Rich Hash
Senior Member
- Mar 7, 2017
- 149
- 203
Inaonekana kuna mkakati wa makusudi wa kuzichafua taasisi za serikali kwa mbinu chafu. Kumbuka kuna baadhi ya vyama au wanasiasa wenye kutaka kufikia malengo yao kwa gharama yeyote ile, na hata kuwatoa watu kafara au kwa kutengeneza mazingira ya kuwatoa watu kafara kwa malengo yao ya kisiasa.
Nirejee mlolongo wa mambo
Na ukiangalia kwa makini-mikakati imeenda mpaka wanawafikia Usalama wa Taifa (TISS). Matumani yao ni kwamba wakishaivuruga idara hiyo basi na kwingine watafanikiwa. Kumbuka unapozungumzia usalama wa taifa unazungumzia nini.
Ila kwa maoni yangu nadhani serikali imeshakwisha litambua hili, na mkakati unaelekea kufilisika.
Panzi Mchanga
Nirejee mlolongo wa mambo
- Operation Ukuta- lengo ilikuwa kuifanya nchi isitawalike; viongozi wa dini hawakuwa pamoja nao
- Matukio yanayoendelea Bungeni na kuhusianisha TISS
- Maafa ya Kagera-tetemeko (tumesahau pia mtwara walipotea watu 84 na kilosa pia kulitokea majanga)
- Uvamizi wa Clouds TV na kuambatanishwa na Usalama wa Taifa
- Tukio la kutolewa bastola Nape na kuhusishwa na Usalama wa Taifa, Mategemeo yalikuwa wamkamate apate more publicity
- Nia ya baadhi ya wabunge kutaka kumwondoa waziri mkuu
- Kutangazwa kwamba kuna ugonjwa wa zika nchini
- Kusudio la kutaka kupandisha bei ya huduma zitolewazo na serikali (Umeme-kumbuka mwaka uliotangulia walishusha bei)
- Makusudi ya kuaminisha kuwa Tanzania kuna janga la njaa
- Matukio ya kutekwa wasaanii-ambapo hakuna hata maelezo kamilifu
- Matukio ya kuvamiwa mkutano wa CUF
- Matukio mengi kwa sasa kuhusishwa na usalama wa taifa.