passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,828
- 3,935
Wakuu habari za uzima?
Kama kichwa cha habari kinavyosema, binafsi naona suala la dhambi ni mtazamo na sio kitu universal standard. Dhambi ni uasi na uasi ni kwenda tofauti na sheria.Na kinyume cha uasi ni UTII.
Embu tuangalie mfano wa kabila la banyankole nchini [emoji1254] Uganda.
Banyankole wanakitu kinaitwa (potency test) kwa maana ya majaribio ya uwezo wa mwanaume kusimamisha uume.
Hili linafanyika vipi?
Nchini Uganda kuna kabila la banyankole, Mara nyingi ndoa huonekana kama mzigo usiofikirika haswa kwa mashangazi wa bibi harusi, kwenye kabila hili nchini Uganda shangazi wa bibi harusi anatakiwa kufanya majaribio na bwana harusi ili kupima uwezo wake kwa kufanya nae mapenzi.
Shangazi ndio huridhia, pia shangazi anapaswa kucheki bikira ya bibi harusi. Hii kwao ni jambo la heshima,kwenda kinyume na jambo hili ni dhambi kwao.
Dini zinatazama vipi kuhusu hili? Kwenye upande wa dini ndoa ni baina ya watu wawili (wakristo) na Mke zaidi ya mmoja(waislamu) kwa maana shangazi hatakiwi hapa kufanya mapenzi na bwana harusi na pia atakiwi kwenda kupima bikira ya bibi harusi.
Isipokuwa tu kuna baadhi ya dhambi ni standard universal kama usiue.
Nikienda umasaani kabla ya kumuamkia mzee masaai warriors wanatemea mate mikono Yao kabla ya kusalimiana na wazee hio ni heshima. Atakutafsiri vipi raisi au bosi wako uteme mate mkononi halafu umpe mkono? Ataona huu ni uasi na ni dharau.
Una mtazamo gani kuhusu hili?
Dhambi ni mtazamo wa watu wa jamii fulani ,hapo bado zunguka sana utashangaa mengi sana .
Kikubwa kila mtu ana lake ukienda India kule baadhi ya makabila na mila hawali ng'ombe kwao ni haramu kabisa ..
Kila mtu aishi chini ya mfumo wake anaoamini.
Umenena vyema sana.Ndugu, kila mfumo wa maisha huongozwa na utaratibu wake na sio mtazamo kama unavyotanabaisha. Ukishaita “Dhambi” moja kwa moja unaingia katika dini na maana ya Dhambi katika dini ni uasi wa Mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu.
Dhambi sio mtazamo kwasababu ili ujue hii ni dhambi na hii sio dhambi, lazima urejee kwenye vitabu vitakatifu kupata muongozo. Haijalishi kabila gani linafanya nini as long as Maandiko yameshasema ni dhambi, hiyo ni Dhambi katika mfumo wa maisha ya kidini
Lakini tukirudi kwenye mfumo wa maisha ya kawaida tuna “Morals” kuna “good morals” na kuna “bad morals” Hapa ndipo jamii zinaweza kutofautiana kulingana na taratibu za tamaduni zao. Mathalani, kuna makabila ndugu wanaweza kujamiiana lakini kuna makabila ndugu hawapaswi kujamiiana.
Hivyo, Dhambi sio mtazamo. Ni suala la kuyajua maandiko matakatifu ili kubaini lipi ni dhambi na lipi sio dhambi. Na kama mtu sio muumini wa dini basi hawezi kuzungumza lolote kuhusu dhambi. Lakini hilo halimfanyi akwepe hukumu ya dhambi.
Dhambi sio mtazamo. Mtazamo upo kwenye taratibu za kijamii ila Dhambi ni Dhambi katika mfumo wa kidini. Biblia ikisema usiue, Muumini yoyote wa Kikristo awapo popote pale hapaswi kuua. Huwezi ukawa mkristo kisha ukasema kwa mtazamo wangu kuua sio dhambi.
HAKUNA MTAZAMO BINAFSI KATIKA DHAMBI.
Tupe maoni yako mkuu😂Wahenga tuliyajua haya kitambo
Vitabu vitakatifu ni vitabu gani na utakatifu wake umehalalishwa vip?Ndugu, kila mfumo wa maisha huongozwa na utaratibu wake na sio mtazamo kama unavyotanabaisha. Ukishaita “Dhambi” moja kwa moja unaingia katika dini na maana ya Dhambi katika dini ni uasi wa Mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu.
Dhambi sio mtazamo kwasababu ili ujue hii ni dhambi na hii sio dhambi, lazima urejee kwenye vitabu vitakatifu kupata muongozo. Haijalishi kabila gani linafanya nini as long as Maandiko yameshasema ni dhambi, hiyo ni Dhambi katika mfumo wa maisha ya kidini
Lakini tukirudi kwenye mfumo wa maisha ya kawaida tuna “Morals” kuna “good morals” na kuna “bad morals” Hapa ndipo jamii zinaweza kutofautiana kulingana na taratibu za tamaduni zao. Mathalani, kuna makabila ndugu wanaweza kujamiiana lakini kuna makabila ndugu hawapaswi kujamiiana.
Hivyo, Dhambi sio mtazamo. Ni suala la kuyajua maandiko matakatifu ili kubaini lipi ni dhambi na lipi sio dhambi. Na kama mtu sio muumini wa dini basi hawezi kuzungumza lolote kuhusu dhambi. Lakini hilo halimfanyi akwepe hukumu ya dhambi.
Dhambi ni mtazamo Kuna vitu sehemu Moja sio kosa sehemu nyingine ni kosa.....mm mpaka nakufa huwezi niambia kulala na mdada ni dhambi kikubwa nisiwe nimemshurutisha, nimemlaghai kivyovyote au nimetumia advantage ya changamoto yake kumdinya!Tupe maoni yako mkuu😂
😂😂Wanadai bila kwenda kanisani kuvaa suti na shera hio ni dhambiDhambi ni mtazamo Kuna vitu sehemu Moja sio kosa sehemu nyingine ni kosa.....mm mpaka nakufa huwezi niambia kulala na mdada ni dhambi kikubwa nisiwe nimemshurutisha, nimemlaghai kivyovyote au nimetumia advantage ya changamoto yake kumdinya!
Daah! Hawa Jamaa Covi19 ikiingia huko itawamaliza.Nikienda umasaani kabla ya kumuamkia mzee masaai warriors wanatemea mate mikono Yao kabla ya kusalimiana na wazee hio ni heshima.
Upuuzi upuuzi TU....😂😂Wanadai bila kwenda kanisani kuvaa suti na shera hio ni dhambi