Dhana ya kujivua magamba na kubakia na vidonda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana ya kujivua magamba na kubakia na vidonda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by King junior, Apr 12, 2011.

 1. King junior

  King junior Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nionavyo mimi " Wananchi wamepunguza imani na CCM kutokana na udhalimu na ufisadi unaofanywa kila leo na chama tawala hadi serikalini.

  Kiukweli hamsomi alama za nyakati, na hambadiliki kutokana na wakati, mmekuwa mkiimba nyimbo zile zile tangu Uhuru ambazo wananchi wengi tumezichoka. Hata mnachokifanya sasa ni danganya toto, kwani kitendo cha 'KUVUA GAMBA' kwa ninavyojua ni kuacha mabaya na kutenda mema yaani kama kitu kinazaliwa upya.

  Kimsingi hamtambui kuwa kansa hukaa kwenye damu na si kwenye gamba kama mnavyofikiri, tatizo sio viongozi, bali ni system yenu mbaya. Mlipaswa kukaa pamoja kuondoa tofauti zenu, ndio muanze mchakato wa kulivua hilo gamba lenu. Hao mnaowatoa wana makundi, wanaoingia NEC wana makundi pia, hivyo mtarudi palepale.

  Mnapaswa kubadili nyimbo, mjisafishe wenyewe kwanza, muwe mstari wa mbele kupiga vita ufisadi ndani ya chama na serikalini na si kuongoza nchi kirafiki kama ilivyo sasa, la sivyo mtakuwa mnafagia uchafu, harafu mnarudisha uchafu" Ni hayo tu, 'MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU IBARIKI AFRIKA.'
   
 2. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Adui mwombee njaa. Hii inakuwa ni faida kwa wapinzani wa kweli.
   
 3. King junior

  King junior Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Saana, waache waneng'eneke, tuchukue nchi kiulainiiii 2015, hawana jipya hawa mabwana, wanafikiri bado tuna tongo tongo tangu enzi za Mwl. Wameula wa chuya.....!
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wapinzan mmeshaanza kuishiwa na cha kusema! Poleni sana!
  CCM juuuuu!!!
   
 5. King junior

  King junior Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwel wewe akili yako ni mbovu, hadi umri huo, hutambui maovu yanayofanywa na CCM....? Unatakiwa upelekwe milembe, si bure....!
   
 6. n

  ndaru Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm wanatakiwa kubadilisha hata damu kwa kuwa jinsi walivyo bado hawajabadilisha kitu.
   
 7. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi nyoka akijivua gamba anabadilika na kuwa chatu au nyoka mwingine yeyote?? CCM hata wajivue magamba mara kumi watabaki wale wale tu!!
   
 8. g

  gmantz New Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri ni hatua muafaka kwa hatua moja kwani hatua zaidi zinabidi kuzingatiwa kukamilisha safari ya kujisafisha na kurudisha matumaini kwa wanachama na chama kiujumla ,naongopa kusema ya kwamba kwa hatua hiyo isije ikawa ni ya saniiiiiiiii tuuuu maana viongozi wetu wamekuwa watu wa porojo zaidi kuliko fact and action
   
Loading...