TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Habari za leo ndugu zangu? Bila shaka mu wazima kabisa...leo naomba tuzungumzie kuhusu siku ya wanawake duniani. Nimekuwa nashangazwa kila mwaka ifikapo tarehe kama ya leo basi watu husheherekea siku hii kwa kuwapost mama zao au hata walezi wao, inawezekana ni kwa kujua au kutokujua kuwa wanachokifanya ni sahihi au si sahihi. Nimewahi kusema hapo awali tofautisha kati ya siku ya "wanawake" duniani na siku ya kina "mama" duniani.
Siku ya wanawake duniani ni siku iliyowekwa mahususi kwa ajili ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia, kuwepo kwa haki sawa kwa wote yaani kutokomeza mfumo dume ambao umetapakaa duniani. Sio siku ya kuonesha mapenzi kuwa unampenda sana mama yako la hasha bali ni siku ambayo unapaswa wewe kuitumia kupaza sauti kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na kuwapa uhuru kama tulivyo na uhuru sisi wanaume.
Ni matukio mangapi ya unyanyasaji ambayo tumekuwa tukiyasikia au hata kuyashuhudia mara kwa mara?
Ni wanawake wangapi ambao wanateswa na waume zao au baba zao kwa kubaguliwa kutopewa elimu kama wanaume. Imekuwepo dhana katika baadhi ya makabila kuwa mtoto wa kike hapaswi kupewa elimu kwakuwa ataolewa na kuachana na familia husika hivyo anayepaswa kupewa elimu ni mtoto wa kiume? Kuna kauli husemwa "ukimuelimisha mwanamke mmoja basi umeelimisha jamii nzima" hii ilipaswa siku ya leo kurasa zenu zijae habari za kukemea na kulaani vitendo viovu vinavyofanywa dhidi ya wanawake wote na sio siku ya kusheherekea mapenzi kwa mama zenu. Ilipaswa tujitafakari je kampeni zinazoendeshwa kumkomboa mwanamke kifikra zimefanikiwa kwa asilimia ngapi, rejea harakati anazozifanya Joyce Kiria kwa kipindi cha "Wanawake live", matukio mangapi maovu ambayo mwanamama huyu amefanikiwa kuyaibua na yakapatiwa ufumbuzi?
Juzi kati tulishuhudia mheshimiwa raisi kupitia kwa mkurugenzi wa habari wa ikulu alipomtembelea yule mama aliyeunguzwa na mume wake na kisha raisi akampatia msaada, yapo mambo mengi sana especially kwa sisi watumiaji wa mitandao ya kijamii tulipaswa kuyakemea na kupambana ili kuyatokomeza kabisa. Badala yake tupo busy kuwasifia mama zetu, je ndilo dhumuni haswa la siku hii ya wanawake duniani? Je siku ya kina mama duniani ina dhumuni gani kama tunashindwa kufahamu utofauti huu?
Yamkini ndani ya familia zetu kuna matukio maovu dhidi ya wanawake yanaendelea hivyo siku ya leo ilikuwa ni siku ya kuwatia moyo na kuwapa haki zao sawa kabisa.
Inanisikitisha kila ninapopitia status za watu humu nakutana na jumbe za kuwasifia mama zao lakini sio kukemea maovu ambayo yapo katika familia zao au jamii zao kwani ninaamini ukatili dhidi ya wanawake bado umeshamiri vya kutosha, tubadilishe hii dhana mbovu ya kuchanganya siku ya wanawake na siku ya kina mama. Kwa pamoja tutaweza kutokomeza unyanyasaji na ukatili uliopo katika jamii zetu.
Asanteni na niwatakie siku njema yenye baraka tele ndugu zangu wote ila msisahau "Mwanamke mmoja tu akipewa daftari anaweza kubadilisha jamii nzima".
Mtenga Gerald
08/03/2017