uhuru wa nchi,alijua hamuwezi kuwa huru kabisa kama hamjapata uhuru wa Taifa,uhuru wa wananchi kuzalisha mali,kuelimika na kudhibiti uchumi wao kwa kuuhodhi,elimu kwa mahitaji ya ndani.
  miaka 50 ya uhuru hamna viwanda,hamna wataalam wenu wa migodi yenu,wa uvuvi bahari n.k
  Matokeo yake tunajisifu kwa sera za uwezekezaji kwa kupotosha hata mantiki yake,tupo tayari kuondoa kodi kwa mwekezaji toka nje lakini siyo muwekezaji wa ndani,tunadai siyo taifa la kibaguzi wa rangi,kwa kudhani rangi ni uzungu,tunawanyenyekea watu weupe na kuwachukia weusi!!!!!!!!!
  baadala ya kuwawezesha wawekezaji wa ndani tunawawezesha wa nje ili wavune na kusafirisha kwao
  Nchi ipo huru lakini Taifa halipo huru daima.
   
Loading...