Devota Minja aweza kuwa mbunge bora kabisa wa viti maalum

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,666
239,164
Kwanza naomba nikiri kwamba simfahamu mheshimiwa huyu bali nimemsikia kidogo siku za nyuma akiripoti kwenye vyombo vya habari , inasemekana ni mwandishi wa habari .

Lakini tangu ateuliwe kuwa mbunge ameanza kazi kwa kasi ya ajabu na mtakubaliana na mimi kwamba huyu mama ni mchapakazi haswa, ghafla sana amekuwa tegemeo la wanyonge wa morogoro !

Amekuwa mtetezi wa wanaobomolewa hovyo na tumeona akishirikiana nao kunusuru nyumba zao , hivi karibuni ameonekana kwenye vyombo vya habari akikusanya kero za wananchi kwenye vijiji vya Mvomero ili aziwasilishe bungeni , huyu ni mbunge wa kuigwa .

Wananchi wa Morogoro wanajuta kwanini Mh huyu hakuwa mbunge tangu miaka ya nyuma maana wanaamini Morogoro ya leo isingebaki hivi ilivyo .

Hongera mheshimiwa , hongera CHADEMA kwa kuiona lulu ya Morogoro .
 
Ni ukombozi mkubwa mno kwetu Mji kasoro bahari, Yaani tumepata mtendaji, nadhani shahada yake ya SUA imemweka ulingoni, kisiasa zaidi kwa kujali maslahi za wananchi
 
Ni ukombozi mkubwa mno kwetu Mji kasoro bahari, Yaani tumepata mtendaji, nadhani shahada yake ya SUA imemweka ulingoni, kisiasa zaidi kwa kujali maslahi za wananchi
hongera sana wana morogoro
 
ana shahada ya SUA? ilikuaje akawa mwandishi wa habari?
Ninavyofahamu mimi alikuwa akiendelea kupiga kitabu SUA huku akiripoti matukio na kuandika habari, hivyo kwa nafasdi hiyo aliyoipata bila shaka Wananchi wa Morogoro wamepata kiungo mpiganaji. Mbunge, mwandishi wa habari, mtetezi wa wananchi. Hapo unakutana na wananchi live, repoti za picha video sauti vyote unavyo, kisha wakawakilishiwa hoja zao Mjengoni,,,......
 
morogoro hiyo kamanda .
Yap naelewewa ni moro, ila nilitaka kujua iweje wabolewe hovyo? au ndo ile kibongo bongo kutekeleza sheria ni kuonea watu? wanajua kabisa wamejenga barabarani lakini leo inaonekana uonevu kuwabomolea?
 
Kwanza naomba nikiri kwamba simfahamu mheshimiwa huyu bali nimemsikia kidogo siku za nyuma akiripoti kwenye vyombo vya habari , inasemekana ni mwandishi wa habari ,

Lakini tangu ateuliwe kuwa mbunge ameanza kazi kwa kasi ya ajabu na mtakubaliana na mimi kwamba huyu mama ni mchapakazi haswa, ghafla sana amekuwa tegemeo la wanyonge wa morogoro !

amekuwa mtetezi wa wanaobomolewa hovyo na tumeona akishirikiana nao kunusuru nyumba zao , hivi karibuni ameonekana kwenye vyombo vya habari akikusanya kero za wananchi kwenye vijiji vya mvomero ili aziwasilishe bungeni , huyu ni mbunge wa kuigwa .

Wananchi wa Morogoro wanajuta kwanini Mh huyu hakuwa mbunge tangu miaka ya nyuma maana wanaamini morogoro ya leo isingebaki hivi ilivyo .

Hongera mheshimiwa , hongera chadema kwa kuiona lulu ya morogoro .
Mchagaaa....!!!?
 
Nafikiri huu ndio wakati wa kujifunza kwa watu wa Moro na kwingineko kuwa kuchagua watu matajiri kama Aboud na wengine eti kwa kigezo kuwa kukiwa na msiba anatoa sanda, mchele,sukari na kusaidia usafiri ni mawazo ya kijima kabisa.
Mfano pia ni pale Singida, eti Dewji aliposema hagombei tena watu wakatoa machozi! Ujinga gani huo? Dewji hata Bungeni haendi bali akienda siku mojamoja jimboni anaenda na lori limejaa sukari ya kugawa na kama kuna kikao cha madiwani atawagawia posho ya ziada yeye. Ona sasa maendeleo yame piga breki miaka mitano, hakuna kitu.
Devota ndio wabunge wa kizazi hiki wanaotakiwa
 
hivi karibuni ameonekana kwenye vyombo vya habari akikusanya kero za wananchi kwenye vijiji vya mvomero ili aziwasilishe bungeni , huyu ni mbunge wa kuigwa .
.
Yaani abebe hizo kero apande bas la ABOOD hadi dodoma kupeleka hizo kero kwani hapo morogoro hakuna viongozi wa serikali wa kusikiliza hizo kama ni kero au la na kuzitolea majibu? Au anataka kuuza sura kwa kuonekana kwenye TV akongea dodoma?

Anaenda kupoteza muda kwa kupeleka Dodoma wakati jibu angepata hapo hapo morogoro.

Mambo kama haya inabidi yakiulizwa ni vizuri waziri aulize kama mleta hoja alishapeleka hiyo kero kwa serikali ya mkoa? Na kama alijibiwa alijibiwa nini ili kuondoa maswali ambayo yangejibiwa mkoa husika mtu kuyapeleka bungeni.Bunge linajikuta lina maswali 100 ya kujibu wakati yangepata majibu mikoa husika lingekuwa labda na swali moja tu la kujibu.
 
mkuu umeishia darasa la ngapi ?
 
Nafikiri huu ndio wakati wa kujifunza kwa watu wa Moro na kwingineko kuwa kuchagua watu matajiri kama Aboud na wengine eti kwa kigezo kuwa kukiwa na msiba anatoa sanda, mchele,sukari na kusaidia usafiri ni mawazo ya kijima kabisa.
Mfano pia ni pale Singida, eti Dewji aliposema hagombei tena watu wakatoa machozi! Ujinga gani huo? Dewji hata Bungeni haendi bali akienda siku mojamoja jimboni anaenda na lori limejaa sukari ya kugawa na kama kuna kikao cha madiwani atawagawia posho ya ziada yeye. Ona sasa maendeleo yame piga breki miaka mitano, hakuna kitu.
Devota ndio wabunge wa kizazi hiki wanaotakiwa
kuna tetesi kwamba wajumbe wengi wa nyumba 10 wanalipiwa ada za watoto wao na wabunge ! halafu kule Temeke kuna mbunge kila penye msiba alikuwa anapeleka ndoo moja ya mafuta ya kula na kiroba cha mchele , na alikuwa anarekodi kila alichotoa na kila aliyempa na alikuwa akiwataja kwenye kila mkutano wa kura za maoni ili wampitishe tena .
 
Back
Top Bottom