Dhambi moja huzaa dhambi nyingine

sizonjemadawa

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
1,053
1,304
Habari wakuu

Dhambi ni nini?

Dhambi ni tendo, hisia au wazo lolote linalopingana na sheria au matakwa ya Mungu

Kwa kifupi Dhambi ni aina yoyote ya kosa ambalo mwanadam analifanya iwe kwa kuvunja sheria ambayo imewekwa na Mungu au Imewekwa na mwanadamu au sheria ya nchi.

Dhambi huanza taratibu sana kwenye maisha ya mwanadamu wakati mwingine unaweza ukafikili, haitoleta madhara baadae na ukafilia haitokuja kujulikana baadae,

Kwa mfano kiongozi aliyegushi vyeti, wakati anafanya hivi alikuwa na focus atimize lengo lake la kufika elimu ya juu, lakini kumbuka anakazi kubwa ya kutunza siri hii ya kugushi vyeti ili watu wasijue, kwenye kutunza siri utafanya kitu chochote ili siri isifichuke unaweza hata kuua, ili kutunza siri yako hapa dhambi ya kudanya imezaa ya kuua kumbuka kuna dhambi ya uongo ndani yake

mfano rahisi kiongozi muongo ambaye, anasimama mbele za watu na kusema kuwa hataki vilaza kwenye serikali yake, akafukuza wanafunzi,akafukuza wafanyakazi, ikatokea katika watoto wake yupo kilaza na asifanye hivyo kama alivyofanya kwa wengine hapa utaona jinsi dhambi moja ilivyozaa nyingine

Au mtoto ambaye ameiba kipande cha kuku akiulizwa lazima atakataa tu, hapa kuna dhambi ya wizi iliyozaa dhambi ya uongo.
 
Back
Top Bottom