1.
Asprin.
Huyu jamaa kwanza ni swahiba wangu. Kwa wasiomkumbuka alikuwa anaitwa Chrispin enzi zilee. Anapenda sketi saana saana. Kuna siri kibao nimemfichia kwa shemeji yangu kiasi kwamba akinimind tu nasema na ataachika soon.
Anapenda kuongea pumba saana na ukifuatilia post zake utaishia kucheka.
MO11 anatabia zinazofanania na huyu ila sema mo11 mdomo wake mzito


. Ila wapo smart saana wawapo serious.
2.
Shunie. Haka kadada ka tanga aseeh kanachekesha saana. Kwanza muda wote kapo online JF nafikir mchuchu wake anakaribia kufilisika

kwa bundle.kama hakanunuliwi bundle kaje kabishe hapa.
Ukikatania kukatongoza basi katakujibu kwa unyonge hadi unakaonea huruma. Nafikiri kanaheshimu mahusiano yake maana viwembe wa jf kama
Saint Ivuga ameshindwa kukachukua.