Devotha Minja wa ITV Morogoro

theoka

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
374
Reaction score
100
Nawapongeza sana CHADEMA kumteua huyu dada Ubunge Viti Maalum anastahili kwa kweli maana alikuwa jasiri kureport habari ambazo zingemtia matatani.

Tutammiss sana wapenzi wa ITV.
 
Sasa kati ya devotha minja na spencer lameck nani alistahili?
 
ITV wamrudishe sasa demu wa Sadiki nae si kashinda!!
 
Sasa kati ya devotha minja na spencer lameck nani alisyahili???

Kwi kwi kwi!!

Kwa hiyo Spencer Lameck abadilishwe jinsia sio??. Sisi tunaongelea viti maalum wewe unakuja na jini uchochezi na kuleta uozo hapa.
 
nawapongeza saaaana chadema kumteua uyu dada ubunge viti maalum anastaili kwakweli maana alikua jasiri kureport habari ambazo zingemtia matatani
tutammiss sana wapenzi wa itv

Mkuu sababu za kupewa ubunge Viti maalumu sijaziona au ndio hizi habari alizoandika ndio zilizompatia ubunge?
Kumbe kuna waandishi wa habari wanaofanya kazi za vyama vya siasa kwenye taaluma zao?

Hata hivyo walau tutajia hata hizo habari mbili tatu labda unaweza kutushawishi kukubaliana na hoja yako.
 
Sasa kati ya devotha minja na spencer lameck nani alisyahili???

Kwi kwi kwi!!
Unafanania na akili yako! Kama alalijitosa ubunge kura za maoni viti maalum mkoa na akashinda ulitaka nani awakilishe mkoa? Au ulitaka wewe upewe?
 


Shaaban Kissu alikuwa TBC akateuliwa Ukuu wa wilaya wala hakuna aliyehoji..
 
Shaaban Kissu alikuwa TBC akateuliwa Ukuu wa wilaya wala hakuna aliyehoji..

Kosa halihalalishwi na kosa lingine jibu hoja.
Kwa majibu haya na mtazamo huu mnamtia matatani mmiliki wa kituo alichokuwa anafanyia kazi huyo aliyeteuliwa.
 
Eti mtu anashangaa mwandishi wa habari coz amechaguliwa chadema ila hashangai naibu mwanasheria mkuu wa serikali kugombea uspika kwa mlango uleule wa chama.
Kwi kwi kwiiiiiii
 
Kosa halihalalishwi na kosa lingine jibu hoja.
Kwa majibu haya na mtazamo huu mnamtia matatani mmiliki wa kituo alichokuwa anafanyia kazi huyo aliyeteuliwa.

Deo Filikunjombe, Betty Mkwasa, Mwigulu Nchemba walishafanya kazi IPP..
 
Ubini ni Minja wa kaskazini kwanini asipewe ubunge??
 
Wakati mwingine inabidi watanzania tuwe wapole tu,maana hatujapata kabisa chama cha kutuletea mabadiliko;hakika hii nchi imejaa udini,ukabila, na kila aina ya vitu vyote alivyowahi kuvikataa na kuvipiga vita His Excellency The Father Of The Nation,hakika ndivyo vinashamili sana katika nchi hii,binafsi sishangai kabisa kwa haya yanayoendelea ndani ya CHADEMA, chama kimeshakuwa cha kujuana tu,dah.

Kitu ambacho kinanithibitishia kuwa hiki chama ni cha kujuana ni huu mgogoro wa utata wa matokeo ya kura za ubunge mjini Shinyanga kati ya Katambi(CDM) na Masele(ccm),baada ya kura kuchakachuliwa hadi basi na hatimae goli la mkono kwa Masele,kama alivyofanya mwaka 2010;utata uliopelekea kifo tata cha aliyekuwa mgombea ubunge CDM Bw,Shelembi ambapo alifariki katika utata wa hali ya juu na muda mfupi kabla ya hukumu ya kesi ya matokeo kusomwa katika mahakama ya kanda ya Tabora. Chadema wanaujua kabisa utata huu na wanajua kabisa sasa ni mara ya pili uchafu huu unafanyika tena na mtu yuleyule,lakini nachoshangaa hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu katika chama hicho ambaye angalau ameonekana kuguswa na tatizo hilo;hakuna hata mmoja anayelizungumzia suala la Katambi.

Lakini pia katika hali isiyo ya kiutu na isiyo ya kistaarabu ni hii hapa;kufuatia kifo cha aliyejitosa katika kinyang'anyiro cha ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka 2010,Bw.Philip Shelembi Magadula(r.a.u),kuna jengo ambalo lipo kwenye usawa wa lenta na walimuahidi mjane wa Shelembi kuwa watalishughulikia,lakini hadi leo liko vilevile,hali ya kuwa marehemu alikufa katika front line ya kukipigania chama. Hii inatia uchungu sana!

Bora yake hata Dr alivyojiengua mapema kabisa baada ya kuona na kuutathmini kwa uyakinifu mkubwa unafiki unaoendelea kwenye chama hicho,wakati yeye mwenyewe amepata kilema kwa ajili ya CDM,na kama haitoshi,mkewe amepata mshono kwa ajili ya CDM,halafu leo hii kiurahisi kabisa wanasimama majukwaani peupe kabisa na kumtetea na kumsafisha mtu ambaye kila leo walikuwa wakisema Fisadi,duh! Hela kweli noma,lakini vitu kama hivi kamwe haviwezi kuleta mabadiliko hatasiku moja,labda kwa maneno na maandishi;si kwa vitendo!

WITO WANGU;kutokana na kupitishwa kwa sheria ya maokosa ya mitandao,sina budi kuwa na staha,lakini pia naamini kuwa siku zote katika taifa hili wanaosema ukweli huwa hawakawii kurudi mavumbini good example ni kama kina Mwangosi,hivyo basi katika mantiki hii,bado hainizuii kuandika ukweli kama huu;ukweli unaozungumzika na ulio wazi kabisa. CDM si chama tulichokuwa tunakifikiria,kimekuwa cha wapiga 'deal' tu,hakuna chochote cha ukombozi wala nini,'otherwise'viva Devotha Minja viva,wewe ingia mjengoni,piga noti kama kawaida na ili kuondoa adha ya kukuzungumza hawa CDM,changia hoja kimtindo ili kuwaonesha kuwa hawakukosea kukuchagua,but kiukweli uchagga wako,ndo kigezo kwao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…