Roho ya korosho haitakufikisha popoteHuyo Mo ni mtoto wa Ghulam Dewji, muda mwingi baba anahangaika na kampuni yao nchini Mo alikuwa masomoni nje ya nchi. Amerudi amekuta kampuni imeimarika kwa juhudi za baba yake na ndugu zake wengine. Kinachonishangaza ni kuona kila siku, anatajwa Mo badala ya mzee Ghulam. Bila shaka siasa ilimpa umaarufu lakini siye aliyeleta mali katika Mohamed Enterprises.
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’ kutoka katika Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) ametajwa kuwa `Kinara wa Uchumi’ barani Afrika, akishika nafasi ya kwanza ya tuzo miongoni mwa kundi la wafanyabiashara vijana 100 waliotambuliwa na Taasisi ya Choiseul ya Paris nchini Ufaransa.
Kwa miaka mitatu mfululizo, taasisi hiyo imekuwa ikitambua na kuanika orodha ya vijana 100 vinara wa biashara Afrika, wanaotarajiwa kung’ara miaka ijayo, na mwaka huu, Dewji ndiye aliyeibuka kinara.
Kwa tuzo za mwaka huu, Choiseul ilishindanisha wafanyabiashara hao wa Afrika kwa vigezo vya uraia katika mojawapo ya nchi 54 za Afrika, waliokuwa na umri wa miaka 40 au chini ya hapo hadi Januari Mosi, 2016, lakini walio na nguvu kibiashara, huku wakichangia kwa kasi maendeleo ya uchumi wa Afrika.
“Nina furaha na ninajiona mwenye bahati kubwa, kutambuliwa kwa kazi yangu ya kuinua uchumi wa kampuni ninayoiongoza, uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla, katika kipindi chote nilichojikita katika biashara, nimepata mafanikio makubwa, na kupitia MeTL, nitaendelea kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiuchumi barani Afrika kupitia sekta binafsi.” Amesema Dewji.
Aidha, aliuelezea ushindi huo kuwa ni kielelezo cha jinsi Tanzania na watu wake wanavyopigana kuinua uchumi wao na Afrika kwa ujumla.
Tangu alipoanza kuiongoza MeTL mwaka 1999 ikiwa na utajiri wa dola milioni 30 (Sh bilioni 63), kampuni hiyo imepata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania, na kufikia mwaka 2014 ilikadiriwa kuwa na utajiri wa dola za Marekani bilioni 1.3 (Sh trilioni 2.7).
Hakuna shaka kwamba kutokana na umri wa miaka 41 tu alionao bilionea huyo kijana zaidi barani Afrika, kuna uwezekano mkubwa wa kuzidi kupaa katika mafanikio kupitia biashara zake katika nchi 11 Afrika, zikiwemo za benki, viwanda vya sukari, nguo, mashamba makubwa ya biashara, ikiwa ni pamoja na katani, chai, korosho na kadhalika.
Chanzo: Hivi Sasa
Ni kweli mkuu....nadhani wanaangali Mkurugenzi mtendaji wa kampuni husika, hisa alizo nazo na sio alie anzisha au kukuza kampuni....Huyo Mo ni mtoto wa Ghulam Dewji, muda mwingi baba anahangaika na kampuni yao nchini Mo alikuwa masomoni nje ya nchi. Amerudi amekuta kampuni imeimarika kwa juhudi za baba yake na ndugu zake wengine. Kinachonishangaza ni kuona kila siku, anatajwa Mo badala ya mzee Ghulam. Bila shaka siasa ilimpa umaarufu lakini siye aliyeleta mali katika Mohamed Enterprises.
Mkuu wakati wengi wanaanzisha kampuni kwa kukata leseni ya kwanza wenyewe, kufungua mlango wa biashara wenyewe... jamaa alikuta 30m $... ambazo zimerekodiwa mwaka 1999.... Mungu akupe nini....baba ndio msingi wa kila kitu kwa METL
Ni MTZ haswa na ameajiri waTZ zaidi ya watu 24,000.......... Mkuu upo JF mda mrefu na michango yako inafaida, Bora ubadilike na mawazo ya ki''' Kubali ukweli !!!huyo mhindi siyo mtanzania
Si kweli mkuu, ndio kampuni ni ya baba yake ila ilikuwa haifanyi vizuri kabla ya ujio wa mo, tafuta kipindi cha mkasi mo alihojiwa na salama umsikilize, mo ameweza kuongeza product na kuzalisha ajira zaidi ya ma elfu tangu amekabidhiwa kampuni, akisifiwa ni haki yake. Tafuta kipindi U tube uangalie hutasema ulicho sema, inaweza kuwa mzazi kajenga nyumba ya kawaida ila mtoto aka i renovate na kuifanya na muonekano mzuri zaidi nani atasifiwa? Tumpe Mo haki yake amefanya kazi kubwa anastahili taji hilo.Huyo Mo ni mtoto wa Ghulam Dewji, muda mwingi baba anahangaika na kampuni yao nchini Mo alikuwa masomoni nje ya nchi. Amerudi amekuta kampuni imeimarika kwa juhudi za baba yake na ndugu zake wengine. Kinachonishangaza ni kuona kila siku, anatajwa Mo badala ya mzee Ghulam. Bila shaka siasa ilimpa umaarufu lakini siye aliyeleta mali katika Mohamed Enterprises.
kama ni Mtanzania je Wahindi wanafanya nini kwenye kampuni za Baba yake Gullamu na kwanini Wahindi walipwe mamilioni halafu Watanzania walipwe 4000 kwa kutwa haijalishi una elimu gani hebu ni jibu utanzania wake unatoka wapi mpaka anawanyonya wenzie?Ni MTZ haswa na ameajiri waTZ zaidi ya watu 24,000.......... Mkuu upo JF mda mrefu na michango yako inafaida, Bora ubadilike na mawazo ya ki''' Kubali ukweli !!!
Ni MTZ haswa na ameajiri waTZ zaidi ya watu 24,000.......... Mkuu upo JF mda mrefu na michango yako inafaida, Bora ubadilike na mawazo ya ki''' Kubali ukweli !!!
Hongera MO !! wa Amini watakao amini.... asiye amini uhuru ni wake!! MO ongeza kasi....Figure za uongo hizi,si kweli....si kweli,nakataa...anything coming from Mo is exagerated as f.uck...siamini ujinga...
Mo anajenga persona based on lies,na sad enough uninformed people ambao ndio 90% ya population are buying into his crap..