dhamana ya vigogo KNCU,TCCCo yagonga mwamba

charles ndagulla

Senior Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
168
Reaction score
110
MAHAKAMA Kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na rushwa maafuru kama 'mahakama ya mafisadi' ,imetupilia mbali maombi ya dhamana ya vigogo wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro(KNCU) na vigogo wa Kiwanda cha kukoboa kahawa cha Tanganyika Coffee Curing(TCCCo).

Maombi hayo yalitupwa jana mjini Moshi na Jaji Winfrida Koroso,baada ya juzi kutumia saa tatu kusikiliza maombi ya dhamana ya washitakiwa hao yaliyowasilishwa na mawakili wao,Julius Semali,Capt.Sawayael na De Souza.

Kabla ya kutolewa uamuzi,jamhuri iliwasilisha hati ya kiapo ya kupinga dhamana kwa washitakiwa hatua ambayo ilipingwa na mawakili wa utetezi kabla ya leo kuhitimishwa na uamuzi wa kutupwa kwa maombi hayo.

Vigogo wanaotuhumiwa kuisababishia hasara KNCU ya Bil.2.9 ni Aloyce Kittau aliyekuwa mwenyekiti na aliyekuwa makamu wake,Khatibu Mwanga pamoja na meneja wao,Honest Temba.

Kwa upande wa vigogo wa TCCCo wanaoshitakiwa kwa kukisababishia hasara kiwanda hicho ya zaidi ya Bilioni moja ni aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi,Maynard Swai na aliyekuwa meneja wake,Andrew Kleruu.

Hao wanadaiwa kununua mtambo feki wa kukoboa kahawa,TCCCo inamilikiwa kwa aslimia 54 na KNCU huku vyama vingine vya ushirika ikiwamo ACU ya Arusha vikimiliki aslimia 46.

Uamuzi huo unamaanisha kwamba,washitakiwa hao wataendelea kusota rumande katika Gereza Kuu la mkoa wa Kilimanjaro,Karanga hadi hapo mashauri yao yatakpofikia hitimisho la kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
 
safi sana hatibu mwanga mdhulumaji ,alizoea kudhulumu hadi damu za wanyonge malipo ni hapa hapa dunia .walizoea kuifanya KNCU kama mali ya familia zao
 
Back
Top Bottom