Rationalizer
Member
- Jul 12, 2013
- 46
- 19
nilijua chadema inashindana na vyama vingine kama vile udp, nccr-mageuzi, tlp, ccm na ccj na vingine vingi tu hapa nchini kwa kujinasibu kwamba ndicho chama pekee cha ukombzi kwa watanzania lakini hatimaye nikagundua kwamba chadema inashindana na uwongo ambao umeshaonesha dalili kwamba chadema inawahadaa watanzania ikiwa ndio mkakati wake wa kupendwa ili waaminiwe na kukabidhiwa dola.
ilianza kwa kutotii amri za mamlaka ya nchi huku ikifanya fujo, kusababisha mauaji ikipaza sauti haraka milithili ya mwanamke aliyemkaba mumeo kooni lakini eti anapiga kelele kuomba msaada akidai ananiua, ameniumiza, niokoeni na maneno mengine chungu mzima lakini mwishowe watu wanapojitokeza wanagundua mwanaume ndio kakabwa. Ndivyo ilivyo kwa chadema kuhadaa watanzania ni ulimwengu mzima kwamba wananyanyaswa na polisi, wanatishiwa kuuwawa, wanaibiwa kura na kadhalika na baada ya kugundua kwamba watanzania wameshawastukia, sasa wanatumia uwongo bila kujua kwamba ndio kaburi lao.
gazeti la chadema katika moja ya makala zake za leo iliyoandikwa na aliyejiita mwandishi wetu wakati jana huyu huyu mwandishi wa chadema ambaye mwongo, mzandiki na mvivu wa kufikiria tena anaejua kuwagawa watanzania kikabila, kidini na hasa kisiasa aliyeandika kwa kuwaaminisha watanzania kwenye mtandao wa jamii forum kwamba mh. Ole medeye (mb) ambaye pia ni naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi amewaagiza malaigwanani wakawaambie kinamama na vijana eti wawapinge wachaga kutokana na fujo za lema ambaye ni mchaga na wasimchague mgombea yeyote ambaye si mmasai katika uchaguzi wa kesho jumapili kata nne za mkoa wa arusha lakini habati nzuri kwa kimasai kuna msemo usemao "meeppoo esipata ngujit" ikimaanisha kwamba majani hata yawe marefu namna gani lakini hayawezi kuficha ukweli.
nasikitika kwamba watu wengi wamechangia mtandaoni tena kwa kumuunga mkono mpuuzi aliyeendika uwongo mtupu lakini niwasihii watanzania tusiwe wepesei wa kuhukumu bila kuchunguza hasa kwa vyanzo mbali mbali uhalali wa kile tunachodhani ni muhimu kuchangia mawazo.
Mwandishi alitaka kuwaaminisha watanzania kwamba malaigwanani walidanganywa wahudhurie mkutano wa kimila lakini eti ajenda ikabadilishwa na kuwa mkutano wa siasa kiasi cha kulazimu malaigwananani wampinge mh. Ole medeye. Alitaka pia kuwaaminisha kwamba wamasai ni wabaguzi na hawawathamini watzania wengine.
kwa kifupi, mimi nilihudhuria mkutano ule na si technical kama mwandishi alivyodanganya kwani wazee wale si wanafunzi wa technical bali eneo linaitwa oreteti loongaik ambayo ni sehemu maalum kwaajili ya mikutano ya mila za kimasai tangu enzi za mababu na si kila mtu anaweza kuingia bali ni wazee maarufu na viongozi wa rika mbali mbali za kimasai ndio tu wanaingia pale tena si kama sokoni bali kwa ratiba maalum kama bungeni vile.
nathubuti kusema mwandishi huyu wa chadema ni mwongo kwani ule ni mkutano wa kimila ambao mh. Ole medeye alihudhuria kwa haki zote za kimila na si kama mbunge wala naibu waziri, bali ni laigwanani kama malaigwanani wengine hasa ukizingatia arusha huezi kuwa kiongozi wa kisiasa tena kwa ngazi ya ubunge bila kusimikwa cheo cha kimila ambayo ndio msingi wa hekima. Mwandishi ni mwongo kwasababu ole medeye hakuuliza swali wala kuchangia mada yoyote iwe ya kimila wala ya kisiasa hivyo basi ni dhahiri kwamba mwandishi wa makala ile ndio anawagawa watanzania kwa ubaguzi wa rangi, ukabila, ukanda, kidini na hasa kisiasa kwa makala yake ya uwongo bila kujua watanzania popote walipo hawapendi kutenganishwa kwa misingi hiyo.
wamasai wangekuwa wabaguzi kama mwandishi alivyosema,basi wasingewakaribisha watanzania wengine bila kujali ukabila na wakawauzia ardhi na bado wanawauzia, wamasai wasingeoana na makabila mengine tu mengi ya kitanzania, wamasai wasingekuabali kushirikiana na watanzania wengine katika shughuli zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa na wasinge wachagua viongozi wa kiasiasa mfano mh. Godbless lema na madiwani wote ambao si wamasai na waliondolewa na chadema hapa arusha. Mbona wamasai wamejaa kwenye dini na vyama vyote vya siasa hapa nchini?
mwandishi huyu ni tishio kwa usalama wa nchi, umoja na mshikamano wa watanzania hivyo anastahili kuwaomba radhi wamasai na watanzania kwa ujumla kwani akifanikiwa kuwagawa wamasai na wachaga, basi ataendeleo kuwagawa makabila mengine na nchi haitabaki sala. Kama chadema inamtumia mtu kama huyu ili kupata huruma ya kupigiwa kura, basi imenoa kwani uwongo ulioandikwa jana tarehe 12/07/2013 na leo ukaandikwa katika gazeti la mtanzania daima si tu itawafanya watanzania waione jamii forum na gazeti la tanzania daima kwamba ni vyanzo vya habari zisizofaniwa uchunguzi, bali pia itawafanya watanzania wasizisome habari mbali mbali katika vyanzo nilivyotaja.
Mwandishi huyu aogopwe si tu kama fujo za chadema, bali pia kama mauaji ya kimbari ya rwanda na burundi.
Mwisho, napenda kuwahakikishia watanzania kwamba huo ni uzushi na mwandishi apuuzwe kwani lengo lake ni kuwagawa watanzania kwa misingi ya ukabila, udini, ukanda ila namsihi awaache watanzania wamchague kiongozi yeyote wa kisiasa wanayemuona anawafaa ili kiongozi huyo asipotekeleza majukumu yake kama anavyoahidi katika kampeni zake basi waliomchagua wajilaumu wenyewe lakini isitokee kiongozi mwenye hekima na maadili kama mh. Ole medeye akapakaziwa uwongo kama huo.
Mungu wabariki watanzani, mungu ibariki tanzania, mungu ibariki africa !