Dewj amesema TP Mazembe wanafungika huko kwao vizuri tu

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
4,079
11,724
Mfanyabiashara na mdhamini wa zamani wa Simba, Azim Dewji ameitabiria makubwa klabu hiyo katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo mwishoni mwa wiki hii huko mjini Lumbumbashi.

Amesema Simba ya mwaka huu ni `moto’ na ina uwezo wa kuwang’oa Mazembe kutokana na kuundwa na wachezaji wenye vipaji na ari ya kupata matokeo chanya.

Dewji aliyeifikisha Simba fainali za Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) mwaka 1993, alisema kitu pekee kinachopaswa kufanywa na wachezaji na viongozi wa Simba ni kuondoa mchecheto wa mchezo na badala yake kuelekeza nguvu katika mchezo wa marudiano.

“Ni kweli Mazembe ni timu ngumu na kongwe. Ukiangalia ina historia kubwa Afrika na ndani ya miaka hii kumi tumeshuhudia ikitwaa ubingwa tofauti wa michuano ya CAF mara tano. Ni rekodi bora sana, lakini pamoja na ubora wao, nikiangalia ubora na uthubutu wa wachezaji wa Simba, naona vijana wetu wanaweza kufanya kweli.

“Wachezaji wa Simba nawafananisha na wale wa enzi zile tunafika fainali CAF. Walikuwa wanajituma uwanjani. Na hawa ukiwaangalia wana kila kitu kinachoweza kuwaduwaza Mazembe kwao.

Angalia walivyowakimbiza hapa Dar es Salaam, kwa kawaida Mazembe si wa kujiangusha hivyo, lakini uliona katika mchezo wa kwanza, walizidiwa sana ila bahati haikuwa kwa Simba.

“Hata hao wanaobeza penalti ya John Bocco watambue Simba hii ni moto wa kuotea mbali na usishangae kuona mpira umetangulia Lubumbushi na wachezaji wanakwenda kumalizia kazi ya kuandika historia zaidi kwa soka ya Tanzania,” alisema Dewji.
 
Yaani amesema Mazembe inafungika halafu kasahau kufikiria ya kwamba hata Simba nayo pia inafungika pia. Mechi iliyochezwa Dar es salaam hata Simba nao walikimbizwa pia na kukoswa koswa magoli mengi pia.

Kasahau record ya Simba hii kwenye mechi za away wanageuka kuwa nyau badala ya simba. Ukiachana na mechi ya Mbabane, mechi zilizofuata zote Simba imepoteza zote away.

Amesahau kuwa kwenye champions league ya msimu huu Simba imeifunga timu zote ndani ya uwanja wa Taifa kasoro Tp Mazembe peke yao, je hii inashindikanaje kuona kuwa Tp Mazembe ni mfupa mgumu kuliko nyama zote walizokutana nazo?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom