mwanademokrasia91
New Member
- Sep 29, 2013
- 3
- 2
KUFUNGIWA KWA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA NI HUJUMA ZA WAZANDIKI WA CHAMA NA SERIKALI
Kwanza napenda kumshukuru mungu muumba wa mbingu na ardhi mwenye kutoa ridhiki zote zile ndogondogo na kubwa. Namshukuru kwakunipa nguvu leo hii kuamka vizuri na nafuu ya kutosha baada ya kulala kitandani kwa siku tatu nikisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
KUFUNGWA KWA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA
Nimepata taarifa yakua serikali imeamua kuyafunga magazeti ya mwananchi na mtanzania.
Kwakweli baada ya kupata taarifa hiyo nilijisikia vibaya sana kwanza kama mpenzi wa kusoma magazeti hayo lakini pia kama kijana mwenye kujali na kupenda mambo yenye ukweli uzalendo na uhakika.
Baada ya kusikitishwa na taarifa hizo nilitamani kujua sababu za msingi zilizopelekea serikali kufikia maamuzi hayo. kwakweli kwa utafiti niliofanya nimepata kujua kua gazeti la"Mwananchi''moja ya sabubu ya kufungiwa kwake ni kutokana na kuchapisha taarifa kuhusu mishahara ya serikali suala ambalo serikali imedai kua ni jambo la siri na halikupaswa kuchapwa kwenye magazeti kwa maana hiyo ama kwa tafsiri rahisi,Si haki ya mwananchi kutambua mishahara ya watumishi wa umma. Je? hiyo ni sahii? Sasa hapo ndipo huwa ninajiuliza mara nyingi maswali ambayo kwa kawaida huwa nakosa majibu juu ya maamuzi yanayofanywa na hawa watawala wetu.
Watawala hawa ambao wamekua wakifanya maamuzi na kutamka mambo ambayo mara nyingi yamekua yakikinzana na ukweli lakini pia na mipango ambayo wao wenyewe waliianzisha. labda niwakumbushe hili ingawa najua mnakumbuka kua serikali ilitia saini mpango wa kuendesha shughuri za kiserikali kwa uwazi(OPEN GOVERNMENT INITIATIVES).
Kwa mujibu wa maneno ya Raisi wetu alikiri kukubali wazi kua uwazi ni jambo bora na ni vyema kuendesha shughuri za serikali kwa uwazi mkubwa lakini vilevile mpango huu umepongezwa sana na mataifa makubwa ikiwemo taifa la marekani ambalo linaongozwa na Rais Obama ambaye alimsifu Raisi Kikwete kutokana na kuwa na mpango huu wa uwazi katika kuendesha shughuri za serikali ambapo Raisi wetu amekua akiitangazia dunia kua anao ndani ya serikali yake,lakini kiuharisia nashindwa kuelewa kua ni uwazi gani huo ambao unazuia kutaja mishahara ya serikali wakati kimamtiki hawa watumishi wa serikali wanalipwa kupitia kodi ya mwananchi ambaye ni mimi na wewe tunaesoma magazeti ya Mwananchi na mtanzania, nchi yetu ni nchi ya kidemokrasia ambapo tunasema nchi yoyote ile yenye demokrasia wananchi ndio wenye mamlaka ambao pia hutoa uhalali wa mtu ama chama fulani kuunda serikali, sasa basi kwa tafsiri hiyo tunasema kua wananchi kwa umoja ndio mabosi na ndio mwenye kufanya maamuzi ndani ya nchi na serikali itawajibika kwa mwananchi na ndivyo hata kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ilivyoandikwa,sasa kwa serikali kuzuia mishahara ya watumishi wa umma kuchapishwa kwenye magazeti ni kukiuka taratibu za kidemokrasia lakini vilevile ni kukinzana na mpango wa OGP.
Hivi ni bosi gani ambaye astahili kujua mishahara ya watumishi wake?je hiyo ndio democrasia? Na pia Je?kunanini ndani ya mishahara hiyo? Kwa kawaida hata kama bila ya mpango huo wa OGP ni muhimu mwananchi kutambua ama kufahamu malipo kwa maana mishahara ya viongozi wote wa serikali kuanzia Raisi makamu wake mawaziri na watumishi wote hadi ngazi ya chini kabisa ya serikali yaani huku serikali za mitaa,hii ni nzuri katika kupima utendaji wa watumishi wa umma kama wanacholipwa kinafanaa na utendaji wao kwa maana mtu ulipwa kutokana na uzalishaji wake ama utendaji wake.
Kwa upande wa gazeti la MTANZANIA nimejaribu kufuatilia sababu ya kufungiwa kwake ukiachana na zile zingine ni kutokana na kuchapisha habari isemayo "MAPINDUZI NI LAZIMA"nashindwa kuelewa ni jinsi gani kauli hii imetafsiriwa na hawa watawala wetu hata kufikia mahala kulifunga gazeti hili nashindwa kuelewa maamuzi yao hawa watawala ambao siku zote ujiona wao ndio makini pekee na hakuna mwingine ambaye anaweza kuishika dola na kufanya mambo ya maana huu ndio udhaifu mkubwa wa fikra za chama na serikali, lakini tukija kwenye hali halisi tu tunapata picha nzuri inayoonyesha uoga walionao hawa watawala wetu juu yakuipoteza dola wanashindwa kuelewa kua dunia kwa sasa ipo kwenye mabadiliko gan?hili ndilo tatizo kwa watawala wetu tatizo linalowapelekea kufanya maamuzi kama haya ambayo nathubutu kuyaita maamuzi yakidikteta maamuzi yasiyofuata misingi yakidemokrasia.
Watawala wetu dhairi yakua ni waoga na ni uoga wa wazi kabisa tena uoga usio hata na haya kwa wananchi waliowapa idhini ya kuwa walipo sasa. kauli iliyo andikwa na gazeti la mtanzania kua "Mapinduzi ni lazima" inautofauti gani? na ile kauli ya Wazanzibari ambao wao wanakauli isemayo "mapinduzi daima"sasa kwa kauli hiyo ya wanzanzibari ambayo yenyewe kiuharisia inaonyesha kukomaa zaidi maana hata uhuru wao ulipatikana kupitia mapinduzi,mbona hawakuikemea kauli hiyo kama ni kauli ya kuashiria uvunjifu wa amani?lakini vilevile tukumbuke wakati ule wa Mwl Nyerere kuwa watu wenye kutetea maslahi ya umma waliitwa "Wanamapinduzi" ukienda mbali zaidi hutaweza kuoji je?chama chao kinapindua nini?
Hatua ya serikali kuyafunga magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA ni hatua ya kidikteta na kizandiki haipaswi kuachwa bila kukemewa na kama itaendelea basi tutajenga uoga kwa waandishi wetu na kuwafanya washindwe kutimiza lengo la ibara ya 18 ya katika ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na vile vile kutengeneza mianya yakifisadi zaidi kwa watumishi wa umma kwa maana hakuna wa kufichua maovu na hatima yake kuifanya nchi kuwa pango la walanguzi.
Napenda kuliomba bunge letu tukufu kuhakikisha linapitia upya sheria ya magazeti ya mwaka 1976 Sheria ambayo licha ya kuwa ya muda mrefu pia ilitajwa kwenye tume ya Jaji. FRANCIS NYALALI kuwa ni sheria kandamizi,lakini hawa watawala wetu hawakuwahi kuitazama sheria hii na badala yake kuendelea kuitumia pamoja na maozo yote hayo.
Watanzania wenzangu tutambue kua mabadiliko katka taifa letu yatakuja kupitia juhudi zetu wenyewe Embu tuwatazame wachina walivyopiga hatua ingawa katka miaka ya 1960s tulikuwa sawa katika maendeleo tazama vile vile malaysia nchi ambayo haina tofauti kabisa na Tanzania katika historia na watu wake lakini tazama maendeleo waliyonayo kwa sasa. Tuamke watanzania tupigane juu ya taifa letu taifa ambalo nathubutu kiliita taifa teule kwa Mungu taifa ambalo linakila kitu ambacho mwenyezi mungu alisema Kiwepo ulimwenguni.
Salamu kwako Mh Raisi salamu zangu kwako zinaambatana na ujumbe wa kukuomba ubadili mfumo wa uongozi wako kwa maana hakuna linalokwenda sawia kama ambavyo watanzania wanavyota na kama ambavyo uliwahaidi awali,kuna hujuma na umimi ubaguzi na uroho wa mali na madaraka kila kitu ninachakachuliwa najua ni kipindi chako cha mwisho naamini hauna mawazo sana juu ya maswali ya watanzania kwa maana hautarudi tena kwenye uchaguzi.
Naomba kupitia hoja hii ufanye jambo kwa ajili ya taifa na ujiweke kando na viongozi wako wenye kukuaribia sifa na kupotezea heshima baada ya uongozi wako kumalizika ni jambo zuri kumaliza muda wako ukiacha watanzania wanakunenea mema una mipango mizuri mingi inatosha sasa chukua miaka hii miwili kuimaliza na kubadili mfumo wa chama na serikali kama vile ambavyo Mwl nyerere aliwataka mfanye katika kitabu chake cha "UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA" ...chukua hili usiliache liende zake.
Prepared by
Mwanaharakati(CGK).